KERO Wakazi wa Kijombe, Wilaya ya Wanging'ombe (Njombe), kwenye huduma ya maji tunaisikia kwenye bomba

KERO Wakazi wa Kijombe, Wilaya ya Wanging'ombe (Njombe), kwenye huduma ya maji tunaisikia kwenye bomba

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Mwanongwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2023
Posts
611
Reaction score
567
Ukosefu wa maji safi na salama kwa sisi Wakazi wa Kata ya Kijombe, Wilayani Wanging'ombe imekuwa kero kubwa sana kwetu.

Kuna kipindi unapita mwezi mzima maji hayajatoka Bombani, hivyo tunalazimika kwenda kuchota wenye madimbwi huko mabondeni.
DSC_0207.JPG

Hii kero haijaanza leo, ni ya muda mrefu sana tumevumilia tumechoka jamani, Serikali liangalieni hili.

Wanafunzi wanakosa masomo sababu ya muda mwingi kuutumia kwenda kutafuta maji kwa ajili ya matumizi ya majumbani.
DSC_0205.JPG

Tunapata taatifa tu kuwa kuna Viongozi wanasema kuwa kwenye hii wilaya yetu maji yanamwagika Mwa mwa mwaaaaa, hivi wamefika kwenye Vijiji vya Lyadebwe, Lyamluki, Ukomola Kijombe na Ikwavila kujionea namna ambavyo wananchi tunapata shida.

Mfano mwezi wa Novemba 2024 tu, zimepita wiki mbili hatujapata maji hapa Kijombe, hatujui tatizo ni nini linasababisha mpaka maji yanakosekana kwa muda wote huo.
DSC_0211.JPG

Ukizunguka katika kata hii karibia kila nyumba imechimba shimo kwa ajili ya kuhifadhia maji, hivyo muda wote mipira ya maji inakuwa imeunganishwa na mabomba ilimradi tu maji yakitoka hata kidogo yapitilizekKwenye shimo.

Kibaya zaidi maji ni ya shida, ila hata yakitoka yanakuwa machafu hadi kupelekea kuziba chujio zilizopo kwenye mitaa na maji kushindwa kutoka.

Sasa tunajiuliza haya maji yanatofauti gani na ya kwenye madimbwi huko mabondeni maana maji yanatoka machafu balaa.
DSC_0209.JPG

Upande wa Halmashauri yetu ya Wanging'ombe inadaiwa zimetolewa fedha kiasi cha Shilingi Bilioni 43, lakini bado tunapata maji machafu na hayo machafu nayo tunayapata Kwa shida.

Hizo pesa mmefanyia nini sasa kama Wananchi bado tunapata msoto wa maji safi na salama.

Naomba niwakumbushe viongozi kuna muda wa siasa na muda wa kufanya kazi, tunaopata shida ni sisi Wananchi, siyo mnakaa kwenye vyombo vya habari mnakazana kudanganya watu kuwa mimaji mwa mwa mwa wakati hakuna cha maji wala nini.

Kwetu kuoga ni anasa na ule msemo wa kula lazima ila kuoga ni hiyari huku ni tofauti kidogo,kula ni lazima ila kuoga ni anasa.

Nawaibia siri sasa hasa ninyi watu wa Idara ya Elimu, jaribuni kufuatilia kwa ukaribu muone ni kiasi gani Watoto wanaacha shule na sababu kubwa ni hii kero ya maji.

Wanafunzi wengi wameacha shule sababu hawezi kwenda mabondeni kuchota maji asubuhi na mapema kisha akawahi shuleni, anaona bora kuacha shule na kuendelea na mambo mengine ,ndiyo maana wamejazana Makambako hapo wamekuwa Wafanyakazi kwenye maduka ya Wafanyabiashara.

Pia soma ~ Njombe: Kata ya Kijombe ukosefu wa Maji ni tatizo kubwa
 

Attachments

  • DSC_0210.JPG
    DSC_0210.JPG
    1 MB · Views: 6
Watafuteni viongozi wa huko popote walipo muwakande, mchome moto ofisi zao maana hazina maana.
 
Back
Top Bottom