Sisi wakazi wa Buswelu Nyamadoke, eneo la Ibinza Msikiti wa Chini, Wilaya ya Ilemela Mkoa wa Mwanza, tunaomba Serikali na mamlaka husika kutusaidia kutufikishia mtandao wa mabomba ya maji ili nasi tuweze kuunganishiwa huduma ya maji safi na salama.
Kwa sasa, eneo letu halina mtandao wa mabomba ya maji licha ya mradi wa maji kufika maeneo ya Nyamadoke. Kutokana na hali hiyo, tunalazimika kununua maji kwa wauzaji wanaotumia baiskeli au kuchota maji kutoka kwenye visima, ambavyo mara nyingi si salama kwa matumizi ya binadamu.
Tunaiomba Serikali itazame changamoto hii kwa jicho la huruma na kuchukua hatua za kupeleka miundombinu ya maji katika eneo letu ili wananchi waweze kupata huduma muhimu ya maji safi na salama kwa urahisi.
Tunatanguliza shukrani zetu za dhati kwa kusikiliza na kufanyia kazi ombi hili.
Kunyweni tope kwanza .. Mshauri wa Afya wa Rais bado anatoa pongezi kule X Mtandaoni..baadaye sasa atamshauri Rais- Samuya muwekewe mabomba mnywe Maji safi muwe na Afya tele...ee..hureeee!??