Wakenya tushukuru kwa demokrasia yettu, kama hizi habari nasoma za Tanzania ni kweli

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Juzi Afrika Kusini rais Uhuru ametunukiwa tuzo la Mandela la mwanademokrasia bora Afrika, hiyo ni baada ya yeye kukubali uamuzi wa mahakama wa kubatili ushindi wake wa awali. Japo aliishia kutema cheche dhidi ya mahakama, lakini hilo tukio la yeye kukubali kurudia uchaguzi, lilipongezwa na wengi.

Sasa nasoma taarifa kwamba makanisa ya Bongo yaweza kufungwa iwapo yatajadili siasa za nchi. Hii ni baada ya mhubiri Kakobe kukosoa uongozi wa sasa. Mambo mengine kama haya yawe fundisho kwetu kwamba tulitoka mbali sana, leo hii hapa Kenya tuna hata wahubiri waliochukua milengo ya kisiasa kabisa, unakuta mhubiri ni wa mlengo wa upinzani kwa kwenda mbele na hakomi kuikosoa serikali kila uchao lakini anapeta tu.

Viongozi wetu wa siasa kila wakialikwa makanisani wanapiga siasa hadi mahubiri yanakosa nafasi, na hii ni desturi ya kila Jumapili.

Lakini siwezi nikasema sana maana sijui serikali ya Tanzania ilifiakiaje maamuzi hayo, maana pia ustawi wa nchi ni jambo la msingi, kukosoa hakufai upite mpaka, unafaa ukosoe ukiwa na nia ya kujenga na sio kubomoa. Kuna watu wakianza kuropoka kwenye vipaza sauti watasema hadi utadhani wamelewa
-----------------------------------------------------------------------

- Tanzanaian churches face being deregistered if their leaders voice their opinions on the country's - This came after a renown bishop accused President Magufuli of turning the country into a one-party state and becoming authoritarian - Magufuli denied this but several newspapers and citizens were previously jailed for insulting or speaking out against the leader Tanzania President John Pombe Magufuli made international news when he threatened to close down churches criticizing him. The threat was made after a Pentecostal cleric, Zachary Kakobe, used a Christmas sermon to bemoan how Tanzania was turning into a one-party state by banning political activity.

According to a report by the BBC on Friday, December 29, the Home Affairs Ministry later issued the threat, warning religious institutions against getting involved in political affairs. Read more: Magufuli threatens to close Tanzanian churches days after wining global award
 
unajua madhara ya siasa kwenye dini?
unajua madhara ya dini kwenye siasa?
Watch out what is happening in Central Africa Republic,Myamar Nigeria Israel Palestine and else where
Acga dini iwe dini na siasa iwe siasa vinginevyo harufu chafu itaanza kusikika soon na hatakuepo wa kuicontrol
 
Siasa kuingia makanisani ni very dangerous,nyie wakenya siasa zenye ukabila ndio zinawasumbua kila kukicha,Tanzania hatutaki siasa zenye udini zipate nafasi hatuna ukabila ss so hatuna siasa zenye ukabila ,wala udini.Lazima tu separate hivyo vitu na siasa
 
Kwa upande wangu sikubaliani kabisa na kauli za naibu waziri wa mambo ya ndani kuhusiana na hili jambo, ninahisi hata serikali yenyewe pia haikbaliani na kauli yake, kwasababu Humprey Polepole kama msemaji wa chama tawala amesema ni ruhusa kwa viongozi wa dini kutoa maoni yao kama wananchi wa kawaida kuikosoa serikali popote pale, siamini kama angeweza kuzungumza hivyo bila Baraka za chama na serikali.

Wale wanaosema kwamba yanayofanywa hapa Tanzania na viongozi wa dini kuikosoa serikali, hiyo haina maana na kusema wanachanganya dini na siasa, sio kweli na wala huko sio kuchanganya dini na siasa, kuchanganya dini na siasa ni pale viongozi wa siasa wanapowashawishi waumini wao kushabikia, kujiunga na kitetea chama fulani kwasababu tu chama hicho viongozi wao, au waumini wao wengi wanatokana na dini yao, kama vile Kenya walivyochanganya ukabila na siasa, Jubilee=Kikuyu+Kalenjins+Kisii; NASA=Jaluo+Luhya+Kamba+cost tribes.

