KERO Wakazi wa Makuburi tunalalamikia Moshi wa Kiwanda cha Mkapa Export

KERO Wakazi wa Makuburi tunalalamikia Moshi wa Kiwanda cha Mkapa Export

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Wakazi wa Makuburi, ninaomba msaada kuhusu moshi unaotolewa na kiwanda cha Mkapa Export kuanzia asubuhi hadi usiku, unatuathiri sana sisi wakazi, lakini mpaka sasa hatujaona hatua zozote za kutusaidia.

Kinachotushangaza ni ukimya wa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, ambaye tunatarajia angefuatilia suala hili na kutoa taarifa kwa mamlaka husika, ikiwemo NEMC, ili hatua zichukuliwe.

Tunashuku kuwa baadhi ya viongozi wanapokea rushwa kutoka kiwandani ili wasifuatilie wala kutoa taarifa kuhusu changamoto hii. Tunaomba mamlaka husika zichunguze madai haya na kufuatilia athari za moshi huo kwa wakazi wa Makuburi.

Soma Pia: Kiwanda cha EPZD Benjamin Mkapa kinatukwaza kwa kelele wakazi wa Mabibo Hostel
 
Back
Top Bottom