KERO Responded Wakazi Keko Juu tuna shida kubwa baada ya Mkandarasi kukata mabomba ya maji kwa takriban wiki nzima

KERO Responded Wakazi Keko Juu tuna shida kubwa baada ya Mkandarasi kukata mabomba ya maji kwa takriban wiki nzima

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Tunapenda maendeleo na tunaipongeza Serikali kwa juhudi zake za kuboresha miundombinu kupitia ujenzi wa barabara za mitaa. Hata hivyo, si vyema mradi unaolenga kuwaletea wananchi maendeleo ukageuka kuwa chanzo cha mateso kutokana na utendaji usioridhisha wa mkandarasi.

Wiki iliyopita mkandarasi (CRJE) alianza kazi ya ujenzi wa mtaro wa kupitisha maji eneo la Keko Juu. Wakati wa uchimbaji, mabomba ya maji yalikatwa, jambo lililosababisha huduma ya maji kusitishwa katika mtaa mzima.

Kinachotusikitisha zaidi ni mwendo wa polepole wa kushughulikia tatizo hilo. Katika kipindi cha wiki nzima, mkandarasi amefika eneo la kazi kwa siku nne pekee. Aidha, hafanyi kazi siku za mwisho wa wiki, yaani Jumamosi na Jumapili. Hata siku anapofika, kazi huanza saa 4 au saa 5 asubuhi na kusitishwa saa 9 mchana.

Kutokana na hali hiyo, wakazi wa eneo hili tunaendelea kupata mateso makubwa. Kwa zaidi ya wiki moja sasa hatuna huduma ya maji kwa matumizi ya kawaida ya nyumbani. Kwa kasi hii ya utekelezaji wa kazi, tuna hofu kwamba tatizo hili linaweza kuendelea kwa muda mrefu zaidi ikiwa hatua za haraka hazitachukuliwa.

Soma Pia: Wakazi wa Ubungo Riverside, Kwa Novo hatuna maji mwezi wa saba sasa

Tunaziomba mamlaka husika kuingilia kati suala hili ili kuhakikisha mkandarasi anaharakisha kazi na kurejesha huduma ya maji kwa wananchi wanaoendelea kuathirika.

Pia soma ~ DAWASA: Tumerekebisha bomba lililopasuliwa na Mkandarasi Keko Juu na huduma imerejea
 
Back
Top Bottom