Wakenya tujivunie, tuzidi kuwa wajasiri na tutembee vifua 'mbere': Miaka miine ya uoga, kunyamazishwa na kukandamizwa nchini Tz- Amnesty International

Wakenya tujivunie, tuzidi kuwa wajasiri na tutembee vifua 'mbere': Miaka miine ya uoga, kunyamazishwa na kukandamizwa nchini Tz- Amnesty International

Lol Tanzania haipo kwenye hiyo level ya kanu

Halafu ni trillion 4 sio 1.5
Kwa mtu anayejua nini maana ya trillion hawezi kuamini hizo hekaya

Ufisadi uliotikisa Tanzania mpaka baraza la mawaziri likavunjwa ni ufisadi wa billion 350, na hizo pesa zilidundulizwa kwenye escrow account kwa zaidi ya miaka 30 ndio ije kuwa trillion 4 ziibiwe ndani ya miezi 4 ya ukaguzi wa mahesabu ya CAG? Tanzania haina huo uchumi
Maajabu haya, yaani umeketi mkao wa kuliwa hadi unawatetea mafisadi? Huo hata sio uoga ni ukichaa wa hali ya juu. Sitashangaa ukianza kutetea chama chenu na ukiukaji wao wa haki za kibinadam. Alafu hii yenu ni zaidi ya KANU maanake miaka yote ya utawala wa Moi hakufanikiwa kuwanyazisha wala kuwadhibiti wakenya. Kwenu uoga umetanda hadi kukohoa tu imekuwa ni shida.
 
I support you at 100% ....Kwenye swala la haki za binadamu TZ tupo sehemu mbaya...Kiukweli ukweli usemwe..
 
Yenu wakenya mbaki nayo na sisi tuachie Tanzania yetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapa tunajadili ripoti ya Amnesty International na Human Rights Watch. Mlijikaanga wenyewe mlipotia saini mikataba ya kimataifa kuhusu haya haya ambayo tunayajadili. Wenzenu wanakesha humu wakiijadili Kenya na kuiponda huku wakituaminisha kwamba nchi yao ni ya asali na maziwa, ya amani na eti ni dona kantri. Itabidi umeze tu jombaa, hata kama ni chungu kama shubiri.
 
Tanzania crackdown on dissent sowing fear and stifling human rights As long as am quiet, am safe- Maneno ya Human Rights Watch kuhusu uhuru wa wananchi na haki za kibinadamu kwa majirani zetu Tz. Amnesty International wametoa ripoti kuhusu ukandamizaji wa haki ya kujieleza na ya kutangamana kwa amani kisiasa nchini Tz. A. Int na HRW wameiweka Tz kwenye darubini kuhusu ukiukaji wa mikataba ya kimataifa, ambayo Tz ilitia saini; kulinda haki za kibinadam na uhuru wa wananchi, wa kujieleza. Kando na kuua, kuteka na kunyamazisha upinzani na wanahabari. Ukiangalia masuala yalioangaziwa utashangaa kuona kwamba ni vitu simpo tu na vya kawaida sana. Km. mashirika haya mawili yametaja kufungwa kwa radio ya Swahiba Fm baada ya wao kuripoti kuhusu kufutiliwa mbali kwa uchaguzi Zanzibar mwaka wa 2015. HRW kuzuiwa na GoT kutoa taarifa kuhusu vijakazi wa kitz wanaoteswa Oman na Dubai! [emoji15]

Ah haa
Hii taarifa mbona ni ya kitambo?
Na hamna jipya linaloelezwa?
Ulivyo shadadia nilifikiri it's a new report.
 
Ah haa
Hii taarifa mbona ni ya kitambo?
Na hamna jipya linaloelezwa?
Ulivyo shadadia nilifikiri it's a new report.
Kitambo ni lini boss? Nilitegemea utabisha useme ripoti hiyo ni ya uongo au uwalaumu mabeberu kama kawa.
 
