Wakazi: Diamond Platnumz ni maarufu ila hajui kuimba, "ukweli unauma mpaka mnanipigia simu za vitisho"

Wakazi: Diamond Platnumz ni maarufu ila hajui kuimba, "ukweli unauma mpaka mnanipigia simu za vitisho"

Sisi tunataka kujua huo umaarufu kaupata wapi ikiwa hajui chochote kwenye kuimba, kama mnavyodai?

Hao wanaojua kuimba ni nani na nani? Watajeni hapa kisha mtueleze kwanini wao sio maarufu kama Diamond.

Kuwa mwanamziki sio kujua kuimba tu, ukiachana na kuimba Mond kawazidi wengine vitu vingi sana kuhusu mziki.

Kuhusu wakazi, ni moja kati ya wasanii ambao wamedumu kuwa ma-underground kwa miaka mingi sana.
Ktk maisha iko kitu kinawezekana ndio maana kuna msemo mchumia juan ula kivuli ,unapofanya kaz kwa juhud mwanzo ukafanikiwa basi ni rahis sana kula matunda kwa muda mref ikiwa tu na akir ,ukwel ni kwamba diamond ni msanii mzur tena sana ila pia amejaliwa na maarifa pamoja na uwezo binafsi ,tukirud ktk muzik kiukwel kuna kiwango kinapungua ktk utunzi mpaka uimbaji japo kipato kinazid kwa sababu tu ya njia aliyojitengenezea ,

Tuwe tu silias iv kwel kuna mfanano kati ya ile kesho au nataka kulewa ,na hii labda fine au unachazaje ,na iyo sio kwa diamond tu kwa watu weng ambao walishatengeneza njia mwsho wake wanabebwa na jina au taasisi au kampuni mfano mzee bakhresa sasa iv hana muda ata wa kuanzisha ktu kipya kama sio jina lake au kampun yake kumbeba leo hii ata p square hawapo vzur ila ni rahis kurud na kushika chat kuliko msanii mpya ambae anaanza ,ni siri za maisha tu lkn usikute diamond sasa iv anaingiza pesa nyng kupitia njia nyngne nje muzk anaotoa ,yote kwa yote mzk ndio chanzo cha umaarufu wake ila haimaanish yeye ndio anaejua kuimba vzur kupita wengine ama kutoa hits song kupita wengine
 
Hip hop imemshinda sasa anataka uanaalakati anazani atateuliwa km niki wa pili
Uteuzi na uwanaharakati hauwez na hatopata sabubalishakosea chama
Moja yan sababu inayosababisha watanzania tubaki maskini ninkitendo cha kutokueshimu na kukubali

Leo unakuta mtu km mbunge msukuma anamponda mbunge profesa muhongo wakat hao watu hawafanai wala hawaendani na mtu km profesa muhongo kujibixana na msukuma ni kupoteza mda
Ila ndo watanzania tunataka alieko juu tumshushe kwa njia yyte
 
Wakazi yuko sahihi Diamond hata atoe ngoma ya dakika mbili halafu humo ndani awe anacheka mwanzo mwisho utaona ngoma hiyo itavyokuwa trend na usikute ikapewa na tuzo

Hayo yote yamerahisishwa kutokana na jina (umaarufu) na ndio maana hata hawa ma underground wana amini wakipata nafasi ya kufanya kazi kwenye lebel yao watatoka tu, kwasababu kitachowafanya wajulikane sio ubora wa kile wanachokiimba

Means hata kwa level zao za huku chini wanaamini hata wakaze msuli namna gani bado ubora wa nyimbo hautakuwa kigezo wao kutoka

Nakubaliana na Wakazi
Iyo ni kwl kak
 
Unaweza ukajua kuimba ila husiwe mkali, unaweza kuimba kawaida na ukawa mkali huku ukipiga hela ndefu. Tanzania Bongo Star Search inatoa wasanii wakali wanaojua kuimba, tatizo baadae hawaji kuwa wakali.

Nakumbuka Akon wakati akiwa Jaji wa shindano lilio andaliwa na Airtel ambalo, Mayunga alishinda. Wakati wale majaji wanaongea, ikafika zamu ya Akon, Akon alisema yy hayupo pale kumtafuta muimbaji bora, bali mburudishaji bora.

Master J anasemaga mara kibao BSS, unaweza kumfundisha mtu kuwa mwimbaji na kufikia hatua ya kuwa mwimbaji mzuri, ila huwezi kumfundisha mtu kuwa mburudishaji (entertainer).

Mondi si muimbaji mkali, bali ni mtunzi mzuri tu, ana vision ya mziki kibiashara na mwisho ana sifa ya mburudishaji bora akiwa jukwaani ambayo wengi hawana halafu ana jijulia aina za nyimbo za kuimba.
 
