KERO Wakazi wa Sokoine, Manispaa ya Songea tunateseka na shida ya maji, hutoka mara moja kwa wiki

KERO Wakazi wa Sokoine, Manispaa ya Songea tunateseka na shida ya maji, hutoka mara moja kwa wiki

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Habari,

Sisi ni wakazi wa Sokoine ndani ya Manispaa ya Songea, Mkoa wa Ruvuma. Tuna kero kubwa ya upatikanaji wa maji. Mara nyingi maji hupatikana mara moja kwa wiki, na kwa nadra sana hupatikana mara mbili kwa wiki, yaani kila baada ya siku 3 au 4.

Tatizo kubwa zaidi ni muda wa maji kutoka. Mara nyingi huanza kutoka usiku sana, wakati mwingine saa 6 usiku, na hukatwa saa 12 asubuhi. Hali hii imetulazimisha kuwa kama watumwa wa kuamka usiku kuchota maji na kujaza vyombo mbalimbali tulivyonavyo.

Tatizo hili limekuwepo kwa miaka mingi. Tunahitaji maji wakati wa mchana, lakini badala yake yanatoka nyakati za usiku wakati watu wanahitaji kupumzika baada ya shughuli za siku nzima.

Kinachotushangaza zaidi ni kwamba kuna mitaa mingine ambayo maji hutoka kila siku bila kuwa na mgao kama ilivyo Sokoine. Hatuipingi mgao wa maji ikiwa unazingatia usawa kulingana na rasilimali zilizopo, lakini tunaomba mamlaka ieleze kwa nini maji ya Sokoine yatoke usiku sana badala ya asubuhi au mchana, na kwa nini mgao huu unaonekana kuathiri zaidi mtaa wetu.

Soma Pia: Kero Ya Maji kwa Wakazi wa TABATA

Tunaomba mamlaka husika, hasa SUWASA, itoe ufafanuzi kuhusu chanzo cha tatizo hili na sababu za Sokoine kuwa na mgao wa namna hii wakati mitaa mingine inapata maji kwa wakati.

Tunaomba utusaidie kupaza sauti ili changamoto hii itatuliwe kwa haraka na wananchi wote wapate huduma ya maji kwa usawa.

Ahsante.
 
Back
Top Bottom