eliakeem
JF-Expert Member
- May 29, 2009
- 17,214
- 15,853
Huu mpango wa kutaka kumuua Ruto, ni nani anayewapa ujasiri mawaziri hao kutaka kumuua Ruto ambaye kwa kipindi chote amekuwa muaminifu kwa mtukufu rais baba.
Mbona mambo yamegeuka? Mtu aliyefanikisha malengo ya JUBILEE, lakini sasa anaoneka hafai.
Uhuru ameahidi kuleta kuleta umoja wa wa Kenya. Hilo ni jambo jema. Pia ni moyo mzuri. Ila kabla ya kuanza na Kenya, aanze na kujenga umoja ndani ya JUBILEE ndiyo aendelee kuhubiri umoja wa kitaifa. Hili la mgawanyiko ndani ya chama mpaka kufikia hatua ya kupanga mauaji si jambo la kuliangalia tu. Mwenyekiti wa chama anapaswa kufanya jambo ili kutuliza na kudhibiti hali.