Wakazi wa Swaswa Dodoma na Mafuriko

Wakazi wa Swaswa Dodoma na Mafuriko

Wakazi wa Swaswa jijini Dodoma waanza kujiandaa na mafuriko, ni kitu kimenishangaza sana mara baada ya kuspend muda kwa wiki yote iliyopita katika jiji hili. kuna mwenyeji wangu amekuwa akinishauri nije kujenga Dom nikasema ngoja niende, zunguruka na madalali kutafuta viwanja ndio nikaonyeshwa Swaswa. Bahati ikawa yangu, baada ya kuachana na dalali si nikarudi eneo lile, jirani akanitonya kuwa niwe makini kununua viwanja maeneo hayo kwasababu hata wao wameshaanza kujiandaa na mafuriko kwa mvua zitakazokuja kwani kila mwaka kuna mafuriko. nilishangaa sana katikati ya jiji miundombinu haidhibiti mafuriko kwenye maeneo yenye viwanja vizuri namna ile. akaniambia pia Swaswa kuna migogoro ya viwanja balaa....kwakweli kiwanja ni kuzuri sana lakini sijajua kama kweli alichosema jirani ni sahihi au alikuwa anambania mshikaji asipate pesa, na hasa lile la migogoro. wenyeji wa Dodoma naomba mtutonye tafadhali anayeyajua mazingira hayo.
Nimeku inbox Nina kiwanja nauza Dodoma.
 
Dah mzee nikajenge maeneo ya mirembe siku vichaa wakitoroka mtaani patakuwaje
Kama bado upo dodoma na hujanunua kiwanja njoo upewe kiwanja 65 kwa 67 barabarani kwa 5.5Mill utakuja kunishukuru.. Nala Ya Kwanza na unanunua kwa wenyeji hata ukitaka heka tatu nne zipo Njia ya kuelekea Chuo Cha DECCa achana na mkalama Wala mtumba Wala kisasa
 
Kwa nini uwekeze Dodoma?

Jiji la Dodoma tayari limeandaa maeneo kadhaa ya uwekezaji na kuweka mazingira wezeshi ili kuwapatia waendelezaji.

Eneo la Uwekezaji Njedengwa:
ambalo lina Hekta 580 na jumla viwanja 141 vya uwekezaji vyenye ukubwa wa kati ya ekari 2 hadi 26 kwa kiwanja kimoja kutegemeana na uhitaji wa mwekezaji.

Majengo yanayo paswa kujengwa ni maghorofa ya makazi,majengo ya biashara na huduma za jamii. Kati ya viwanja hivyo, viwanaja vya Taasisi ni 46, vya kibiashara 20 na makazi maalumu 75. Eneo hili tayari lina miundo mbinu ya barabara za lami, maji na umeme na yote inatumika.

Mji Mpya wa Iyumbu: Una ukumbwa wa hekta 252 na kuna viwanja 242, kati ya hivyo vya biashara ni 10, Viwanda vidogo 2, biashara na makazi 173 na makazi maalum 57 na kuna uwanja wa michezo "Iyumbu Town Center".

Kwa ujumla Jiji la Dodoma
  • Maeneo yaliyopangwa na miundombinu iliyosanifiwa vizuri.
  • Hakuna msongamano wa magari kutokana na kuwepo kwa mpangilio mzuri wa mfumo wa barabara. (barabara za lami za ndani zinaendelea kujengwa. Mf barabara za Martin Luther – Swaswa, Wajenzi – Chang’ombe, Meriwa – Swaswa, Emaus – African dream, Ipagala –Ilazo, Kisasa - Njedengwa).
  • Kuna maeneo ya kupumzikia kama vile Nyerere Square, Bustani ya Chinangali Park, nk.
  • Gharama za kutwaa ardhi ni nafuu na ni vyepesi kupata hati milki za ardhi kutoka Manispaa
  • Kuna wepesi katika kuidhinishiwa ramani za ujenzi na
  • Manispaa inajali na kuzingatia mahitaji binafsi ya waendelezaji.
 
