Wakenya tujivunie, tuzidi kuwa wajasiri na tutembee vifua 'mbere': Miaka miine ya uoga, kunyamazishwa na kukandamizwa nchini Tz- Amnesty International

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]hapa ndio huwa sioni tofauti ya mkenya na kitimoto.

kwani sasa hivi sio kazi tena iliwatoa huko.

na mbona bado mnapewa mpaka mahindi ya msaada[emoji23][emoji23][emoji23]

Uchapa kazi ulichangia pakubwa, ila kazi huku ukiogopa ogopa hauwezi ukafanikisha mengi. Nilikua nasoma taarifa za yanayomsibu Kabendera kwenu huko, mpaka mama yake kafariki kwa pressure ya mwanaye kuteseka, yote hayo kisa jamaa kakosoa serikali, mwenzake Tundu Lissue marisasi yalimuondoa kwenye nchi na hana uthubutu wa kukanyaga kwenye ardhi ya mababu zake.
Kwa sasa ushauri wangu kwenu, mshindane misifa, kila mtu asifie na kuimba mapambio maana dah noma huko, msituige uhuru wetu huu hata kidogo maana usitake uwe kafara.
Mjikite kwenye kusifia tu, bana pua, funga macho wewe sifia tu, imba tena uwe kama chizi, kitaani ufahamike kama CCM damu, vaa mavazi na sare za chama, chumbani weka bendera kabisa, kila siku waza CCM, hata ofisini/kanisani/msikitini wakufahamu kama "Yule jamaa wa chama".
Hapo utaishi kwa amani, shughuli zako zitaenda....uwe kama huyu jamaa kwenye hii picha

uhuru bila mipaka ni uwendawazimu.

umoja wa kitaifa ni jambo la msingi kuliko upuuzi au mpuuzi yeyote.
 
uhuru bila mipaka ni uwendawazimu.

umoja wa kitaifa ni jambo la msingi kuliko upuuzi au mpuuzi yeyote.

Ndio maana kuna sheria, hata Marekani hawana uhuru bila mipaka, sheria zipo zimechora mistari wapi uhuru wa kila mmoja unaanzia na kuishia.
Sema kuna shitholes ambapo huo uhuru unabanwa kabisa, yaani hawaachi hata mwanya wa kupumulia, ukiwa kijiweni umkosoe rais, ukiondoka tu, jamaa fulani hivi wanakuibukia, na kuanzia hapo utatafutwa hutapatikana. Tuliwahi kuishi hayo maisha, ovyoo sana dah...
 
unadhani hakuna anayemkosoa rais tz!!

shida wengi wanaongozwa na mihemko na hasira,wanajikuta wanaongea mambo yasiyohusika.mfano tuchukulie ile la kutoonekana kwa tsh t1.4 na mkaguzi wa serikali,mkrupukaji mmoja anakaa kijiweni atie kamba wenzie kwamba magu kapeleka hizo hela kwao!!!
 
Mbona hiyo kawaida sana, rais kusemwa kwamba kafisadi hapa Kenya na duniani kote huwa wanasemwa sana, kasoro ya kule Korea kwa Kim na sasa hapo Tz.
Mkaguzi akisema haoni hela, na hazitolewi maelezo wapi zilipo, basi kuna kitu kinaitwa "where buck stops", hapo kete inasimama kwa rais, ndiye mwenye dhamana.
Yeye hapo ameajiriwa na hao maskini kitaani, akapewa jukumu la kuteua nani afanye naye kazi, akiajiri mijizi, lawama zinaishia kwake, hapaswi aamrishe kamata kamata kwa kila anayemshuku.
 
Jibu la huyo Madenge kwa kila shutma ni kwamba 1Trillion TZSHS haziwezi zikaliwa kifisadi, wakati CAG alitoa ripoti inayoashiria kwamba zilitafunwa. Nadhani ule wali ambao hawa watu huwa wanalishwa wakati wa kampeni una nguvu za ajabu kupindukia.
 
Nchini mwenu kulikuwa na kubanwa kwa uhuru na viongoz kutokufnya kaz.. ss kazi inapigwa ttzo n uhuru wa kuongea tu....
 
