Wakenya tuendelee kukumbatia Uchina ili kuepukana na adhabu wanayopokea wenzetu wa Tanzania

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Mabalozi wote wa Tanzania wanaoiwakilisha kwenye mataifa yaliyo ndani ya muungano wa Ulaya wameamrishwa na hao wazungu mara moja kila mmoja aende kwenye nchi husika na kuitetea Tanzania ili kuepukana na adhabu wanayoendelea kuipa Tanzania.

Pamoja na kwamba huwa tunataniana humu na Watanzania lakini hii imeanza kuniuma balaa, kwamba hawa wazungu mbona huwa wamefumba macho kwenye nchi za waarabu ambapo mashoga huchinjwa kabisa tena kwa mujibu wa sheria za nchi, kwanini likija kwa Afrika huwa wanapiga makelele utadhani mashoga wanauawa kwa halaiki. Mawaziri wa Tanzania wamejitokeza na kujitetea na kusema ilikua kauli ya mkuu wa mkoa lakini jamaa wanaendeleza kipodo na vurugu bila kuachia.

Hili la ushoga pona yetu rais Uhuru alilijibu kwa kutumia akili alipobanwa mbele ya Obama, maana kama naye angebwatuka naona tungechezea mateso wanayopitia wenzetu. Yeye alisema sio kipau mbele kwa sasa kwenye nchi yetu, tuna mengine mengi ya kuwaza, nafikiri kama angefyatuka kama wabongo eti tutawafuata mashoga mlango kwa mlango, hatungepona.

Kwa nguvu inayotumika dhidi ya Tanzania ni wazi kuna lingine, sio bure, maana hata Museveni alipofyatuka, alinyamazishwa na yakaisha, hawakuendelea kumfuata fuata, lakini kwa Tanzania wamekomaa, ni kama walikua wanasubiri mlango wa kuingilia, hadi nashuku chokochoko yote hii ina kauhusiano fulani na suala la makinikia.

Nadiriki kusema Wakenya tujilinde kwa kukumbatia Uchina likija suala la ufanikishaji wa miradi yetu, wale huwa hawafuatilii unachokula au unaishi vipi, kufikia sasa tumeona walivyofanikiwa kukamilisha miradi mikubwa ndani ya nchi yetu, tujiondoe kabisa kwenye kumi na nane ya hawa wazungu maana ni maisha ya utumwa kabisa.

Hii hapa taarifa ya jinsi wameamrisha mabalozi wote wa Tanzania wakajitetee na kubembeleza Tanzanias ambassadΓΆr i Sverige kallad till UD
 
MNAFKI NA MUONGO NA UNAENEZA HABARI FEKI TANZANIA HATUSHOBOKEI MTU WALA TAASISI YYTE WATAKUJA WENYEWE
 
Akili za kima hizi..Eti Kenya ikumbatie Uchina na Juzi tu Uhuru alikuwa ulaya kuzungusha bakuli😝😝😝
Wazungu wana wakula tigo na wachina wana wapiga bakora za matako hii yote sababu ya kuzungusha bakuli..
Afadhali JPM hata kama bado lazima azugushe bakuli, anajitahidi kutumia pesa zake za ndani angalau kupunguza ujinga..
Naona wazungu wana zimezea mate sana tigo za wa Tz, wanajua kenya kupata tigo ni kazi rahisi
 
Bongo inalazimishwa kuwa taifa la mashoga. Ni aibu sana
 
Wacha wee, Balozi wa Tanzania nchini Sweden aitwa na serikali ya Sweden kuhusu ufafanuzi wa waharakati zinazoendelea nchini Tanzania. Tanzania haijamtuma balozi wake akajielezee, ameitikia diplomatic summon.
Hatutafeli kama nchi kwa kunyimwa mikopo, mikopo ipo tu hata leo WB imetoa mkopo wa $300 millions.
Africa kwenye suala la ushoga tunashindwa kujinasua kwasababu taratibu zetu zimevurugwa. Mapadri wakianza kuhubiri kuukubali ushoga tu basi kwetu itakua kitu cha kawaida sana. Tungekua na dini na taratibu zinazokataza tungekua salama. Waarabu wana taratibu zao tangu karne ya 5 kwahiyo inaeleweka.
 
Bongo inalazimishwa kuwa taifa la mashoga. Ni aibu sana
wapi limelazimishwa.... wao wanachokiongelea n haki za binadam kwa maana hujamkamata mtu akiwa anakifanya hicho kitendo unaanza kumsimanga na ndo tatzo lilipoanza Ila Kama wangeshikwa kabisa red handed basi Hakuna WA kusema lolote. na sio kwa message za watu au hisia za watu
 
Waambie hao tena makamu WA raisi
WA BENK YA DUNIA AMEKUJA MWENYEWE NA AMEKUBALI KUTOA ILE DOLA MIL. 300 ILIYOKUWA IKIPIGIWA MISUMARI KUWA TUMECHINJIWA BAHARINI KISA MASHOGA
 
Haha
Ha kaka huo utani WA kibua au unamanisha kweli kuwa wadhungu wanataman Tigo za watz.. Ila Leo wamekuja WB makamu WA rais WA upande WA Africa na wamekubal kutoa zile $300 MIL. Sa sijui wameruhusiwa kula Tigo zetu ama wamesarenda
 
World Bank TodayπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡Tanzania ni nchi yenye asaliπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ‘‡πŸ˜ŠπŸ˜ŠπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
 
World Bank todayπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
 
Hii kutoka Africa Develepment BankπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡Tanzania sio nchi ya kuchezeaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
MNAFKI NA MUONGO NA UNAENEZA HABARI FEKI TANZANIA HATUSHOBOKEI MTU WALA TAASISI YYTE WATAKUJA WENYEWE
Mkuu umesoma vizuri alicho andika na kushauri huyu ndugu MK254 ?
Jamaa ameongea ukweli na kwa mapenzi mema sio tu kwa Kenya bali Tanzania na Africa yote.

Hapa jamaa kaweka ushabiki wa kitoto pembeni.
 
Tanzania huwa aiteteleki kamwe.. Swala EPA kutoka EU tumegoma sasa wanasambaza propaganda kupitia media zao huko kunyaland
 
Nyie WaKenya.
Tanzania ni Nchi huru na tutabaki hivyo milele, hakuna Taifa Duniani lenye haki ya kutupangia Jamii yetu itakuwaje wala kuingilia Utanzania wetu kisa hatuishi kama wao.

Nyie wakenya endeleeni kuwakumbatia watu wanaowashika makalio
 
Mkuu umesoma vizuri alicho andika na kushauri huyu ndugu MK254 ?
Jamaa ameongea ukweli na kwa mapenzi memo sio tu kwa Kenya bali Tanzania na Africa yote.

Hapa jamaa kaweka ushabiki wa kitoto pembeni.
World Bank kapangua hizo Taarifa. πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Leo mkuu wao kusema atatoa hizo pesa nakuendelea kufadhili miradi mingineπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡ Jana AD Bank pia kuleta billionsπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Mkuu umesoma vizuri alicho andika na kushauri huyu ndugu MK254 ?
Jamaa ameongea ukweli na kwa mapenzi memo sio tu kwa Kenya bali Tanzania na Africa yote.

Hapa jamaa kaweka ushabiki wa kitoto pembeni.
China sisi niswala lakugusa alafu wanacheuwa.. China sisi hutupatia grants.. China na Tanzania huwezi kuitenga kamwe. Huwa tunawasimamia sana huko UN. πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡Latest from China. Endeleeni kupeleka vikapuπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…