Mzee wa Code
Member
- Sep 23, 2024
- 61
- 91
Sisi Wakazi wa maeneo ya Viwege na Pugu Kinyamwezi, Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam tumekuwa na changamoto ya kuwa na barabara mbovu, ikinyesha mvua ndio kabisa hali inazidi kuwa mbaya kuliko maelezo.
Barabara za mitaani kwetu zimeharibika vibaya, hali inayotulazimu kulaza magari mbali na nyumbani maeneo ya barabarani na kulipia Tsh. 2,000 kwa siku.
Gharama hizo zimekuwa mzigo mkubwa kwetu kwa kuwa tunalipa hivyo kila siku, wakati wengine maeneo ya kuegema magari yapo kwenye makazi yetu lakini hatufiki kutokana na changamoto ya barabara.
Tunazitaka mamlaka husika ikiwemo TARURA kuingilia kati na kufanyia matengenezo barabara hiyo kwa haraka.
Hali hii imekuwa kero kwetu Wananchi na tunaiomba Serikali ichukue hatua haraka ili kurahisisha usafiri na kupunguza mzigo wa gharama.