Mleta mada ameileta mada nzuri sana, ila ameiweka kiushabiki kidogo, anataka kutuambia kwamba serikali ya Kenya inaruhusu kukosolewa na viongozi wa dini, sio kweli jambo hili, tofauti ya Kenya na Tanzania ni kwamba, Tanzania wanatishia kwa maneno lakini hawatekelezi, Kenya ukiipinga serikali hawakusemi ila wanakumaliza kwa kukuua bila hata kukupa warning.
Kenyan Catholic priest who publicly denounced the killing of opposition demonstrators by Kenyatta's government found dead
 
December 25, 2017
Dar -es-Salaam, Tanzania

Askofu Zachary Kakobe amshauri Rais John Pombe Magufuli atubu. Askofu huyo alitoa ushauri huo jijini Dar-es-Salaam wakati wa kuadhimisha sikukuu ya Christmas 25.12.2017.

Imekuwa kawaida ya viongozi wa kisiasa Tanzania wakienda ktk nyumba za ibada kuwataka viongozi wa kidini kuwaombea wao binafsi "kwa vita wanayoiongoza kupigania rasilimali za nchi zisiibiwe " na umoja/amani ya Taifa.

Hivyo Askofu akaona ni fursa muafaka pia kuwakumbusha kutubu mapungufu yao ili wabadili mienendo yao. Mfano suala la viongozi kutofuata katiba ya nchi na kubinya uhuru wa demokrasia / vyama vingi vya siasa kufanya kazi ni mojawapo ya kero ktk taifa la Tanzania.

Magufuli, peace and equality prize. Uhuru, democracy prize. Hehe dikteta alinyimwa. U.Kenyatta, baba wa demokrasia this side of the Sahara!
Award ilikuwa ni "Mandela peace award", mwaka jana ilinyakuliwa na mfalme wa Morocco, mwaka huu ni Magufuli, ndiyo sababu gazeti lenu limeandika Magufuli beats Uhuru, hizo awards zingine ni kwa ajili ya kusindikiza mshindi wa jumla, haiwezikani na haijatokea mshindi wa jumla pia akaepewa zawadi hizo ndogo ndogo, soma vizuri hilo gazeti lenu utaelewa.
 
Gazeti letu eeh? Tuko news! Hehe afadhali ungeeka article kutoka kwa porn site. Nilidhani we akili kubwa. Site za umbea huku Kenya huwa zinasomwa na washamba tu. Back to the topic at hand, atatubu au la?
 
unajua madhara ya siasa kwenye dini?
unajua madhara ya dini kwenye siasa?
Watch out what is happening in Central Africa Republic,Myamar Nigeria Israel Palestine and else where
Acga dini iwe dini na siasa iwe siasa vinginevyo harufu chafu itaanza kusikika soon na hatakuepo wa kuicontrol
Acha unafiki wewe!
Umekaririshwa hivyo?
Mbona Maaskofu wanaposema Mheshimiwa kuwa chaguo la Mungui huji hapa na kusema "Unajua madhara ya kusema Siasa Kanisani?"

Kwako wewe siasa huja pale viongozi wa dini wakisema Negatively tu?

Wakisema Positive mko kimya!!!
Acheni Unafiki!
 
Gazeti letu. Tuko news! Hehe afadhali ungeeka article kutoka kwa porn site. Back to the topic at hand, anatubu ama hatubu?
Kama hata watu wenu huwaamini, vipi wewe tukuamini?, tafuta sources zingine unazoziamini utakuta ni sawa na hicho kilichoandikwa na tuko news
 
Sasa mimi ndo nitafute source ya habari ambazo hata hazihusiani na mada hii? Data umenisambazia za hela ngapi? Kweli mbege noma.
 
Juzi Afrika Kusini rais Uhuru ametunukiwa tuzo la Mandela la mwanademokrasia bora Afrika, hiyo ni baada ya yeye kukubali uamuzi wa mahakama wa kubatili ushindi wake wa awali. Japo aliishia kutema cheche dhidi ya mahakama, lakini hilo tukio la yeye kukubali kurudia uchaguzi, lilipongezwa na wengi.

