Tunaomba radhi kwa kuchelewa kukujibu kutokana na changamoto ya muda kwenye akaunti yetu, ambayo kwa sasa imetatuliwa. Pole sana kwa usumbufu wa kukosa huduma ya umeme.
Tunapenda kukufahamisha kuwa endapo huduma itasitishwa kwa sababu yoyote ile, ikiwemo dharura, tunatoa taarifa kwa wateja wetu mapema iwezekanavyo, zikieleza sababu ya katizo, pamoja na makadirio ya muda wa kurejeshwa kwa huduma.
Tunatumiaga majukwaa yetu ya WhatsApp na SMS kutoa taarifa mapema na kwa haraka. Tunaomba kufahamu kama tayari umejiunga na huduma hizi ili tuweze kukufikia kwa urahisi zaidi? Kama bado, tafadhali tutumie namba yako ya WhatsApp katika inbox yetu tukuunge.