MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
Mabalozi wote wa Tanzania wanaoiwakilisha kwenye mataifa yaliyo ndani ya muungano wa Ulaya wameamrishwa na hao wazungu mara moja kila mmoja aende kwenye nchi husika na kuitetea Tanzania ili kuepukana na adhabu wanayoendelea kuipa Tanzania.
Pamoja na kwamba huwa tunataniana humu na Watanzania lakini hii imeanza kuniuma balaa, kwamba hawa wazungu mbona huwa wamefumba macho kwenye nchi za waarabu ambapo mashoga huchinjwa kabisa tena kwa mujibu wa sheria za nchi, kwanini likija kwa Afrika huwa wanapiga makelele utadhani mashoga wanauawa kwa halaiki. Mawaziri wa Tanzania wamejitokeza na kujitetea na kusema ilikua kauli ya mkuu wa mkoa lakini jamaa wanaendeleza kipodo na vurugu bila kuachia.
Hili la ushoga pona yetu rais Uhuru alilijibu kwa kutumia akili alipobanwa mbele ya Obama, maana kama naye angebwatuka naona tungechezea mateso wanayopitia wenzetu. Yeye alisema sio kipau mbele kwa sasa kwenye nchi yetu, tuna mengine mengi ya kuwaza, nafikiri kama angefyatuka kama wabongo eti tutawafuata mashoga mlango kwa mlango, hatungepona.
Kwa nguvu inayotumika dhidi ya Tanzania ni wazi kuna lingine, sio bure, maana hata Museveni alipofyatuka, alinyamazishwa na yakaisha, hawakuendelea kumfuata fuata, lakini kwa Tanzania wamekomaa, ni kama walikua wanasubiri mlango wa kuingilia, hadi nashuku chokochoko yote hii ina kauhusiano fulani na suala la makinikia.
Nadiriki kusema Wakenya tujilinde kwa kukumbatia Uchina likija suala la ufanikishaji wa miradi yetu, wale huwa hawafuatilii unachokula au unaishi vipi, kufikia sasa tumeona walivyofanikiwa kukamilisha miradi mikubwa ndani ya nchi yetu, tujiondoe kabisa kwenye kumi na nane ya hawa wazungu maana ni maisha ya utumwa kabisa.
Hii hapa taarifa ya jinsi wameamrisha mabalozi wote wa Tanzania wakajitetee na kubembeleza Tanzanias ambassadör i Sverige kallad till UD