Maana miaka ya 1800 Sultani alianzisha kilimo cha karafuu Zanzibar. Biashara hii na ile ya utumwa ilikuwa ya pesa nyingi. Mwishowe akaamua yeye mwenyewe kuhamia Zanzibar.
Hapo waarabu kibao kutoka Oman wakahama naye. Wakaanzisha mashamba ya karafuu na kuweka watumwa kibao kufanya kazi. Hata leo wakazi wengi unakuta wanaasili ya wanyamwezi, wayao, hadi wamanyema kutoka Congo. Mababu zao walikuwa watumwa.
Sasa wakazi wa asili kabisa wa Zanzibar ni watu gani? Lugha yao ni ipi? Au kulikuwa hakuna watu, maana visiwa vingi vya bahari ya hindi vilikuwa haviishi watu miaka watu wameanza kusafiri huku na huko baharini.
Ni vigumu kuelewa historia ya visiwa vyote vya Indian ocean. Wengi walikuja kama siyo watumwa mfano wahindi, waarabu, wapakistani, washirirlanka na wengine toka visiwa ndani ya bahari ya indi. Walikuja waajemi, wachina na makabila mengi.
Wareno kalne ya 15 walipiga nanga Zanzibar wakaoana na wenyeji mazalia yakawepo bara hata pwani. Wakasafiri mpaka Zanzibar wakaacha alama meaning mazalia na majengo.
Ikumbukwe wachina walitangulia kuja earlier wakaacha ramani meaning ukienda zenj kuna familia moja naifahamu mama ni mweusi, baba ni chotara wa kiarabu lakini watoto wana uarabu, uchina na nywere kama za kibantu.
Wale wanaojiita wazanzibari ni mazalia ya watumwa. Wazanzibari wenyewe hawakuwa na kabila bali walijichanganya wenyewe .
Hao waimba matarumbeta wengi ni watoto wa askari waliotumwa 1963 kuua na kusambaratisha ustarabu uliokuwepo wa wazanzibari. Wazanzibari wana asili ya Wachina, waajemi, wareno, waarabu na wangazija. Bara walitoka kigoma kama watumwa wakapitia tabora, dodoma mpaka Zenj.