Wakazi wa Bwawani Dodoma walalamika kunyanyaswa na diwani kisa kudai maendeleo

Wakazi wa Bwawani Dodoma walalamika kunyanyaswa na diwani kisa kudai maendeleo

Sijapewa username bado

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,775
Reaction score
2,891
Wananchi wa Kijiji cha Mlowa Bwawani, Wilaya ya Chamwino, Mkoa wa Dodoma, wamemlalamikia Diwani wa kata hiyo, Andrew Richard Mseya (CCM), kwa madai ya kutumia mamlaka yake kuwanyanyasa, kuwapiga, na kuwatoa vitisho pindi wanapodai maendeleo katika kijiji chao.

Wakizungumza na waandishi wa habari, wakazi hao wamesema wananyimwa uhuru wa kutoa maoni yao, hasa kuhusu masuala ya maendeleo. Wamedai kuwa Diwani huyo huwafuatilia, kuwanyanyasa, na hata kuwapiga wanapozungumza kwa uwazi kwenye mikutano au kupitia majukwaa mbalimbali.

Kwa mujibu wa mmoja wa wakazi hao, Abdulaziz Aboubakar, tukio la hivi karibuni lilitokea baada yake kuuliza maswali kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo kupitia kundi la WhatsApp la kata hiyo. Anadai kuwa kitendo hicho kilimkasirisha Diwani, ambaye baadaye alimtishia na hatimaye kumfuata na kumpiga.

"Nilihoji kwenye kundi la WhatsApp kuhusu maendeleo ya kijiji chetu, hasa kuhusu mali ambazo zilikuwepo ofisini lakini sasa hazipo. Nilishangaa kuona baadhi ya mali hizo zikiwa mtaani. Baada ya mazungumzo hayo, Mheshimiwa Diwani alinitafuta na kuniomba tukutane. Tulipokutana, maelewano hayakupatikana, ndipo akanipiga na kuninyang’anya laini za simu, kisha akazivunja," alisema Abdulaziz.

Tukio jingine linalodaiwa ni la Mzee John, mkazi wa kijiji hicho, ambaye inasemekana alipigwa na Diwani huyo hadi kuzimia.

"Mzee John alikuwa maeneo ya vijiweni, na inaonekana alikwaruzana na Diwani kwa namna fulani. Badala ya kutumia hekima, Diwani alimpa kofi moja kali hadi mzee huyo akazimia na kuanguka chini," alieleza mmoja wa mashuhuda.

Wananchi hao wamesisitiza kuwa wanahitaji kiongozi anayewajali na kuwatetea badala ya kuwanyanyasa.

"Kwa nini kiongozi ampige mwananchi? Ifike wakati viongozi watambue wajibu wao. Wamechaguliwa ili kututetea, siyo kutuumiza. Tukitoa kero, tunatishiwa. Wanatufanya tuogope kusema ukweli kwa kuhofia hatua kali," aliongeza mmoja wa wakazi.

Hata hivyo, Diwani Andrew Richard Mseya alipotafutwa kwa njia ya simu na mwandishi wetu, alikanusha tuhuma hizo, akidai hajawahi kufanya vitendo vya unyanyasaji kama inavyodaiwa.
 
Ndio madhara ya kuwa na chama dola
Kwa Sasa ukitaka mambo yawe magumu basi tofautiana na kiongozi wa ccm
 
Back
Top Bottom