Mimi na mtazamo tofauti kidogo na wewe, tukianzia kwa wasomali, wasomali wanachinjana kwasababu ya tamaa ya pesa. Wasomali wengi wanapenda pesa kuliko kitu kingine chichote, hakuna wa kumuachia mwingine na yeye ale. Kwa wao kabila moja, lugha moja na dini moja havija saidia kudumisha umoja wao, tamaa ya mali na pesa ndio inawatafuna Wasomalia. Naamini vita itaendelea hadi pale kizazi kilicho jaa ubinafsi na kupenda mali kita kufa na kupote. Somalia needs new breed of youth who are less selfish and more progressive.
Wakoloni kuipa kabila dogo utawala hauchangii kupunguza ukabila, Rwandan waliwachia kabila dogo kutawala, Zanzibar na wao hivyo hivyo, South Africa na wao waliwapa wazungu wachache. Sisemi kama huko hakuna ukabila, lakini kama ukipata kiongozi anayeweza kuunganisha makabila bila kujali maslahi yake binafsi au ya kabila lake, ukabila utapungua kwa asilimia kubwa sana katika nchi hiyo. Nyerele came from very small tribe, lakini alijitahidi kumpa kila mmoja nafasi japo kuna wengine waliona wanatakiwa kupewa zaidi. Mwisho wa siku alifanikiwa na kuacha Tanzania ikiwa na sura ya umoja. FYI wachanga sio kabila kubwa Tanzania, ni kabila dogo sana, usidanganyike kwa kuwaona wao kila upande wa nchi, huwezi kuwalinganisha na Wasukuma au Wanyakusa.