Hehehe! Huwa mna nongwa sana nyie, hamkawii kuibuka na hizi mada za kupimana urefu wa dushe. Nimewaambia mara si haba kwamba Wakenya hatuwezi fugwa kwenye zizi la lugha moja kama mazombi, sisi ni wajanja wa lugha, tunaongea nyingi.
Tunapenda zetu za asili, na tunaongea pia za kigeni. Hii ndio sababu moja ambayo imetufanya kuwa wajanja zaidi ya raia wa nchi zote ukanda huu wote wa Afrika Mashariki na Kati. Wanasayansi walifanya utafiti uliodhihirisha kwamba mtu mwenye kuongea lugha kadhaa ana uawezo mkubwa kiakili na kimawazo.
Sasa nyie Wabongo mumefungiwa kwenye lugha moja, na hata hicho Kiswahili wengi hamkijui vizuri kwa ufasaha. Nikiangalia alivyoandika mleta mada, humo kuna makosa mengi ya kiufasaha halafu anajinadi kwamba yeye mtaalam wa Kiswahili. Vijana wa mjini kazi kuvaa milegezo na kuimba Bongo flava na kuomba omba buku jero mjini.