Kibunango,
Hao Daily Mail ni anti-migrants miaka na miaka. Huko nyuma articles zao zote zilikuwa kwa sehemu kubwa refugees na watu kama sisi ambao tulikuwa kwenye work permit.
Baadaye wakaandama Wanafunzi, serikali ikawaambia wakizuia wanafunzi wa nje, itabidi taxes zipande maana hao ndio wanasaidia vyuo kujiendesha kwa
fees zao ambazo nyingi ni kuanzia pounds 8000.
MIaka ya 90 wakati wanatutaka walikuwa wanatumia kila njia tuje, walihitaji Engineers, nurses, doctors, sasa wanashangaa kuona idadi ya watoto waliozaliwa na mama kutoka nje ni moja ya tano? Wao wamejazana USA, tena wanaishi illegally, wamejazana Australia, Afrika na kwingineko.
Daily mail sasa wamehamia kwa watu wa Eastern Europe, ni ubaguzi huo huo. Wamekuja kwasababu wamewaruhusu kuja, kama hawawataki si wangesubiri mpaka hiyo miaka saba?
Kwa taarifa tu business za Waingereza kwenye hizo nchi za Eastern Europe ni kubwa zaidi ya interests za watu wa Eastern Europe hapa UK.
Ubaguzi ni ule ule whether umeelekezwa kwa mzungu au mweusi.