Wakazi wa Geita walalamikia miundombinu duni

Wakazi wa Geita walalamikia miundombinu duni

Bawabu wa pili

Senior Member
Joined
Nov 14, 2025
Posts
147
Reaction score
433
Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini, Mhandisi Chacha Wambura, amefanya kikao kazi na zaidi ya wenyeviti 70 wa mitaa na vijiji kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Geita, kwa lengo la kusikiliza kero na mahitaji ya wananchi katika maeneo yao.

Katika kikao hicho, hoja zilizotawala ni changamoto za miundombinu ya barabara, upungufu wa miundombinu ya elimu, upatikanaji wa maji safi na salama, pamoja na uboreshaji wa huduma za afya.


Wenyeviti hao wameeleza kuwa maeneo mengi bado hayana barabara za uhakika, hali inayosababisha ugumu wa usafiri hasa nyakati za mvua. Pia, wamebainisha kuwa baadhi ya mitaa haina shule, jambo linalowalazimu wanafunzi kutembea umbali mrefu kufuata elimu.

Mbunge Wambura ameahidi kushughulikia changamoto hizo kwa kuimarisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo, ikiwemo ujenzi na matengenezo ya barabara, kuongeza miundombinu ya elimu pamoja na kusimamia upatikanaji wa huduma bora kwa wananchi.
 
Back
Top Bottom