Jibu la huyo Madenge kwa kila shutma ni kwamba 1Trillion TZSHS haziwezi zikaliwa kifisadi, wakati CAG alitoa ripoti inayoashiria kwamba zilitafunwa. Nadhani ule wali ambao hawa watu huwa wanalishwa wakati wa kampeni una nguvu za ajabu kupindukia.
Trillion moja hazikuliwa.. zilifanyiwa matumiz ambayo hayakupitishwa na bunge!! Tr 1.5 ni sawa na US $680billion.. pesa kubwa kam hiyo haiwez kuibwa katk nchi ya kiafrika na pengo lake lisionekne
 
Suala la rushwa ufisadi na mikataba mibovu mnalo mpka leo... SGR si mmesain juz tu!! Uhuru wenu wa kuongea hujawasaidia kitu kama vitu nyeti kama hivyo mnashindwa kuvizuia
 
Suala la rushwa ufisadi na mikataba mibovu mnalo mpka leo... SGR si mmesain juz tu!! Uhuru wenu wa kuongea hujawasaidia kitu kama vitu nyeti kama hivyo mnashindwa kuvizuia

Hili la SGR huwa naliskia kwa Watanzania, mnaimba sana kuhusu SGR SGR ya Kenya, inawapa tabu sana ila ipo inafanya kazi kutokea Mombasa hadi Naivasha, reli ya kisasa ambayo haipo ukanda wote huu, hamna nchi yenye SGR nyingine hapa Afrika Mashariki, huwa naski kwenu huko kunayo mnajaribu kujenga ila hadi mgurumishe tuone mizigo na abiria itabaki stori za vijiweni maana Watanzania tunawajua sana kwa kujikweza.
 
mbana mnamsema uhuru na bado anawapiga pesa!!

hawagusi sababu ni kweli anawawasha.
 
Jibu la huyo Madenge kwa kila shutma ni kwamba 1Trillion TZSHS haziwezi zikaliwa kifisadi, wakati CAG alitoa ripoti inayoashiria kwamba zilitafunwa. Nadhani ule wali ambao hawa watu huwa wanalishwa wakati wa kampeni una nguvu za ajabu kupindukia.
unaweza nionyesha CAG aliposema zimeliwa!!au unadhani tz ni kama kenya hapo watu wanakula kula tu hela za ngedere???
 
Trillion moja hazikuliwa.. zilifanyiwa matumiz ambayo hayakupitishwa na bunge!! Tr 1.5 ni sawa na US $680billion.. pesa kubwa kam hiyo haiwez kuibwa katk nchi ya kiafrika na pengo lake lisionekne
huyu mpuuzi ni hasara kwa kenya nzima.anajibu jibu lolote kwenye swali.
 
mbana mnamsema uhuru na bado anawapiga pesa!!

hawagusi sababu ni kweli anawawasha.
Tolea mfano wa wapi ametupiga, tunamsema na tutamsema maana ufusadi wowote nchini yeye ndiye mwenye jukumu la kukomesha, japo anajaribu sana ila lazima tumseme asije kulegea, huku kwetu kutuongoza lazima ukubali kusemwa.
 
Aiya mchina atachukua bandari... kuweni makini jamen...
 
Trillion moja hazikuliwa.. zilifanyiwa matumiz ambayo hayakupitishwa na bunge!! Tr 1.5 ni sawa na US $680billion.. pesa kubwa kam hiyo haiwez kuibwa katk nchi ya kiafrika na pengo lake lisionekne
unawazimu wewe? karne hii, madafu trillioni 1.5 haitawahii kuwa Dollar billioni 680.
 
Tolea mfano wa wapi ametupiga, tunamsema na tutamsema maana ufusadi wowote nchini yeye ndiye mwenye jukumu la kukomesha, japo anajaribu sana ila lazima tumseme asije kulegea, huku kwetu kutuongoza lazima ukubali kusemwa.
kuwapiga sio kuwapiga fimbo mzee,kuwaibia namaanisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…