Maajabu haya, yaani umeketi mkao wa kuliwa hadi unawatetea mafisadi? Huo hata sio uoga ni ukichaa wa hali ya juu. Sitashangaa ukianza kutetea chama chenu na ukiukaji wao wa haki za kibinadam. Alafu hii yenu ni zaidi ya KANU maanake miaka yote ya utawala wa Moi hakufanikiwa kuwanyazisha wala kuwadhibiti wakenya. Kwenu uoga umetanda hadi kukohoa tu imekuwa ni shida.
mkuu acha ujinga ni hasara kwa watoto wako.

akikwambia mtu,uhuru ameiibia kenya 200bln unachukua masaa mangapi kutafakari hili kabla utoke ndani ya nyumba yako ukiwa frustrated!!!
 
Kitu hunifurahisha kwa Wakenya ni jinsi huwa tunaungana kulaani ukiukwaji wowote wa haki za kibinadamu, unakuta hata mtu ambaye hushabikia serikali anaibadilikia na kuikosoa, ila kwa wenzetu nilishangaa sana jamaa wa CCM wanashangilia pale Tundu Lissu alipigwa risasi 38.
Vipi wakenya viongozi wenu walishatubu kuhusu ukandamizwaji wa haki za binadamu wanaofanya au tuwaache kama mlivyo ?
 
1577644601711.png

Ripoti zinasema Evans Njoroge, mwanafunzi ambaye alikua kiongozi Chuo kikuu cha Meru nchini humo, aliuawa kwa kupigwa risasi na anayedaiwa kuwa polisi.

Mwandishi wa BBC, Ferdinand Omondi anasema pichaza mwili wa kijana huyo, damu yake ikionekana imetapakaa kote, zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii huku raia wa Kenya wakighadhabishwa na kile walichodai kuwa mauaji yanayotekelezwa na polisi.

Evans alipigwa risasi Jumanne wakati wa maandamano ya wanafunzi waliokuwa wakilalamikia ongezeko la ada dhidi ya chuo cha Meru.

Vyombo vya habari nchini Kenya vimemnukuu shuhuda mmoja akisema polisi walimkimbiza Evans wakamfikia kisha mmoja wao akampiga risasi na kuondoka.
Mkuu wa polisi Jenerali Joseph Boinnet ameamuru kufanyika uchunguzi kuhusu kifo hicho baada ya kuwepo kwa wanasiasa na makundi ya wanaharakati waliokuwa wakitaka mauaji yanayodaiwa kutekelezwa na polisi kukoma mara moja.

Shirika huru la kiraia linalofuatilia shughuli za polisi (IPOA) limesema limewatuma maafisa wake kuchunguza tukio hilo.

Mwanafunzi huyo aliuawa katika eneo la Nchiru, eneo la Tigania West katika jimbo la Meru ambalo linapatikana katika eneo la Mlima Kenya.

IPOA wamesema maafisa wa uchunguzi wametukwa kwa lengo la: "kuchunguza kuhusu yaliyotokea wakati wa mauaji hayo na iwapo kuna mtu anayefaa kulaumiwa, na kuhakikisha afisa yeyote wa polisi atakayepatikana na hatia anawajibishwa kisheria."

Wakenya mtandaoni wamekuwa wakishutumu mauaji hayo.

Shutuma hizi mpya zimekuja siku kadhaa baada ya shirika linalotetea haki za binadamu la Human Rights Watch kuwasilisha ushahidi mpya kuwa polisi nchini Kenya waliua watu takriban 23 wakati wa kipindi cha marudio ya uchaguzi nchini humo mwaka jana.

Kwa mujibu wa ripoti,uchunguzi umebaini kuwa wengi wa waathirika walifyatuliwa risasi na silaha za nguvu.

Polisi wameendelea kukana shutuma hizo.

