Gavana ni yule ambaye ana kitambi kikubwaa, alafu ana kiburi kupindukia. 😄 Kisa eti anaitwa his excellency, mke wake first lady na yeye ni rais wa 1/47 ya taifa la Kenya. Ana mawaziri ambao anawateua kusimamia sekta tofauti kwenye gatuzi lake. Ana hela za bajeti ambazo anapokea kutoka kwa serikali kuu, 35% ya hela zote ambazo zinakusanywa nchini.
Yeye kupitia wawakilishi kwenye bunge la gatuzi lake, almaarufu MCA(madiwani), ndiye anayeamua masuala yote yanayohusiana na maendeleo kwenye gatuzi lake. Seneta naye ni mwakilishi wa gatuzi lake kwenye bunge la kitaifa, seneti(upper house).
Alafu hayo yote yanajirudia kwenye level ya kitaifa. Wabunge wakiwa kwenye ngazi ya chini, pamoja na wawakilishi wa kina mama, Women Rep. Wakiwakilisha maeneo bunge yao kwenye bunge la kitaifa, Lower House. Wakisimamia maendeleo, sheria, miradi ya serikali kuu chini ya rais, wizara tofauti na mihimili mingine ya serikali. Wote hao wanachaguliwa moja kwa moja na wananchi kwenye uchaguzi mkuu, kila baada ya miaka mitano.