Wakenya tujivunie, tuzidi kuwa wajasiri na tutembee vifua 'mbere': Miaka miine ya uoga, kunyamazishwa na kukandamizwa nchini Tz- Amnesty International

pingli-nywee

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2015
Posts
11,923
Reaction score
13,350
Tanzania crackdown on dissent sowing fear and stifling human rights As long as am quiet, am safe- Maneno ya Human Rights Watch kuhusu uhuru wa wananchi na haki za kibinadamu kwa majirani zetu Tz. Amnesty International wametoa ripoti kuhusu ukandamizaji wa haki ya kujieleza na ya kutangamana kwa amani kisiasa nchini Tz. A. Int na HRW wameiweka Tz kwenye darubini kuhusu ukiukaji wa mikataba ya kimataifa, ambayo Tz ilitia saini; kulinda haki za kibinadam na uhuru wa wananchi, wa kujieleza. Kando na kuua, kuteka na kunyamazisha upinzani na wanahabari. Ukiangalia masuala yalioangaziwa utashangaa kuona kwamba ni vitu simpo tu na vya kawaida sana. Km. mashirika haya mawili yametaja kufungwa kwa radio ya Swahiba Fm baada ya wao kuripoti kuhusu kufutiliwa mbali kwa uchaguzi Zanzibar mwaka wa 2015. HRW kuzuiwa na GoT kutoa taarifa kuhusu vijakazi wa kitz wanaoteswa Oman na Dubai! [emoji15]
 
Kitu hunifurahisha kwa Wakenya ni jinsi huwa tunaungana kulaani ukiukwaji wowote wa haki za kibinadamu, unakuta hata mtu ambaye hushabikia serikali anaibadilikia na kuikosoa, ila kwa wenzetu nilishangaa sana jamaa wa CCM wanashangilia pale Tundu Lissu alipigwa risasi 38.
 
Eti leo hii usikie kwamba rais Uhuru amepiga marufuku shughuli zote za vyama vya kisiasa hadi 2022, tena vyama vya upinzani pekee yake! Alafu eti wakenya wanyamazie hivyo tu bila kumpa jibu wakati ni haki yao tena live kwenye katiba? Vitu ambavyo Amnesty International na Human Rights Watch wanazungumzia ni vitu ambavyo ukisikia vinafanyika Afrika Mashariki utaona aibu. Naona wameangazia sana Twaweza walivokatazwa kutoa ripoti kuhusu kura yao ya maoni 'Sauti za Wananchi'. Ambayo ilikuwa inaashiria kwamba umaarufu wa mzee ulikuwa umepungua kwa kiasi kikubwa. Kwa kweli hiyo move ilikuwa ya kiboya kupindukia, hivi mzee huwa hana watu wa kumshauri?
 
Kwa hiyo Tanzania yetu ndo kipimo cha furaha na maisha ya Wakenya?
Hapana. Ila naona mwenzako ametoa jibu murua sana kwa swali lako hata kabla hujaliuliza.
Tusaidiane kuwaombea "LAANA na MAANGAMIZO" chama cha CCM, au lasivyo tutakimbilia kwenu kama Tanzania ikiingia kwenye machafuko. Mjiandae kisaikolojia tu kwa hilo.
Kuna kitu kinaitwa EAC, haki za kibinadamu zinapotupiliwa mbali tunachafuliwa hata na sisi ambao tupo pembeni. Haingii akilini kabisa kwamba muongo mmoja uliopita rais wenu JK alivuka mpaka kuja kumpa Koffi Annan support kwenye shughuli ya kuwapatanisha wakenya. Sasa hivi ni nani ambaye ana 'moral authority' ya kufanya vitu kama hivyo ukanda huu wote? Ug, Rwanda, Burundi, S.Sudan, Somalia, Ethiopia?
 
Hakika hakuna mtu mwenye calibre hio ya morality. God bless the dead.
 
Naapa kila kitu ni ukweli mtupu....kasoro hapo kwenye waTz kutumikishwa Oman,,hapo tusimlaum magufuli bali tumlaum mwanzilishi Muhammad.... Unajua M zinachanganyaga sometimes
 
Naapa kila kitu ni ukweli mtupu....kasoro hapo kwenye waTz kutumikishwa Oman,,hapo tusimlaum magufuli bali tumlaum mwanzilishi Muhammad.... Unajua M zinachanganyaga sometimes
Wala halaumiwi, ila kuwashurutisha Human Rights Watch wasitoe taarifa hiyo kuhusu watz wanaoteswa uarabuni ni jambo la busara kweli? Kenya taarifa kama hizo zilivochimbuka wakenya walifahamishwa kila kitu na mashirika husika na wanahabari pia. Wakenya nao kupitia viongozi wao wakaliamsha na mashirika yote, 'agencies' zilizokuwa zinawahadaa wakenya ambao wanatafuta ajira zikapigwa marufuku. Hadi mabalozi wa nchi za uarabuni wakahojiwa ili suluhisho lipatikane.
 
