Wakazi wanne wa Wilaya ya Same wamefikishwa Mahakamani wakidaiwa kusafirisha dawa za kulevya aina ya mirungi

Wakazi wanne wa Wilaya ya Same wamefikishwa Mahakamani wakidaiwa kusafirisha dawa za kulevya aina ya mirungi

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
819
Reaction score
1,093
Wakazi wanne wa Wilaya ya Same wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi jana tarehe 28 Machi 2025, wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi, wakidaiwa kusafirisha dawa za kulevya aina ya mirungi zenye uzito wa jumla ya kilogramu 518.57.

Watuhumiwa hao, Nimkaza Mbwambo, Prosper Lema, Nterindwa Mgalle, na Stephanie Mrutu, walisomewa mashitaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Ally Mkama.

Wakili wa Serikali, Julieth Komba, aliwasomea mashitaka kwa nyakati tofauti ambapo alidai kuwa, Machi 21, 2025, watuhumiwa hao walitenda makosa hayo katika kijiji cha Rikweni, Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro.

Soma Pia: DCEA yamnasa Kinara wa Mirungi, yateketeza Ekari 285.5 Same

Katika mashitaka, ilidaiwa kuwa mshitakiwa Nimkaza Mbwambo alikamatwa akisafirisha kilogramu 138.58 za dawa za kulevya aina ya mirungi, huku Prosper Lema naye akikamatwa akiwa na kilogramu 113.29. Pia, Nterindwa Mgalle alikamatwa akiwa na kilogramu 160.25 za mirungi, wakati Stephanie Mrutu alikutwa akisafirisha kilogramu 106.45 za mirungi.

Kwa mujibu wa wakili wa serikali, upelelezi wa kesi hizo bado haujakamilika. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 11, 2025 kwa kutajwa, na watuhumiwa wote wamepelekwa mahabusu.

Wakati huo huo, wakazi wawili wa Wilaya ya Same, Dorisiana Mchome na Aisha Mbaga, wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Same wakikabiliwa na shtaka la kusafirisha kilogramu 54.15 za dawa za kulevya aina ya mirungi.

Watuhumiwa hao walisomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Hellen Hozza. Inadaiwa kuwa, Machi 21, 2025, katika kijiji cha Rikweni, Dorisiana alikamatwa akiwa na kilogramu 17 za mirungi, wakati Aisha alikamatwa akiwa na kilogramu 37.15.

Wakili wa serikali, Michael Matowo, aliieleza mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na Kesi imeahirishwa hadi Aprili 10,
2025 kwa kutajwa, na watuhumiwa wote wamerudishwa mahabusu. Hata hivyo, mtuhumiwa Dorissian Mchome kosa lake linadhaminika isipokuwa wadhamini wake wameshindwa kutoa taarifa sahihi mahakamani ila dhamana bado ipo wazi.

Kuanzia Machi 19 hadi 25, 2025, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) ilifanya operesheni maalum wilayani Same, mkoani Kilimanjaro, ambapo Interindwa Kirumbi, maarufu kama "Mama Dangote", ambaye anadaiwa kuwa kinara wa biashara ya mirungi, alikamatwa pamoja na wenzake. Aidha, jumla ya ekari 285.5 za mashamba ya mirungi zilibainika na kuteketezwa, hatua inayodhihirisha jitihada za serikali katika kupambana na biashara haramu ya dawa za kulevya nchini.
IMG-20250329-WA0014.jpg
IMG-20250329-WA0019.jpg
IMG-20250329-WA0013.jpg
IMG-20250329-WA0017.jpg
IMG-20250329-WA0016.jpg
IMG-20250329-WA0018.jpg
IMG-20250329-WA0015.jpg
 
Vita dhidi ya dawa za kulevya ni ngumu kuitokomeza, bila ya msaada toka kwa wananchi ambao tunaishi nao hao wasambazaji kuweza kuwatolea taarifa kwenye vyombo husika ili kuweza kuikomesha hiyo biashra haramu.

Sisi raia wema tunatakiwa kuonyesha uzalendo kwanza kwa nchi yetu na kuisaidia taasisi inayopambana na dawa za kulevya. Haiwezekani mtu analima hekari kadhaa za dawa za kulevya Hadi anavuna na kupeleka sokoni, halafu eti wananchi ambao wako naye karibu mtaani, wanashindwa kutolea taarifa kwenye vyombo/mamlaka husika.

Wananchi tuwe wazalendo haswa. La sivyo ukifumbia Macho, utajakuta siku moja mwanao ndio mteja wao. Hapo sijui utamlaumu nani.
 
Vita dhidi ya dawa za kulevya no ngumu kutokomea, bila ya msaada toka kwa wananchi ambao tunaishi nao hao wasambazaji kuweza kuwatolea taarifa kwenye vyombo husika ili kuweza kuikomesha.

Sisi raia wema tunatakiwa kuonyesha uzalendo. Haiwezekani mtu analima hekari kadhaa za dawa za kulevya Hdi anavuna na kupeleka sokoni, halafu eti wananchi ambao wako naye karibi wanashindwa kutolea taarifa kwenye vyombo husika

Wananchi tuwe wazalendo haswa. La sivyo ukifumbia Macho, utajakutq siku mwanao ndio mteja wao. Hapo sijui utamlaumu nani.
Sasa mirungi ni madawa ya kulevya kweli?
 
Uzalendo maana yake nini? Walio katika nafasi n ngazi mbalimbali wote ni wazalendo? Asiyetaka hela au anayefanya kazi ya kujitolea na kuamuliwa malipo huyo ndo mzalendo? Anayenyimwa haki na akanyamaza huyo ndie mzalendo?
 
Wale mapacha wa TA walikuwa wanatafuna hilo gomba Ijumaa mpk jumapili hatari. BIG G na pepsi bonge nikiona wana pepsi najua w-end imeanza sasa.
 
Back
Top Bottom