SAWA SWALI NI KWAMBA HAOOO WANAOMZIDI KUIMBA, HAO WENYE MELODY NZURI, HAO WENYE TUNGO KALI NA SAUTI YA KUVUTIA MBONA HAWAFIKI POPOTE??? MBONA KAZI ZAO HAZISONGI KAMA ZA HUYO WANAEMKOSOA???

NAJUA MNAJUA, NA TUNAJUA MNAJUA TUNAWAPIGAJE MNAJUA😂😂😂
Mkuu Diamond ni mwimbaji wa kawaida tu, hayo mengine mtatoana macho kisa ushabiki wenu
 
Msanii kutoka Tanzania, Wakazi amesema kwamba Diamond Platinumz ni maarufu ila sio mzuri katika uiambaji.

Kupitia ujumbe aliochapisha kwenye ukurasa wake wa Twitter, Wakazi alisema kwamba kuna tofauti kubwa kati ya umaarufu na ubora wa msanii, na hivyo kuwa maarufu haimaanishi kuwa mzuri katika sanaa ya muziki.


======
Yeye je?!
 
Msanii kutoka Tanzania, Wakazi amesema kwamba Diamond Platinumz ni maarufu ila sio mzuri katika uiambaji.

Kupitia ujumbe aliochapisha kwenye ukurasa wake wa Twitter, Wakazi alisema kwamba kuna tofauti kubwa kati ya umaarufu na ubora wa msanii,

======


Pia soma: Diamond Platnumz ahoji kwanini Ali Kiba (mkongwe) hana media yake? Atoa onyo kushindanishwa na wasanii wa Tanzania 'ni wadogo sana kwake'
Kitu ambacho Wakazi hajui ni kwamba, uzuri wa kitu kipo kichwani mwa mtu na hata uzuri wa sauti upo masikioni mwa mtu hivyo asilazimishe kile anachosikia yeye , ubaya anaousikia yeye ndio uzuri anaousikia mwingine. Ni sawa na msichana mrembo unamtambua pale unapomuona, mwingine atamuona mbaya wewe utamuona mzuri. Hivyo kadri kazi za Diamond zinavyotembea ndio zinadhihirisha uzuri wake na ubora W wake.

Mziki wa sasa unaangalia soko lilivyo, soko la sasa ni tofauti na miaka 10 nyuma. Sasa mnamlazimisha abaki miaka 10 nyuma atauzaje mziki wake? Naamini anajua wasanii wazuri kwa mawazo yake, je kwa nini wadau akiwa na yeye mwenyewe awaendi kuwekeza huko? Aoni akiwa na msanii wake mzuri na bora kwa mtazamo wake atapiga hela nyingi, kwa nini asiingie huko? Mziki umebadilika duniani kote leo muangalie CARD B, 6ix9ine wanaimba nini, je mashairi yao ni bora kuliko NAS? Lakini nani anaingiza hela nyingi? 6ix9ine na NAS nani maarufu na nani bora?

Suala la msanii yeyote akienda kwenye label ya Diamond lazima atoke, ni kweli kwa sababu amewekeza kwenye biashara na afanyi ilimradi tu. Ni sawa na shule, ukiwekeza vizuri kwenye shule yako utafaulisha tu. Ndio maana shule bora na nzuri wamewekeza ikiwa ni pamoja na mishahara mizuri. mfano Aslay na Mboso nani mzuri? Kwa nini Aslay anafeli, kwangu mimi kang'ang'ania uzamani.
 
Wakazi yuko sahihi Diamond hata atoe ngoma ya dakika mbili halafu humo ndani awe anacheka mwanzo mwisho utaona ngoma hiyo itavyokuwa trend na usikute ikapewa na tuzo

Hayo yote yamerahisishwa kutokana na jina (umaarufu) na ndio maana hata hawa ma underground wana amini wakipata nafasi ya kufanya kazi kwenye lebel yao watatoka tu, kwasababu kitachowafanya wajulikane sio ubora wa kile wanachokiimba

Means hata kwa level zao za huku chini wanaamini hata wakaze msuli namna gani bado ubora wa nyimbo hautakuwa kigezo wao kutoka

Nakubaliana na Wakazi
Sasa nini mnataka aimbe ma hardcore halafu hela wala umaarufu?ndio nini sasa... acheni wivu
 
Sasa nini mnataka aimbe ma hardcore halafu hela wala umaarufu?ndio nini sasa... acheni wivu
Sasa hapo wivu una husika vipi?

Kumkosoa mtu hakuwezi kuwa na maana ya wivu

Labda nikukumbushe tu kuwa hata huyo diamond kafanya interviews kibao ambapo humo kawakebehi watu na kuwashusha viwango, je na hiyo unaihesabu kama wivu?

Tukubaliane hapa, kwamba diamond naye ana wivu kwa wasanii wengine kwa kauli zake za kuwakosoa wengine kwenye interviews

Vinginevyo wewe utakuwa ni mnafki usiekuwa muungwana, na ni mtu ambaye unafata meza yenye bia nyingi kwasababu ya utimu.
 
Back
Top Bottom