Sasa nasoma taarifa kwamba makanisa ya Bongo yaweza kufungwa iwapo yatajadili siasa za nchi. Hii ni baada ya mhubiri Kakobe kukosoa uongozi wa sasa. Mambo mengine kama haya yawe fundisho kwetu kwamba tulitoka mbali sana, leo hii hapa Kenya tuna hata wahubiri waliochukua milengo ya kisiasa kabisa, unakuta mhubiri ni wa mlengo wa upinzani kwa kwenda mbele na hakomi kuikosoa serikali kila uchao lakini anapeta tu.

Viongozi wetu wa siasa kila wakialikwa makanisani wanapiga siasa hadi mahubiri yanakosa nafasi, na hii ni desturi ya kila Jumapili.

Lakini siwezi nikasema sana maana sijui serikali ya Tanzania ilifiakiaje maamuzi hayo, maana pia ustawi wa nchi ni jambo la msingi, kukosoa hakufai upite mpaka, unafaa ukosoe ukiwa na nia ya kujenga na sio kubomoa. Kuna watu wakianza kuropoka kwenye vipaza sauti watasema hadi utadhani wamelewa
-----------------------------------------------------------------------

- Tanzanaian churches face being deregistered if their leaders voice their opinions on the country's - This came after a renown bishop accused President Magufuli of turning the country into a one-party state and becoming authoritarian - Magufuli denied this but several newspapers and citizens were previously jailed for insulting or speaking out against the leader Tanzania President John Pombe Magufuli made international news when he threatened to close down churches criticizing him. The threat was made after a Pentecostal cleric, Zachary Kakobe, used a Christmas sermon to bemoan how Tanzania was turning into a one-party state by banning political activity.

According to a report by the BBC on Friday, December 29, the Home Affairs Ministry later issued the threat, warning religious institutions against getting involved in political affairs. Read more: Magufuli threatens to close Tanzanian churches days after wining global award

MK254 huwa napenda uelewa wako. Nadhani si viile kama anavyodaiwa kusema msemaji wa Serikali. Magazeti yamelikuza jambo kupita jinsi lilivyosemwa. Katiba ya nchi inawapa Watanzania uhuru wa kuabudu wa kutosha kabisa. Raisi wetu amesali kwa Wakatoliki, amesali kwa Makanisa mengine pia. Aidha amehudhuria matukio katika Msikiti wa Waislamu. Wakosoaji wetu wameidaka hiyo na kuipeperusha wanavyotaka. Nimependa ulinganishi wako hata hivyo.
 
This award is an insult to what Mandela stood for. Giving it murderous regimes is to say the least stupid and insensitive to victims. Which peace when you kill your own using the police like chicken!!!!
 
Acha unafiki wewe!
Umekaririshwa hivyo?
Mbona Maaskofu wanaposema Mheshimiwa kuwa chaguo la Mungui huji hapa na kusema "Unajua madhara ya kusema Siasa Kanisani?"

Kwako wewe siasa huja pale viongozi wa dini wakisema Negatively tu?

Wakisema Positive mko kimya!!!
Acheni Unafiki!
Done
 
Sasa mimi ndo nitafute source ya habari ambazo hata hazihusiani na mada hii? Data umenisambazia za hela ngapi? Kweli mbege noma.
Kama haingiliani na mada hii, vipi umejibu kuhusu hizo awards za Uhuru na Magufuli?, au maisha ya Kibera yamekuchanganya?
 
This award is an insult to what Mandela stood for. Giving it murderous regimes is to say the least stupid and insensitive to victims. Which peace when you kill your own using the police like chicken!!!!
I can see some points in you
 
Kama haingiliani na mada hii, vipi umejibu kuhusu hizo awards za Uhuru na Magufuli?, au maisha ya Kibera yamekuchanganya?
Kibera? Nipo mbali sana na Nairobi lakini nahisi hata Kibera yenyewe imeizidi tz saaana kwa demokrasia. Teh teh.😀
 
Back
Top Bottom