Wakazi wa Swaswa Dodoma na Mafuriko

Wakazi wa Swaswa Dodoma na Mafuriko

Yesu Anakuja

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2019
Posts
12,675
Reaction score
25,924
Wakazi wa Swaswa jijini Dodoma waanza kujiandaa na mafuriko, ni kitu kimenishangaza sana mara baada ya kuspend muda kwa wiki yote iliyopita katika jiji hili.

Kuna mwenyeji wangu amekuwa akinishauri nije kujenga Dom nikasema ngoja niende, zunguruka na madalali kutafuta viwanja ndio nikaonyeshwa Swaswa.

Bahati ikawa yangu, baada ya kuachana na dalali si nikarudi eneo lile, jirani akanitonya kuwa niwe makini kununua viwanja maeneo hayo kwasababu hata wao wameshaanza kujiandaa na mafuriko kwa mvua zitakazokuja kwani kila mwaka kuna mafuriko. nilishangaa sana katikati ya jiji miundombinu haidhibiti mafuriko kwenye maeneo yenye viwanja vizuri namna ile. Akaniambia pia Swaswa kuna migogoro ya viwanja balaa..

Kwakweli kiwanja ni kuzuri sana lakini sijajua kama kweli alichosema jirani ni sahihi au alikuwa anambania mshikaji asipate pesa, na hasa lile la migogoro. wenyeji wa Dodoma naomba mtutonye tafadhali anayeyajua mazingira hayo.
 
Ukitaka kununua kiwanja nenda kafanye hivyo wakati wa mvua
Ukitaka kujua kiwanja kina mgogoro au la chakua nakala za nyaraka za kiwanjahusika nenda jiji kafanye kitu kinaitwa search hapo utakua salama ikiwa utakuta kila kitu kiko sawa.
 
Dodoma kuna mvua za kuleta mafuriko?
zipo mzee, nasikia eneo la swaswa kuna mafuriko kila mwaka. hivi pale hawawezi kutengeneza miundombinu ya kumanage maji? kuna viwanja vizuri balaa utashangaa kwanini watu hawanunui. nimeuliza watu wengi naona kama kuna kaukweli fulani.
 
Nadhani huko ni kwa akina MC PiliPili
 
Dodoma kuna mvua za kuleta mafuriko?
Maeneo fulani fulani hua yanatuamisha maji kipindi cha mvua na kusababisha usumbufu sana
Hakuna mafuriko kivile na mvua ni za masiku tu,( November/December - April)zikisha hakuna mvua nyingine mpaka masika nyingine.
Karibu sana Makao Makuu ya Nchi.
 
specifically, Swaswa unapajua mzee, kuna mafuriko? ndio swali.
 
zipo mzee, nasikia eneo la swaswa kuna mafuriko kila mwaka. hivi pale hawawezi kutengeneza miundombinu ya kumanage maji? kuna viwanja vizuri balaa utashangaa kwanini watu hawanunui. nimeuliza watu wengi naona kama kuna kaukweli fulani.
Kwakua mji unazidi hiyo ni changamoto ya muda tu.
 
Kama Hujui Uliza Mkuu

Unapajua Nkuhungu Mpaka Kesho Kuna Nyumba Zaidi Ya 200 Zipo Kwenye Maji Na Mvua Zikirudi Aibu

Serikali inawasaidiaje wananchi wa eneo hilo sasa, nyumba 200? hawawezi kuchimba mifereji mikubwa kuokoa hilo? Nkuhungu ndio karibu na swaswa au mbali na swaswa?
 
Viwanja Tazama Mkalama, Kisasa Juu Kama Unakwenda NEC, Msalato, Nala Mkonze

Kwakua mji unazidi hiyo ni changamoto ya muda tu.
Makao Makuu ya nchi, kamji kenyewe kadogooo, wanashindwa nini kudhibiti mambo kama hayo sasahivi kabla mji haujakua? kwa jinsi watu wanavyohamia Dodoma baada ya Serikali kuhamia pale, wana mpango gani?
 
specifically, Swaswa unapajua mzee, kuna mafuriko? ndio swali.
Napajua ndiyo maana nasema si mafuriko kivile
Labda ntakua sijui maana ya mafuriko kwakua mm si mtaalamu wa mambo hayo japokua ikiwa maji kutuwama mahali kwa wingi mkubwa sana nayo inachukuliwa kua ni mafuriko, I stand to corrected.
 
