Wakazi wa Kigoma wainuliwa kiuchumi

Wakazi wa Kigoma wainuliwa kiuchumi

Nyabukika

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2022
Posts
1,440
Reaction score
1,046
Rais Samia Suluhu anaelekea kufanya ziara ya siku 3 mkoa wa Kigoma kwaajili ya kukagua shughuri mbali mbali za maendeleo.

Sasa tuangalie maendeleo mbalimbali yaliyopelekwa na serikali katika mkoa wa Kigoma

1. Tanzania ina vituo 17 vya uwezeshaji wananchi kiuchumi, 6 vipo mkoani Kigoma.
Mwaka 2021 viliwezesha wajasiriamali kukopeshwa TZS bilioni 5.4, fedha zilizobadili biashara na kuboresha maisha yao. Mhe. Rais Samia anataka kuwaona wanakuwa wafanyabiashara wakubwa.

2. Rais Samia Suluhu Hassan ametoa zaidi ya Shilingi Bilioni 52.9 kwa Mkoa wa Kigoma kwaajili ya Ujenzi wa Meli kubwa mbili, moja ya kubeba mizigo na nyingine ya kubeba abiria.

Pia Mhe.Rais Samia ametoa fedha kwaajili ya ukarabati na Maboresho ya MV Liemba na MV Miongozo.
Kukamilika kwa meli hizo kutarejesha Kigoma ktk uelekeo sahihi kiuchumi

3.Grid ya taifa kufika Kigoma
"Umeme wa Grid ya Taifa kufika Kigoma ina maana Shirika la Tanesco linaenda kuokoa kiasi cha sh. bilioni 22.4 kwa mwaka. Kupitia umeme huu umechochea shughuli mbalimbali za maendeleo

Yapo mengi yaliyofanywa na Rais Samia Suluhu katika mkoa wa kigoma.
 
Ila bado kigoma maskini wa kutisha unajua kigoma wanakusanya kodi TRA bilioni 10 KWA mwaka wakati Arusha wanakusanya bilioni 250 kwa mwaka?
 
Kigoma hauwezi kulinganisha na Arusha hata kidogo mji wenye biashara ya madini na utalii mwingi lazima uwe na uchumi wa juu pia so kigoma bado inaendelea na Rais Samia Suluhu anaendelea kupeleka maendeleo zaidi
 
Kigoma inajikongoja sana kwenye swala la maendeleo ni moja ya mikoa iliyo "sahaulika" kimaendeleo serikali iwakumbuke angalau kuleta wawekezaji wajenge viwanda itasaidia pakubwa
 
Mama amepakumbuka sana kigoma na kigoma kipindi hiki cha Rais Samia Suluhu kuwepo madarakani wajiandae kuramba asali
 
Miradi inayoendelea sasa hivi kigoma aliahidi magufuli na mingi ikaanza utekelezaji kabla hajafariki, hata gridi ya taifa aliacha imefika nyakanazi tusisahau hilo
 
Lakini nani amesimamia na imekamilika mzee, Rais Samia Suluhu alisema atahakikisha anamaliza miradi yote iliyoachwa na mtangilizi wake na amemaliza kwa wakati kwaiyo sioni shida hapo
 
Rais Samia Suluhu anaelekea kufanya ziara ya siku 3 mkoa wa Kigoma kwaajili ya kukagua shughuri mbali mbali za maendeleo.

Sasa tuangalie maendeleo mbalimbali yaliyopelekwa na serikali katika mkoa wa Kigoma

1. Tanzania ina vituo 17 vya uwezeshaji wananchi kiuchumi, 6 vipo mkoani Kigoma.
Mwaka 2021 viliwezesha wajasiriamali kukopeshwa TZS bilioni 5.4, fedha zilizobadili biashara na kuboresha maisha yao. Mhe. Rais Samia anataka kuwaona wanakuwa wafanyabiashara wakubwa.

2. Rais Samia Suluhu Hassan ametoa zaidi ya Shilingi Bilioni 52.9 kwa Mkoa wa Kigoma kwaajili ya Ujenzi wa Meli kubwa mbili, moja ya kubeba mizigo na nyingine ya kubeba abiria.

Pia Mhe.Rais Samia ametoa fedha kwaajili ya ukarabati na Maboresho ya MV Liemba na MV Miongozo.
Kukamilika kwa meli hizo kutarejesha Kigoma ktk uelekeo sahihi kiuchumi

3.Grid ya taifa kufika Kigoma
"Umeme wa Grid ya Taifa kufika Kigoma ina maana Shirika la Tanesco linaenda kuokoa kiasi cha sh. bilioni 22.4 kwa mwaka. Kupitia umeme huu umechochea shughuli mbalimbali za maendeleo

Yapo mengi yaliyofanywa na Rais Samia Suluhu katika mkoa wa kigoma.
Jambo jema....ngoja nidandie saratoga nikashuhudie
 
Gridi ya taifa kila siku umeme unakata kigoma wakazi wa kigoma wameyamis majenereta yao u me me ulikuwa haukatiki km unavyokatika kwa sasa
 
Back
Top Bottom