joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,617
Kwanini tatizo hili lipo zaidi Kenya kuliko nchi nyingi za Africa?, unataka kutuambia watoto wa Kenya wanazaliwa wakiwa na tatizo la mtindio wa ubongo?, sio kweli kama mtoto utamuandalia mazingira mazuri ya kuishi akimbie na kurudi barabarani aokoteze chakula majalalani, kama wapo watakaorudi hawazidi asilimia moja, hata huku Tanzania tunao, ila tuna mfumo mzuri wa kuwakusanya na kuwaweka katika vituo bora kama vile, The child on the Sun, SOS na vituo mbali mbali vya watoto yatima.Kuna wale hata ukiondoa vipi wanarudi, ipo siku tuliwakusanya na kuwapeleka kwenye makao ya watoto ambapo tumewekeza sana lakini wakaanza kutiririka mjini mmoja mmoja. Siku nyingine tukakusanya waliotimiza umri na kuwaingiza NYS (kama JKT yenu), hata hawakumaliza wiki, wakakimbia wengi na kurudi barabarani.
Ni shughuli ya kijamii, hata Marekani wapo kwa wale wazungu ambao huwa mnawapa makinikia na wametajirika hadi basi.
Tofauti inayojitokeza kati ya Kenya na Tanzania ni urithi wa siasa za Kibepari zisizojali hali za maisha ya watu masikini, kujali mali na pesa kuliko UTU wa mtu ambao ndiyo msingi wa Ujamaa wa Nyerere, haya tunayoyaona sasa hivi ya Kenya kuwa na watoto wengi wa mtaani, unemployment rate kubwa, na population kubwa below poverty line pamoja na uchumi mkubwa kuliko TZ ni athari za Mfumo wa uchumi wa kibepari, kila kitu kina faida na hasara zake, hizi ndizo hasara za ubepari mkubali kuishi nazo.
Sent using Jamii Forums mobile app