A
Anonymous
Guest
Mimi ni Kijana wa Jamii ya Kimasai kutoka Longido, Kata ya Tinga Tinga, naomba malalamiko haya wa Wananchi yamfikie Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda.
Kata yetu inashida ya maji tangu enzi na enzi japo tuko karibu sana na vyanzo vingi vya maji, pia Serikali imekuwa ikileta miradi mbalimbali ya maji katika kata yetu lakini maji bado ni shida.
Kuna mradi wa Ukolo ambao upo takriban Miaka 12 sasa na bado haujakamilika, cha kushangaza Mwaka 2023 Serikali ilileta Mradi mwingine wa Takriban Shilingi Bilioni 1.7 kwa ajili ya maji kwenye kata yetu.
Kinachoiangusha miradi hiyo ni Wakandarasi na baadhi ya viongozi wetu ndani ya kata akiwepo Diwani wetu, Peter Lekaneth kutowajibika inavyotakiwa.
Naomba TAKUKURU Mkoa wa Arusha mfuatilie miradi hii ambayo ni mikubwa lakini Wananchi hatufaidiki kwa chochote.