Mfahamu Isaya Yunge, kijana wa Kisukuma aliyemposa binti wa Rais Ruto wa Kenya

Mfahamu Isaya Yunge, kijana wa Kisukuma aliyemposa binti wa Rais Ruto wa Kenya

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
78,914
Reaction score
168,320
1000032183.jpg

ISAYA Yunge, kijana Mtanzania mwenye asili ya jamii ya Wasukuma, ameingia katika hatua mpya ya maisha baada ya kutambulishwa kama mchumba wa Charlene Ruto, binti wa Rais wa Kenya, William Ruto.

Uhusiano huo umefahamika zaidi baada ya hafla ya uchumba iliyofanyika nchini Kenya Agosti 8, ambapo Charlene alimtambulisha Isaya kama mwanaume anayetarajia kufunga naye ndoa.

1000032182.png
Hata hivyo, jina la Isaya si geni katika maeneo ya uongozi wa vijana, teknolojia na ubunifu barani Afrika. Safari yake ilianza mapema, huku akiwa miongoni mwa vijana waliopewa nafasi ya kushiriki katika shughuli za kitaifa na kimataifa kabla hata hajafikisha miaka 20.

Katika elimu, Isaya alisomea Bachelor of Science in Insurance and Risk Management katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Tanzania.

1000032181.png
Uongozi wake wa vijana ulianza kuonekana akiwa bado katika umri mdogo. Kati ya mwaka 2006 na 2007, aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Tanzania Junior Council, nafasi iliyompa fursa ya kuiwakilisha sauti ya watoto katika majukwaa mbalimbali.

1000032180.png
Mwaka uliofuata, akiwa na miaka 17, alichaguliwa kuwa Balozi wa Vijana wa UNICEF Afrika kwa kipindi cha 2007–2008. Kupitia nafasi hiyo, alishiriki katika mijadala na majukwaa ya kimataifa yaliyolenga kutetea haki na ustawi wa watoto, ikiwemo Mkutano wa G8.

Miaka iliyofuata ilimfungulia milango zaidi katika matumizi ya teknolojia kama nyenzo ya kuleta mabadiliko katika jamii. Mwaka 2018, juhudi hizo zilitambuliwa kimataifa baada ya Isaya kutunukiwa The Queen’s Young Leaders Award na aliyekuwa Malkia wa Uingereza, Elizabeth II.

1000032179.png
Tuzo hiyo ilitolewa kwa kutambua mchango wake katika kutumia teknolojia na ubunifu kutengeneza suluhisho zenye manufaa kwa jamii.

Mbali na tuzo hiyo, Isaya pia aliwahi kutajwa katika orodha ya Forbes Africa 30 Under 30, inayowatambua vijana wenye mafanikio na ushawishi katika sekta mbalimbali barani Afrika.

1000032178.png
Katika ulimwengu wa teknolojia na biashara, Isaya ni mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Goodsam Technologies. Pia amehusika na Smart Kaya, inayolenga kutumia teknolojia katika kuendeleza dhana ya nyumba janja barani Afrika.

Jina lake pia linahusishwa na SomaApp, jukwaa la kidijitali linalolenga kurahisisha upatikanaji wa vitabu na maudhui ya kusoma kupitia mtandao.

Falsafa yake kuhusu maisha na kazi inaonekana pia kupitia utambulisho wake wa “The Unshakable Optimist”, huku kauli yake ya kazi ikiwa “Building the Gateway to Africa’s Digital Economy.”

Kwa hiyo, zaidi ya kuwa jina lililovuma baada ya kuhusishwa na familia ya Rais wa Kenya, Isaya Yunge ana historia ya safari ya uongozi wa vijana, utetezi wa haki za watoto, teknolojia na ujasiriamali.

Kutoka Tanzania na katika familia yenye asili ya Wasukuma, safari hiyo sasa imemfikisha katika hatua nyingine muhimu ya maisha yake—kuwa mume mtarajiwa wa Charlene Ruto, na hivyo kuunganisha simulizi yake binafsi na familia ya kwanza ya Kenya.
 
Binti wa kwanza June Ruto ni mke wa Dr. Alexander Ezenagu Minigeria.
Charlene binti yake mwingine anaeolewa na Isaya Yumbe Mtanzania
Pamoja na kutudharau Watanzania wakajifanya mashapu, inakuwaje mabinti wa rais wanaolewa nje?
Vijana wa kiume wa Kenya mnashindwa wapi au ni kwa sababu ya one term?
Angalia Wakenya walivyopigika na kulia BONYEZA HAPA
 
Mashemeji hawaamini kilichotekea. Kila la kheri kwa dogo katika kuimarisha Jumuiya.
 
Pesa katolea wapi? Kwnye hizo apps na kujulikana unicef na kwa malkia? Money laundering? Project ya ruto? Hebu watueleze isijekua ruto analeta za sisiemu sasa kudistruct wakenya Kama tunavyoimbishwa hapa kila wakati na stori za kina zuchu na diamond wkt tunaibiwa kila pembe ya inchi
 
Haha nilikuwa naisubiri hii comment kwa hamu sana,
Huyu bwana mdogo ni "mjanja mjanja" mno alichowafanyia wazungu miaka ya nyuma walijuta kumuamini akakimbia na nchi kwenda kuishi barani Asia.😂😂.

Mwisho kabisa he's so damn smart upstairs na kila move anayofanya kwenye maisha yake huwa well calculated, hata hapo kwa ruto tujipe muda tu.
 
Mkuu jazia nyama kidogo

Hapo inaingia kichwani kwani huyo bibi harusi ni nung'aembe ila anaungwa na kuwa mtoto wa Rais tu. Eti Lamomy si ni sawa wajameni (Kenyatta)
 
Vile vijana wenyewe wamependanga, basi mimi nawapea baraka zangu.
 
Africa bwana.

Unaweza ukawa tech enterpreneur usijulikane, lakini siku ukioa mtoto wa rais tu, kila mtu atakujua na kukufuatilia.

What we reward with our attention explains our poverty.
 
Haha nilikuwa naisubiri hii comment kwa hamu sana,
Huyu bwana mdogo ni "mjanja mjanja" mno alichowafanyia wazungu miaka ya nyuma walijuta kumuamini akakimbia na nchi kwenda kuishi barani Asia.😂😂.

Mwisho kabisa he's so damn smart upstairs na kila move anayofanya kwenye maisha yake huwa well calculated, hata hapo kwa ruto tujipe muda tu.
Mhhh
 
Back
Top Bottom