HIYO ILIKUWA MWAKA 2018
 
Mwaka huo huo wa 2018, afisa wa Polisi wa kitengo cha AP(Polisi wa Utawala), Leakey Maina akafikishwa mbele ya hakimu mjini Meru ili ajibu mashtaka kwasababu ya mauji ya Evans Njoroge. Yupo korokoroni hadi sasa hivi.
View attachment 1306748 Ripoti zinasema Evans Njoroge, mwanafunzi ambaye alikua kiongozi Chuo kikuu cha Meru nchini humo, aliuawa kwa kupigwa risasi na anayedaiwa kuwa polisi. Mwandishi wa BBC, Ferdinand Omondi anasema pichaza mwili wa kijana huyo, damu yake ikionekana imetapakaa kote, zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii huku raia wa Kenya wakighadhabishwa na kile walichodai kuwa mauaji yanayotekelezwa na polisi. Vyombo vya habari nchini Kenya vimemnukuu shuhuda mmoja akisema polisi walimkimbiza Evans wakamfikia kisha mmoja wao akampiga risasi na kuondoka.
 
mkuu acha ujinga ni hasara kwa watoto wako.

akikwambia mtu,uhuru ameiibia kenya 200bln unachukua masaa mangapi kutafakari hili kabla utoke ndani ya nyumba yako ukiwa frustrated!!!
1Trillion hela ya madafu si ni KES 42billion? Si huwa mnasema kwamba mnajenga kwa hela zenu, imekuwaje leo unasema kwamba hamna hela? Mnatumia logic ya kipuuzi sana kutetea ufisadi.
 
Kwa hiyo na huku Tanzania ndivyo hivyo hivyo au?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna tofauti gani kama habari moto moto ambazo huwa tunazipokea kutoka kwa media za kimataifa ni kwamba CCM imeshinda kwenye uchaguzi, kwa asilimia 99%! Walimu nao mnawatishiwa kwamba mtawalimbikizia kesi za kuhujumu uchumi wasipokichagua na kukiunga mkono chama tawala kwenye uchaguzi. Kuna tofauti gani?
 
1Trillion hela ya madafu si ni KES 42billion? Si huwa mnasema kwamba mnajenga kwa hela zenu, imekuwaje leo unasema kwamba hamna hela? Mnatumia logic ya kipuuzi sana kutetea ufisadi.
uhuru anaweza iba KES 42bilion!!!kisha anunue nini hapo kenya msijue!!!
 
uhuru anaweza iba KES 42bilion!!!kisha anunue nini hapo kenya msijue!!!
Acha utoto, tumia facts, ripoti ya CAG wenu ilionesha kwamba Tzsh2.4Trillion(zaidi ya KES 100Billion) zilitafunwa mwaka wa 2016/17. Rudi kwenye mada, ambayo ni kwamba hata wanahabari pia wamenyamazishwa. Hawewezi kabisa wakaripoti kuhusu ufisadi, hata kama ni wa milioni 10 tu.
 
Kitu hunifurahisha kwa Wakenya ni jinsi huwa tunaungana kulaani ukiukwaji wowote wa haki za kibinadamu, unakuta hata mtu ambaye hushabikia serikali anaibadilikia na kuikosoa, ila kwa wenzetu nilishangaa sana jamaa wa CCM wanashangilia pale Tundu Lissu alipigwa risasi 38.
Mkuu..haya ndio matatizo ya kuongozwa na kichaa.
 
Jinai ina ukitambo?! Kwa nini watanzania tunakubali kuwa mahohehahe!
Ripoti yenyewe ni ya mwaka huu huu 31, mwezi wa kumi. Ripoti nyingine ambayo Amnesty International wameitaja ni hii hapa ya Human Rights Watch. Ambayo waliitoa 28, Okt 2019 na wakajumuisha maoni kutoka kwa mahojiano ya watz zaidi ya 80 kwenye ripoti yao. Wanahabari, bloggers, wanachama wa upinzani, mawakili, NGO's n.k, n.k.
 
Kuna tofauti gani kama habari moto moto ambazo huwa tunazipokea kutoka kwa media za kimataifa ni kwamba CCM imeshinda kwenye uchaguzi, kwa asilimia 99%! Walimu nao mnawatishiwa kwamba mtawalimbikizia kesi za kuhujumu uchumi wasipokichagua na kukiunga mkono chama tawala kwenye uchaguzi. Kuna tofauti gani?
Ndiyo maana mabeberu hawapendi vyombo vya habari vya kipuuzi,,,
Tanzanite
Jenefa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom