Mwafrika wa Kike
JF-Expert Member
- Jul 5, 2007
- 5,185
- 60
Now I have another reason to move my base to somewhere near Leincester...
Mwafrika wa Kike,
Dada yangu gari kinaweza chukua abiria wanne lakini abiria wanne hawawezi beba gari moja, safarihaitakuwepo!.... Haa haaa haaa!
Admin,
Please unaweza kuihaisha mada hii kule kwenye dini maanake sielewi kabisa inachoendelea hapa. Kuruhusiwa kwa waisklaam kuwa na wake wanne na hayo ya Eastern Europe?... Navyojua mimi ni Turkey na Bosnia tu zenye waislaam lakini zilizobaki zote ni nchi zenye kikristu na pengine hakuna kabisa Muislaam isipokuwa mhamiaji.
Kuwa na wake wanne haikuanza jana toka Ibrahim, church zaKatoliki ndio waliobadilisha as a fact ukitazama mti wa kizazi cha Ibrahim utakuta karibu mitume wote walikuwa na wake zaidi a mmoja..
Tatizo kubwa la Uislaam ni kuendeleza yale yaliyokubaliwa na mwenyezi Mungu toka zamani hali dini nyingine zinatupa mabadiliko yaani changes kiasi kwamba najiuliza kumbe Mungu naye alikuwa akifanya makosa kiasi kwama binadamu wamepewa nafasi ya kurekebisha kipi halilli na kipi haramu..
talia sana jamaa zangu mbona mwala nguruwe na halali yenu nasi hatupigi kelele...
Idimi,
Mimi niko UK na nina taarifa za kutosha kuhusu watu wa Eastern Europe. Lakini nilichoandika ni je kuja kwao kuna uhusiano gani na hili la kuoa wanawake wengi pamoja na benefits?
Pia kusema wenyeji wanalalamika, inategemea ni wenyeji gani, kama ni mwajiri hasa wa viwanda vidogo vidogo kuja kwa watu wa Eastern Europe ni baraka kubwa. Wengi wa wanaolalamika ni wenyeji ambao hawafanyakazi na pia wenyeji waliokuwa wanafanya manual jobs ambao walikuwa wanacharge ile mbaya kwa kazi zao kwa mfano plumbers. Wao Waingereza wamejazana kila sehemu, kwanini walalamike wenzao wakija kwao?
Kuhusu kuzaa watu wanaosemwa ni pamoja na sisi weusi. Je wao huko waliko hamia mbona hawasemwi? Katika hao wanaosema moja ya tano wamezaliwa na mama ambao hawakuzaliwa hapa ni pamoja na watoto wangu ambao baba yao na mama yao tumelipa tax muda wote na hatujawahi kupata social benefits.
Pia kwa taarifa yako watu wa Eastern Europe hawazai watoto wengi. Wanazaa watoto wachache kuliko Waingereza. Wanaozaa watoto wengi ni watu wa middle East, Asia na Afrika.
Wakati mwingine stereotype bila kuwa na data za uhakika ndio mwanzo wa ubaguzi.
Kibunango,
Hao Daily Mail ni anti-migrants miaka na miaka. Huko nyuma articles zao zote zilikuwa kwa sehemu kubwa refugees na watu kama sisi ambao tulikuwa kwenye work permit.
Baadaye wakaandama Wanafunzi, serikali ikawaambia wakizuia wanafunzi wa nje, itabidi taxes zipande maana hao ndio wanasaidia vyuo kujiendesha kwa
fees zao ambazo nyingi ni kuanzia pounds 8000.
MIaka ya 90 wakati wanatutaka walikuwa wanatumia kila njia tuje, walihitaji Engineers, nurses, doctors, sasa wanashangaa kuona idadi ya watoto waliozaliwa na mama kutoka nje ni moja ya tano? Wao wamejazana USA, tena wanaishi illegally, wamejazana Australia, Afrika na kwingineko.
Daily mail sasa wamehamia kwa watu wa Eastern Europe, ni ubaguzi huo huo. Wamekuja kwasababu wamewaruhusu kuja, kama hawawataki si wangesubiri mpaka hiyo miaka saba?
Kwa taarifa tu business za Waingereza kwenye hizo nchi za Eastern Europe ni kubwa zaidi ya interests za watu wa Eastern Europe hapa UK.
Ubaguzi ni ule ule whether umeelekezwa kwa mzungu au mweusi.
Si Uingereza pekee yenye interest za kibiashara katika nchi hizo, kwa mfano hivi karibuni Nokia walipoamua kufunga kiwanda chao chta ujerumani, wafanyakazi waliandamana na zaidi chancellor wao alikuja juu. Lakini haikusaidia kitu.
Kuhusu hizo benefits kwa wakaazi, sina ufahamu mkubwa nazo, ila kwa macho na masikio yangu nimeona jinsi baadhi ya watanzania hapo UK wakizitegemea katika maisha yao ya kila siku. Hali hii imewafanya kuwa na familia kubwa ili kuweza kupata benefit nyingi zaidi.
Haya Mkuu nimekuelewa katika hili! hasa mfano wa gari ambao sasa unadhihirisha kabisa kuwa hii mada inabidi iende kule kwenye dini au somewhere!
Sasa hii issue ni kwa mwanaume ambaye atakuwa na wake wanne. Itakuwaje kwa mwanamke mwenye waume wanne?
Kaazi kweli kweli. Yaani nyie kazi zenu kuutukana tu Uislam. Mbona kuna Wakristo wengi tu wanazaa hovyo na vimada. Na cha ajabu siku hizi kanisa linahalalisha watoto wa nje ya ndoa.
Kama hujui kitu ni bora ukauliza ueleweshwe.
Kabla ya Uislam watu matajiri Middle East na duniani kote walikuwa wanaoa wake wasio na idadi kulingana na mfuko wa mtu 10, 20, 30, 100, nk. Wengine walikuwa wakichukuwa mabint na kuwabikiri basi hawawarudii tena. Lakini anaitwa mke wa fulani. Haki yake ya unyumba hapewi na anatakiwa kukaa hivyo hadi umauti umkute.
Uislam uliondoa tabia hii na ikaweka kiwango cha mwisho wake wanne kwa mwenye uwezo economically, physically.
Haitoshi kuoa mke halafu huduma muhimu pamoja na tendo la ndoa humtimizii. Utakuwa umekiuka maadili ya ndoa.
Sheria ya mke mmoja imeshindwa kuondoa uzinzi. KWa mfano mtoto wa Malkia wa Uingereza Prince nani sijui, angeruhusiwa kuoa mke zaidi ya mmoja, asingemtaliki Diana. Angeweza kuwa nao wote Diana na Camila.
Ruhusa ya kuoa zaidi ya mmoja ina faida zake
1. Wake wote wanakuwa na haki sawa ukiondoa kuheshimiana kati ya aliyetangulia kuolewa na wake wanaofuta. Mume anatakiwa kutoa haki sawa kuanzia matunzo na hata unyumba. Ndiyo maana anatakiwa kila nyumba akae kwa siku sawa na nyingine. Sio leo kwa Bi Fatuma siku nne, kwa Wadiri saa moja, kwa Kidawa siku mbili.
2. Watoto wote wanaozaliwa wana haki sawa kwa baba yao. Hakuna cha mtoto wa nyumba kubwa wala nyumba ndogo
3. Uwajibikaji. Kuna tabia ya wanaume wakristo wanajidai wana ndoa ya mke mmoja, huku mitaani wana watoto kibao ambao wanawatelekeza. Mama anaogopa kwenda kudai haki ya matunzo ya mtoto kwa sababu ati ni mume wa mtu.
4. Imethibitika kuwa katika ndoa za mitala maradhi ya zinaa ni kidogo sana. kwa anayebisha atazame data za ukimwi duniani. Hata hapa Bongo kuna utafiti ulifanywa kwa waathoirika wa Ukimwi na ilionekana kuwa wengi wao wana ndoa za mke mmoja.
Najua kuna watakaobisha. Endeleeni tu kubisha
Hivi ni taratibu zipi mtu anatakiwa kuzifuata ili awe muislam...