A
Anonymous
Guest
Mheshimiwa Waziri Juma Aweso, Wakazi wa Kinyerezi, hasa Wakazi ambao tupo karibu na mitambo ya kuzalishia umeme ya Kinyerezi; tunasikitika kukiarifu kuwa hatuna huduma ya maji safi kabisa, leo ikiwa ni siku ya 3 tangu DAWASA walipositisha kutupatia huduma hii. Cha kushangaza zaidi ni kwamba wamesitisha kutupatia huduma ya maji bila kutupatia taarifa yoyote, wala hakuna mahali popote ambapo DAWASA wametoa taarifa ya kuhusu kukatika kwa maji katika maeneo haya, labda kwa sababu za matengenezo, au kwa sababu nyinginezo.
Mheshimiwa Waziri, tatizo la kukatika kwa maji mara kwa mara maeneo ya Kinyerezi, si geni, kwani tatizo hili limekuwepo muda mrefu. Katika maeneo haya, maji yamekuwa yakikatika mara kwa mara, wakati mwingine hata mara 2 kwa siku. Wakati mwingine maji yanaweza kukatika kwa siku nzima, siku 2, au hadi siku 3. Na mara baada ya kukatika, DAWASA wakati mwingine wanaweza kuamua kuyarejesha maji hayo usiku wa manane, halafu asubuhi wanayakata tena hadi hapo baadae watakapo amua kuyarejesha tena.
Tukiachana na tatizo la maji kukatika mara kwa mara; huduma ya maji tunayoipata wakazi wa maeneo haya si ya kuridhisha. Kwanza kabisa, msukumo wa maji tunaoupata ni mdogo sana kiasi kwamba wakati mwingine inawia vigumu maji hayo kuingia kwenye matenki ya maji. Lakini pia, wakati mwingine maji tunayo yapata wakazi wa maeneo haya yanakuwa si safi na salama kwa ajili ya matumizi ya binadamu.
Mheshimiwa Waziri, tunatambua ya kuwa una ufahamu juu ya changamoto ya maji katika eneo la Kinyerezi. Ndio maana katika ziara yako ya kukagua mtambo wa Ruvu juu uliyoifanya tarehe 28 Oktoba, 2024; uligusia changamoto za maji ulizo zisikia katika maeneo haya ya Kinyerezi na maeneo mengine na ukatoa maelekezo kuwa DAWASA wawajibike kwa kutoa huduma bora ya maji na waache visingizio. Pia ukatoa maelekezo kuwa Watendaji wa DAWASA waache kukaa ofisini. Waende mtaani wakakague na kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma ya uhakika ya maji safi na salama. Mheshimiwa Waziri, ninasikitika kukuarifu kuwa maelekezo uliyoyatoa kwa Watendaji wa DAWASA hayajafanyiwa kazi kabisa. Leo ikiwa ni siku ya 12 tangu ulipotoa maelekezo haya, sijawahi kumuona Mtendaji yoyote wa DAWASA akipita kufuatilia matatizo ya maji katika maeneo haya kama ambavyo ulielekeza. Kama DAWASA wangekuwa wametimiza wajibu wao na kutekeleza maelekezo uliyo yatoa, leo hii nisingekuwa na sababu ya kuandika malalamiko haya.
Mheshimiwa waziri, tunaomba uingilie kati na utusaidie kutatua kero hii ya maji katika eneo hili la Kinyerezi ambayo imekuwepo kwa muda mrefu.