Wakenya ndio ndugu na marafiki wa kweli wa Tanganyika

Wakenya ndio ndugu na marafiki wa kweli wa Tanganyika

Tajiri Tanzanite

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2016
Posts
3,078
Reaction score
5,882
Hapo vip!!

Katika nchi za afrika mashariki na Afrika kwa ujumla,sijawahi kuona nchi inayoipenda nyingine kama kenya wanavyoipenda Tanzania na watanzania kwa ujumla.

Nadhani hii nature kati ya kenya na Tanzania utaiyona kwa Marekani,uingereza,ujeruma,canada na Israel ila pia hii ya kenya kwa Tanzania ni zaidi.

Kenya imefanya kazi kubwa sana kupaza sauti juu ya ushetani na ukatili wa mauwaji,utekaji na ufisadi unaendelea Tanganyika na wakenya wanaumia kuliko hata baadhi ya watanzania.Hata kipindi cha maandamano na hali ya kuzimwa kwa mitandao wakenya walikuwa wanaitarifu dunia ushetani na vitendo vya kuzimu wanayofanyiwa watanganyika.

Nimefikiria na nikaona ni ile nature ya sisi na wakenya kuwa na usiano wa kidamu kuliko nchi yeyote duniani..mfano makabila yafuatayo yapo kwa wingi katika hizi nchi 2.wamasai,waarusha,wameru,wakurwa,wajaluo,wapare n.k

Nb.mtanganyika yeyote ukimkuta mkenya popote ndani ya nchi au duniani,jua umekutana na ndugu yako anayekupenda na anayekutakia mema na wewe mpende na mpe ushirikiano.

Nadhani baadaye Tanganyika ifikirie namna ya kuungana na ndugu zao wakenya iwe shirikisho au jamuhuri moja.

Wakenya tunawapenda sana
 
Rafiki wa kweli utamjua nyakati za shida .

Wakenya ndio ndugu zetu halisi.

Kenya wapo wakurya[wakuria] , wamasai, wajaluo sambamba na Tanzania japo hawajawahi kuonana wa upande mmoja na wa pili ila yatokeapo matatizo wanaguswa .

Hawa ndio ndugu zetu tuliotakiwa kuwa na muungano nao.

Zanzibar hakuna jamii hata moja kiasili katika kabila tajwa hapo juu.
 
Muda itazungumza ila naona baadaye Tanganyika na kenya ikiwa kitu kimoja
Rafiki wa kweli utamjua nyakati za shida .

Wakenya ndio ndugu zetu halisi.

Kenya wapo wakurya[wakuria] , wamasai, wajaluo sambamba na Tanzania japo hawajawahi kuonana wa upande mmoja na wa pili ila yatokeapo matatizo wanaguswa .

Hawa ndio ndugu zetu tuliotakiwa kuwa na muungano nao.
 
Wakenya na watanzania ni ndugu kabisa, watanzania wakipata shida wakenya huumia sana. Huu msala wakenya wameubeba kama wao. Media zao ziliripoti kinagaubaka wakati media za tanzania zilikula kubisi kuhabarisha msala wote uliotokea
 
bila ya wakenya tungemalizwa kama kuku, na hakuna mtu angejua wama kujali, wametusaidia sana, na ikiendelea hivi nina wasi wasi hata wakamvamia kijeshi kutuokoa, naona tu jinsi mambo yanavyokwenda ndivyo sivyo ...
 
Ukiacha mipaka ya kikoloni nadhani jamii za wa Kenya na wa Tanzania wanamuingiliaono mkubwa sana kuliko majirani wengine wa Afrika mashariki.
Mfano mombasa na Tanga ni kama jamii moja, wakurya, wajaluo, wakamba na wachaga wapo Kenya na Tz, pia lugha ya kiswahili inazungumzwa sana Kenya na Tz. Kiufupi Tz na Kenya ni ndugu wa karibu sana na ni watani wa jadi.
 
Back
Top Bottom