Viwanja Tazama Mkalama, Kisasa Juu Kama Unakwenda NEC, Msalato, Nala Mkonze

Kisasa nimekimbia bei, watu wanaanzia 20m, Mkalama kama ndio hio njia ya Singida nimepata kimoja kwa 6m au sijui ndio Nala huko? Msalato nina mpango kununua viwanja hata 5 vya kuja kuuza baadaye kwasababu si ndio uwanja wa ndege unajengwa kule na magereza nafikiri wapo kule kama sikosei...wasipokuja kununua nitajenga hata loji miaka hiyo.
 
Napajua ndiyo maana nasema si mafuriko kivile
Labda ntakua sijui maana ya mafuriko kwakua mm si mtaalamu wa mambo hayo japokua ikiwa maji kutuwama mahali kwa wingi mkubwa sana nayo inachukuliwa kua ni mafuriko, I stand to corrected.
Noted ndugu. thanks.
 
Serikali inawasaidiaje wananchi wa eneo hilo sasa, nyumba 200? hawawezi kuchimba mifereji mikubwa kuokoa hilo? Nkuhungu ndio karibu na swaswa au mbali na swaswa?

Serikali Iliwapa Viwanja Vingine, Nkuhungu Ukifika Wajenzi Ni Uelekeo Wa Chang'ombe

Swaswa Huko Ukisikia Majaruba Ndiyo Hayo
Eneo La Kisasa Shell Kwa Mbele Tanroad Wamefumua Barabara Kuu Kuongeza Kipenyo Cha Daraja

Sababu SGR Tuta Lake Litakinga Maji Sasa Yatakapokuwa Mengi
Wananchi Watajuta
 
Makao Makuu ya nchi, kamji kenyewe kadogooo, wanashindwa nini kudhibiti mambo kama hayo sasahivi kabla mji haujakua? kwa jinsi watu wanavyohamia Dodoma baada ya Serikali kuhamia pale, wana mpango gani?
Dodoma imepangika vizuri sana kuliko miji yote hapa bongo, miundo mbinu ya kuthibiti mafuriko tangu miaka na mikaka ndiyo maana husiki mafuriko yapo
Hata hivyo maboresho yanaendelea.
 
Serikali Iliwapa Viwanja Vingine, Nkuhungu Ukifika Wajenzi Ni Uelekeo Wa Chang'ombe

Swaswa Huko Ukisikia Majaruba Ndiyo Hayo
Eneo La Kisasa Shell Kwa Mbele Tanroad Wanefumua Barabara Kuu Kuongeza Kipenyo Cha Daraja

Sababu SGR Tuta Lake Litakinga Maji Sasa Yatakapokuwa Mengi
Wananchi Watajuta
hapo wajenzi ndio maeneo yale ya Martin Luther? au unapita
 
Dodoma imepangika vizuri sana kuliko miji yote hapa bongo, miundo mbinu ya kuthibiti mafuriko tangu miaka na mikaka ndiyo maana husiki mafuriko yapo
Hata hivyo maboresho yanaendelea.
mwaka juzi niliona kwenye taarifa ya habari mafuriko. usitupige porojo hapa.
 
Kisasa nimekimbia bei, watu wanaanzia 20m, Mkalama kama ndio hio njia ya Singida nimepata kimoja kwa 6m au sijui ndio Nala huko? Msalato nina mpango kununua viwanja hata 5 vya kuja kuuza baadaye kwasababu si ndio uwanja wa ndege unajengwa kule na magereza nafikiri wapo kule kama sikosei...wasipokuja kununua nitajenga hata loji miaka hiyo.
Airport Inajengwa Maeneo Ya Mipango Unaingia Kulia Ukitoka Mjini, Mkalama Ukitoka JK CONVENTION CENTRE
Ukianza Kupanda UDOM Kulia
 
Back
Top Bottom