KERO Wakazi wa Kisemvule - Mkuranga tulilipia gharama za umeme ikiwemo nguzo 4 lakini mpaka leo kimya

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Wakazi wa Kisemvule, Wilaya ya Mkuranga, Mkoa wa Pwani tumelipia umeme kwa kiasi cha Shilingi 320,000. Kabla ya kufanya malipo, alikuja surveyor ambaye alipima eneo letu na kutuambia kuwa ili umeme ufike tulipo, zinahitajika nguzo nne, ambapo kila nguzo inagharimu Shilingi 200,000.

Baada ya hapo, tulienda kufanya malipo, lakini cha ajabu ni kwamba tangu mwezi wa nane tulipolipia hadi leo, hatujaletewa umeme.

Tumeenda kufuatilia ili kujua tatizo ni nini, lakini tunaambiwa tutoe Shilingi 500,000 ili watuletee umeme. Pia, wanatuambia kwamba hakuna nyumba ya kupokea umeme katikati ya eneo hilo.

Hata hivyo, kabla hatujafanya malipo yoyote, surveyor alifika, akapima na kutuambia kuwa umeme unaweza kufika katika eneo letu.

Tunaomba msaada wako kuhusu changamoto hii.
 
Habari Ndugu mteja, asante kwa kuwasiliana nasi na pole kwa changamoto hiyo.

Tafadhali tuandikie namba yako ya ombi la umeme au namba ya malipo ili tuweze kufuatilia suala lako na kukupatia msaada zaidi.

Asante.^FL
 
Wakazi wa Kisemvule, Wilaya ya Mkuranga, Mkoa wa Pwani tumelipia umeme kwa kiasi cha Shilingi 320,000. Kabla ya kufanya malipo, alikuja surveyor ambaye alipima eneo letu na kutuambia kuwa ili umeme ufike tulipo, zinahitajika nguzo nne, ambapo kila nguzo inagharimu Shilingi 200,000.

Baada ya hapo, tulienda kufanya malipo, lakini cha ajabu ni kwamba tangu mwezi wa nane tulipolipia hadi leo, hatujaletewa umeme.

Tumeenda kufuatilia ili kujua tatizo ni nini, lakini tunaambiwa tutoe Shilingi 500,000 ili watuletee umeme. Pia, wanatuambia kwamba hakuna nyumba ya kupokea umeme katikati ya eneo hilo.

Hata hivyo, kabla hatujafanya malipo yoyote, surveyor alifika, akapima na kutuambia kuwa umeme unaweza kufika katika eneo letu.

Tunaomba msaada wako kuhusu changamoto hii.
Ndugu mteja tunaona bado hujaturudia na taarifa na kutupatia taarifa tulizokuomba.

Hata hivyo tunaamini taarifa zako ni za usiri na sisi kama taasisi tunatamani kukomesha vitendo hivyo, hasa kama kuna wafanyakazi wanahusika.

Kwa kutambua unyeti wa taarifa hizo, na mahitaji ya shirika kupambana na vitendo vya rushwa, tunaomba uwasilishe taarifa zako kwenye mfumo wetu wa usiri, kwa kubofya whistleblower .

Lakini, kama itakupendeza tutumie na sisi pia, taarifa zako za msingi kama namba yako ya ombi au namba ya simu kama tulivyoomba awali, kwaajili ya kuwezesha na kukamilisha huduma yako uliyowasilisha. Unaweza kutuma taarifa hizi kupitia inbox ndani ya jukwaa hili la Jamii Forums.

Asante. ^NI​
 
Nyie wakazi mmetumia nguvu nyingi kuleta kero zenu; mtatupatia mrejesho japa jf, mana bwana Tanesco wa jf amejitokeza kutoa msaada
 
Habari, ndugu mdau.

Ni kweli tumepokea taarifa kutoka kwa mteja wetu wa mkuranga. Hata hivyo kwasabau hakuna taarifa muhimu za mteja, tumemuomba aweze kutupatia taarifa hizo ilituweze kumfikia na kutatua changamoto yake.

Kama ulivyosema, Tanesco tumejitokeza, ni kweli. Tupo hapa tunamsubiria mteja wetu atupatie taarifa zake ili tuweze kutatua changamoto yake.

Asante. ^NI
 
Back
Top Bottom