KERO Wakazi wa Miembeni, mtaa wa Msituni, Moshi hatuna gari la taka na hivyo taka zinazagaa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Wananchi wa Miembeni, Mtaa wa Msituni, tunakabiliwa na changamoto ya kutopatikana kwa huduma ya ukusanyaji taka katika eneo letu. Hali hii imepelekea baadhi ya wananchi kutupa taka ovyo, ikiwemo nyakati za usiku, barabarani na hata mashambani.

Utaratibu huo unahatarisha afya za wananchi na mazingira, pamoja na kuathiri usafi wa eneo.

Tatizo hili si la Mtaa wa Msituni pekee, kwani baadhi ya mitaa mingine pia inakabiliwa na changamoto ya utupaji taka ovyo, hali ambayo imekuwa kero kwa wakazi.

Tunaomba Manispaa ya Moshi kuchukua hatua na kuhakikisha huduma ya ukusanyaji taka inapatikana kwa wakati na kwa utaratibu katika maeneo haya.

Hatua za haraka zinahitajika ili kulinda usafi wa mazingira, afya na usalama wa wananchi.
 
kwa muda gani mmekuwa mnapitia cha

kwa muda mmekuwa mkipitia changamoto hio
 
Back
Top Bottom