GE2025 Wakazi wa Mababu, Kyela wapata daraja lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 80

GE2025 Wakazi wa Mababu, Kyela wapata daraja lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 80

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
557
Reaction score
1,039
Changamoto iliyokuwa ikiwakabili zaidi ya wakazi elfu kumi wa Kata ya Mababu, Wilaya ya Kyela, mkoani Mbeya, ya kushindwa kutekeleza shughuli zao za kiuchumi na kijamii kutokana na mvua za Mapinduzi kukosa daraja na kujaa maji kipindi cha mvua, imepata suluhisho baada ya Serikali kujenga daraja lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 80.

Wananchi wa Kata ya Mababu walipokuwa wakizungumza na TBC, wameeleza kwamba walikuwa wakikumbana na changamoto kubwa kabla ya kujengwa kwa daraja hilo, hasa walipokuwa wakitafuta mahitaji yao, kwani iliwalazimu kuzunguka upande mwingine.

Kabla ya kujengwa kwa daraja hilo, eneo la Mababu mara kwa mara lilikuwa likikumbwa na mafuriko wakati wa mvua, hali iliyosababisha maji mengi kuingia katika makazi ya watu.

Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Wilaya ya Kyela, Mhandisi Salim Mtungata, ametoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo wa ujenzi wa daraja, akisema kazi za ujenzi zimekamilika kwa asilimia 100.

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa kwa mwaka huu, Ismail Ali Ussi, amekagua mradi huo na kuwasihi wakazi wa eneo hilo kutunza miundombinu ya daraja hilo.

Screenshot 2025-10-13 181550.png
 
Kazi ya ukandarasi inalipa sana kama kweli hilo daraja limegharimu hayo mamilioni.
 
Duuh.

Siku hizi milioni 80 imeshuka thamani sana.
 
Back
Top Bottom