Tanzania ya Sasa ndio Kenya ya 80s. Saa Hii ndio Watanzania wanaanza kugutuka. They are 30 years behind Kenya na Ni kweli juu hata GDP zimeachana kwa kiasi hicho Cha $30 billion...10 for each decade.
Wananikumbusha enzi za KANU na majasusi wa Moi walivokuwa wanawavamia wananchi usiku wa manane. Eti kwasababu kwenye mikutano hawakunyoosha kidole kimoja juu kuashiria kwamba wao ni KANU damu.
 
Wananikumbusha enzi za KANU na majasusi wa Moi walivokuwa wanawavamia wananchi usiku wa manane. Eti kwasababu kwenye mikutano hawakunyoosha kidole kimoja juu kuashiria kwamba wao ni KANU damu.
Huu upumbavu ulitokea lini Tanzania?

Mnachekesha mnavyojifanya mnawadhibiti wanasiasa kwenye uhuru wenu wa habari na siasa lakini wanawaibia na kuwatapeli mpaka huruma. Mbaya zaidi wanawafisadi billions of dollars na njaa inawauwa
 
Huu upumbavu ulitokea lini Tanzania?
Mnachekesha mnavyojifanya mnawadhibiti wanasiasa kwenye uhuru wenu wa habari na siasa lakini wanawaibia na kuwatapeli mpaka huruma. Mbaya zaidi wanawafisadi billions of dollars na njaa inawauwa
Jombaa, kwani KANU ilikuwa Tz? Mnanikumbusha kuhusu enzi hizo za KANU kwasababu waliotutangulia waliishi kwa uoga kama wenu. Nakuelewa lakini kwasababu najua unaogopa kulimbikiziwa kesi ya kubaka na kuhujumu uchumi. Ndio maana hata mkulu alipotafuna 1.5 Trillion hukuwa na ujasiri kama ulionao sasa hivi, wala ubavu wa kuhoji. 'Anayetoka chumbani kwa mama yako na taulo huyo ndiye babako'. Hiyo sentensi moja tu inaashiria ujeuri wa viongozi wa chama chenu na serikali yenu na wanavowabeba kama malofa.
 
Ni masikitiko makUbwa sana,,, na huzuni, na simanzi, na aibu kuona yanayotendeka kwa nchi yetu Tanzania kila kukicha. Sijui ni lini Tanzania tutakua na akili kama Wakenya.
 
Ni masikitiko makUbwa sana,,, na huzuni, na simanzi, na aibu kuona yanayotendeka kwa nchi yetu Tanzania kila kukicha. Sijui ni lini Tanzania tutakua na akili kama Wakenya.
Wewe endelea tu hivyo ndugu yangu. Walipitisha sheria ya kuwachunguza na kuwafata wapinzani hadi kwenye cyber. Tena bila order kutoka kwa mahakama. Utatekwa na wasiojulikana, wakukabe kweli kweli kwenye m*p#mb# hadi ukubali kila watakachokuambia. Alafu baadaye wakutupe kichakani ukiwa nusu hai. Baada ya hapo lazima utashika adabu zako na uanze kuimba hitsong ya haleluya sisiemu.
 
Nyie si mmesema.mnataka tuwape.magufuli na nyie mtupe uhuru na odinga..


Sasa tumepitisha maamuzi ya kuwapa hata ccm na viongozi wake wote bure


Sent using Jamii Forums mobile app
Jaribuni kwa waganda au wahabeshi. Huo ulikuwa ni uongo tu wa kutafuta kiki za kisiasa. Ukizingatia kwamba wakenya walitawalwa kidikteta kwa miaka 24. Sidhani kama kuna mkenya mwenye akili timamu ambaye ana hamu ya kurudi kwenye enzi hizo.
 
Lol Tanzania haipo kwenye hiyo level ya kanu

Halafu ni trillion 4 sio 1.5
Kwa mtu anayejua nini maana ya trillion hawezi kuamini hizo hekaya

Ufisadi uliotikisa Tanzania mpaka baraza la mawaziri likavunjwa ni ufisadi wa billion 350, na hizo pesa zilidundulizwa kwenye escrow account kwa zaidi ya miaka 30 ndio ije kuwa trillion 4 ziibiwe ndani ya miezi 4 ya ukaguzi wa mahesabu ya CAG? Tanzania haina huo uchumi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…