DOKEZO Wakazi wa Muheza, Maili Moja – Kibaha tulilipa Tsh. 150,000 tupimiwe Viwanja, huu Mwaka wa 4 kimyaaa

DOKEZO Wakazi wa Muheza, Maili Moja – Kibaha tulilipa Tsh. 150,000 tupimiwe Viwanja, huu Mwaka wa 4 kimyaaa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Nyakijooga

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2018
Posts
276
Reaction score
473
Mimi ni Mkazi wa Kibaha Maili Moja, Mtaa unaoitwa Muheza, tangu Mwaka 2020 sisi Wakazi wa huku tulilipishwa kiasi cha Shilingi 150,000 kwa ajii ya kupimiwa viwanja vyetu lakini hadi sasa Agosti 2024 hakuna kilichofanyika.

Ipo hivi Halmashauri ya Kibaha kupitia Serikali za Mtaa ilisema tulipia kiwango hicho kupitia Namba za Malipo ambazo walitupatia (Control Number) kwa ajili ya kupimiwa Viwanja.

Tukafanya mchakato huo kwa kulipia, kish tukaenda Halmashauri wakatupa risiti, baada ya hapo Serikali za Mtaa zikatukabidhi ‘Bikoni’ ili zoezi likishafanyika la upimaji iz Bikoni ziwekwe.

Kuna idadi kubwa wa Watu ambao tulilipia lakini mpaka sasa kimya, hata tukiuliza hakuna majibu yanayoeleweka kutoka kwa Serikali za Mtaa na Halmashauri ya Kibaha ambayo ndio ilitoa Control Number na risiti pia.

Tunaomba suala hili lifike ngazi za juu, tunataka mchakato wa kutupimia ufanyike, hatupati majibu ya Wanaohusika.

Pia soma ~ Madai ya Halmashauri kuingia Mitini na 150,000 za Wananchi, Mwenyekiti wa Mtaa afafanua
 
Back
Top Bottom