Kama bado upo dodoma na hujanunua kiwanja njoo upewe kiwanja 65 kwa 67 barabarani kwa 5.5Mill utakuja kunishukuru.. Nala Ya Kwanza na unanunua kwa wenyeji hata ukitaka heka tatu nne zipo Njia ya kuelekea Chuo Cha DECCa achana na mkalama Wala mtumba Wala kisasa
chuo cha decca ndio chuo gani?
 
Wakazi wa Swaswa jijini Dodoma waanza kujiandaa na mafuriko, ni kitu kimenishangaza sana mara baada ya kuspend muda kwa wiki yote iliyopita katika jiji hili. kuna mwenyeji wangu amekuwa akinishauri nije kujenga Dom nikasema ngoja niende, zunguruka na madalali kutafuta viwanja ndio nikaonyeshwa Swaswa. Bahati ikawa yangu, baada ya kuachana na dalali si nikarudi eneo lile, jirani akanitonya kuwa niwe makini kununua viwanja maeneo hayo kwasababu hata wao wameshaanza kujiandaa na mafuriko kwa mvua zitakazokuja kwani kila mwaka kuna mafuriko. nilishangaa sana katikati ya jiji miundombinu haidhibiti mafuriko kwenye maeneo yenye viwanja vizuri namna ile. akaniambia pia Swaswa kuna migogoro ya viwanja balaa....kwakweli kiwanja ni kuzuri sana lakini sijajua kama kweli alichosema jirani ni sahihi au alikuwa anambania mshikaji asipate pesa, na hasa lile la migogoro. wenyeji wa Dodoma naomba mtutonye tafadhali anayeyajua mazingira hayo.
Sijui,ngoja nikutafutie Mimi sio dalali you meet the real owner,0716884436.
 
Kisasa nimekimbia bei, watu wanaanzia 20m, Mkalama kama ndio hio njia ya Singida nimepata kimoja kwa 6m au sijui ndio Nala huko? Msalato nina mpango kununua viwanja hata 5 vya kuja kuuza baadaye kwasababu si ndio uwanja wa ndege unajengwa kule na magereza nafikiri wapo kule kama sikosei...wasipokuja kununua nitajenga hata loji miaka hiyo.
Nala mil.6?

Achana na madalali nenda direct kwa wenye mali
 
Wakazi wa Swaswa jijini Dodoma waanza kujiandaa na mafuriko, ni kitu kimenishangaza sana mara baada ya kuspend muda kwa wiki yote iliyopita katika jiji hili. kuna mwenyeji wangu amekuwa akinishauri nije kujenga Dom nikasema ngoja niende, zunguruka na madalali kutafuta viwanja ndio nikaonyeshwa Swaswa. Bahati ikawa yangu, baada ya kuachana na dalali si nikarudi eneo lile, jirani akanitonya kuwa niwe makini kununua viwanja maeneo hayo kwasababu hata wao wameshaanza kujiandaa na mafuriko kwa mvua zitakazokuja kwani kila mwaka kuna mafuriko. nilishangaa sana katikati ya jiji miundombinu haidhibiti mafuriko kwenye maeneo yenye viwanja vizuri namna ile. akaniambia pia Swaswa kuna migogoro ya viwanja balaa....kwakweli kiwanja ni kuzuri sana lakini sijajua kama kweli alichosema jirani ni sahihi au alikuwa anambania mshikaji asipate pesa, na hasa lile la migogoro. wenyeji wa Dodoma naomba mtutonye tafadhali anayeyajua mazingira hayo.
Aaaah acha uswahili kama masaki,msasani katikati ya Dar mafuriko yanatokea,wewe unashangaa mafuriko Dodoma?
 
IMG-20200116-WA0058.jpg

picha zote ni mafuriko eneo la Msasani jiji la Dar

IMG-20200116-WA0048.jpg

Kama bado upo dodoma na hujanunua kiwanja njoo upewe kiwanja 65 kwa 67 barabarani kwa 5.5Mill utakuja kunishukuru.. Nala Ya Kwanza na unanunua kwa wenyeji hata ukitaka heka tatu nne zipo Njia ya kuelekea Chuo Cha DECCa achana na mkalama Wala mtumba Wala kisasa
Kimepimwa?
 
Back
Top Bottom