RESOLVED Wakazi wa Kijiji cha Maisha Plus wakubali kuhama kupisha kilimo cha Mkonge Wilayani Muheza

RESOLVED Wakazi wa Kijiji cha Maisha Plus wakubali kuhama kupisha kilimo cha Mkonge Wilayani Muheza

Imefanyiwa kazi au kupatiwa ufumbuzi na Mamlaka husika

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Kaya 67 zinazoishi kwenye eneo la maarufu la Maisha Plus la Kitongoji cha Bago, Kijiji cha Msakangoto na Kata ya Kigombe Wilayani Muheza wamekubali kulihama eneo hilo, kumpisha mwekezaji wake kuendeleza upanuzi wa kilimo cha mkonge.
MAISHA PLUS WAKUBALI KUHAMA KUPISHA KILIMO CHA MKONGE MUHEZANa Mashaka Mgeta, OMM TANGAKAYA 67 z.jpg

MAISHA PLUS WAKUBALI KUHAMA KUPISHA KILIMO CHA MKONGE MUHEZANa Mashaka Mgeta, OMM TANGAKAYA 67...jpg
Hatua hiyo imefikiwa baada ya ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dkt. Batilda Burian, aliyeongozana na Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Mhe. Ayubu Sebabili kufanya kikao cha wazi wakazi hao, kuwajulisha hatima yao.

Wakazi hao wanaoishi kwenye eneo hilo kwa madai ya kupewa na Serikali ya Kijiji cha Msakangoto, ingawa uongozi huo umekana kuhusika, wamekuwa katika mgogoro ambao hata hivyo, hatima yake ilifikiwa kupitia uamuzi wa Mahakama uliotoa ushindi kwa Mwekezaji.
MAISHA PLUS WAKUBALI KUHAMA KUPISHA KILIMO CHA MKONGE MUHEZANa Mashaka Mgeta, OMM TANGAKAYA 67...jpg

MAISHA PLUS WAKUBALI KUHAMA KUPISHA KILIMO CHA MKONGE MUHEZANa Mashaka Mgeta, OMM TANGAKAYA 67...jpg

MAISHA PLUS WAKUBALI KUHAMA KUPISHA KILIMO CHA MKONGE MUHEZANa Mashaka Mgeta, OMM TANGAKAYA 67...jpg

MAISHA PLUS WAKUBALI KUHAMA KUPISHA KILIMO CHA MKONGE MUHEZANa Mashaka Mgeta, OMM TANGAKAYA 67...jpg
Baada ya uamuzi huo, Mei 22, mwaka 2026, dalali wa mahakama alikwenda kutekeleza amri ya muhimili huo, kuwaondoa wakazi hao kwa kubomoa makazi yao, ili kuliachia eneo hilo.

Balozi Dkt. Batilda na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga, Rajabu Abdalla, walitoa msaada wa mahema na chakula wakati jitihada za kutafuta ukweli kuhusu tukio na umiliki wa eneo hilo vikifanyiwa,

Akizungumza kwa niaba ya wakazi hao, Dora Gambo amesema kufuatia uamuzi huo ni vema eneo wanalohamishiwa ndani ya siku saba walizopewa, haliingiliani na umiliki wa ardhi ya Mwekezaji, ili kuepuka migogoro inayoweza kutokea baadaye.

Mkazi mwingine, Ali Mohamed amesema suala la kuhama kwa sasa ‘halina mjadala’ na ombi lao ni kulipwa fidia, hoja iliyojibiwa na Balozi Dkt Batilda, kwamba fidia hiyo haipo kwenye uamuzi wa mahakama, ndio maana Mwekezaji akatoa Shilingi laki mbili kwa kaya, ikiwa ni kishamkono.

Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Timotheo Samwel, ameomba waruhusiwe kuondoa mali zao ili viwasaidie katika matumizi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa makazi.

Diwani wa Kata ya Kigombe, Shahongwe Mgandi amesema eneo wanalohamia lipo vizuri ikiwemo miundombinu iliyoruhusu kuendelezwa kwa mchakato wa huduma ya umeme kufikishwa kwenye eneo hilo.

Pia soma:
~
Kaya 67 za Msakangoto (Tanga) tumebomolewa makazi yetu, tunalala nje, tunaambiwa Mwekezaji atupe laki 2 tuondoke!
 
Back
Top Bottom