Wakazi wa Makuburi, ninaomba msaada kuhusu moshi unaotolewa na kiwanda cha Mkapa Export kuanzia asubuhi hadi usiku, unatuathiri sana sisi wakazi, lakini mpaka sasa hatujaona hatua zozote za kutusaidia.
Kinachotushangaza ni ukimya wa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, ambaye tunatarajia angefuatilia suala hili na kutoa taarifa kwa mamlaka husika, ikiwemo NEMC, ili hatua zichukuliwe.
Tunashuku kuwa baadhi ya viongozi wanapokea rushwa kutoka kiwandani ili wasifuatilie wala kutoa taarifa kuhusu changamoto hii. Tunaomba mamlaka husika zichunguze madai haya na kufuatilia athari za moshi huo kwa wakazi wa Makuburi.