Hili ni Bomba la Maji ambalo lina miaka kadhaa sasa halifanyi kazi, tunategemea maji ya kwenye visima.
Ukoefu wa Maji umekuwa na madhara kwetu Kiafya pamoja na kupata ugumu wa kutafuta maji safi, kwani tumekuwa tukiifuata huduma hiyo masafa marefu katika maeneo ya Milima na Mabondeni.
Tatizo hilo la Maji limesababisha hata wakati wa ibada kutokuwa rafiki kwetu na hivyo kusababisha wakati mwingine kuswali tukiwa maeneo ya mabondeni, ama kwenda misikiti ya Vijiji vya jirani.
Hata inapotokea misiba kuna muda tunapata hofu wa kujiuliza tutapata mapo Maji ya kumsitiri mwenzetu au wenzetu.
Kwa vile tilishakwenda kwenye Mamlaka husika kupeleka kilio chetu hicho, ni vyema Mamlaka kufika kijijini hapo na kufanya matengenezo ili kuona wanalipatia ufumbuzi tatizo hilo.