Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
ampeni za Uchaguzi Mkuu zimeendelea katika Jimbo la Mbarali, mkoani Mbeya, ambapo baadhi ya wakazi wametoa ombi kwa mgombea ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bahati Ndingo, kusimamia agenda ya upatikanaji wa ardhi ya kutosha kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji.
Ombi hilo limeibuliwa baada ya uzinduzi wa kampeni uliofanywa na Katibu Mstaafu wa CCM, Daniel Chongolo, katika Kijiji cha Kongolo Mswiswi, wilayani Mbarali.