A
Anonymous
Guest
Mimi ni mkazi wa Ubungo Riverside, eneo maarufu kama Kwa Novo. Kwa takribani miezi saba sasa, maji ya DAWASA hayatoki kabisa, jambo ambalo limeleta adha kubwa kwa wakazi wa eneo hili. Kwa sasa tunalazimika kununua dumu moja la maji kwa shilingi 1,000, hali inayoongeza gharama kubwa ya maisha kwa wananchi wa kawaida.
Mbali na gharama hizo, tatizo hili pia linasababisha upotevu mkubwa wa muda, kwani kila siku tunalazimika kusubiri kwa masaa mengi kutafuta maji kwa matumizi ya nyumbani. Uongozi wa eneo unaendelea kutuambia tuvumilie hadi mradi wa kufungwa kwa pampu mpya ukamilike, lakini hadi sasa hakuna mabadiliko yoyote yanayoonekana zaidi ya wananchi kuendelea kupata mateso.
Tunaomba mamlaka husika, hususan DAWASA na viongozi wa eneo, kuchukua hatua za haraka kutatua changamoto hii ili wananchi waweze kupata huduma ya maji safi na salama kama ilivyo haki yao ya msingi.
Pia soma ~ DAWASA: Pampu 8 zenye uwezo wa kuzalisha Lita 1,500 kila moja kwa siku zimenunuliwa kutatua changamoto ya maji Ubungo DC