Wakenya tushukuru kwa demokrasia yettu, kama hizi habari nasoma za Tanzania ni kweli

Wakenya tushukuru kwa demokrasia yettu, kama hizi habari nasoma za Tanzania ni kweli

Kibera? Nipo mbali sana na Nairobi lakini nahisi hata Kibera imeipiku tz kwa demokrasia. Teh teh.😀
Na mimi ninahisi hivyo hivyo, ila haijaipuku kwa njaa, mauaji ya wananchi yanayofanywa na polisi, unemployment, poverty and tribalism, wasalimie huko Kibera.
 
Acha unafiki wewe!
Umekaririshwa hivyo?
Mbona Maaskofu wanaposema Mheshimiwa kuwa chaguo la Mungui huji hapa na kusema "Unajua madhara ya kusema Siasa Kanisani?"

Kwako wewe siasa huja pale viongozi wa dini wakisema Negatively tu?

Wakisema Positive mko kimya!!!
Acheni Unafiki!
daah hapa ndio naamini shule ni muhimu
hata hiki nilichoandika nacho kinahtaji ufafanuzi?
 
unajua madhara ya siasa kwenye dini?
unajua madhara ya dini kwenye siasa?
Watch out what is happening in Central Africa Republic,Myamar Nigeria Israel Palestine and else where
Acga dini iwe dini na siasa iwe siasa vinginevyo harufu chafu itaanza kusikika soon na hatakuepo wa kuicontrol
acha porojo. Bennauawe, azory auawe, lisu apigwe risasi eti wahubiri wasekemee hali hiyo, acha porojo
 
Na mimi ninahisi hivyo hivyo, ila haijaipuku kwa njaa, mauaji ya wananchi yanayofanywa na polisi, unemployment, poverty and tribalism, wasalimie huko Kibera.
Lissu pia yupo mitaa ya Kibera? Sidhani ni wakenya ndo walimgeuza kichungi kwa mtutu wa bunduki. Kuna tetesi flani nilisikia, kwamba jua likitua Kibera huwa ni ya watz. Yaani washika doria kwa rungu wote ni watz, kina Lepatit na Lemalon ndugu zenu kutoka Oldonyo Lenkai, afu wanalipwa kwa hela za usalama wanazotozwa wakazi wote wa Kibera. Nikifika Nai ntachunguza madai hayo kisha ntarudi na mrejesho.
 
acha porojo. Bennauawe, azory auawe, lisu apigwe risasi eti wahubiri wasekemee hali hiyo, acha porojo
kla ktu kna protocali zake beni akiuwawa mahakama zipo kashtak
lisu akipigwa bomba kama umamjua alyempiga akatoe ushahid mahakamani sio kuropoka kwenye madhabahu kule kunatakiwa mazungumzo ya kimungu sio politics ushaambiwa huo ni mchezo mchafu
 
Tunajua kinachoendelea lazima tukemee maana mahakama amezinyamazisha, kila kitu amekiua, lazima kusema kuwa azory yuko wapi...
 
Tunajua kinachoendelea lazima tukemee maana mahakama amezinyamazisha, kila kitu amekiua, lazima kusema kuwa azory yuko wapi...
sasa bro kama unajua alipo azory c utuambie? then kama unamjua exactly aliyemuua tuwekee hapa tumjue ili rupate pa kuanzia hatutak habar za redio za mbao
Mana nashangaa mara serikali who is serikali? na kama ndivyo huyo bwna serikali alimuua lini na wapi na uliona? na kama huwezkujibu haya tutaendeleaje kukuamini?
 
Siasa kuingia makanisani ni very dangerous,nyie wakenya siasa zenye ukabila ndio zinawasumbua kila kukicha,Tanzania hatutaki siasa zenye udini zipate nafasi hatuna ukabila ss so hatuna siasa zenye ukabila ,wala udini.Lazima tu separate hivyo vitu na siasa
Ukiambiwa ukatubu hiyo imekuwa siasa,
Ukiambiwa Pombe ni chaguo la mungu hiyo siyo siasa.
 
Lissu pia yupo mitaa ya Kibera? Sidhani ni wakenya ndo walimgeuza kichungi kwa mtutu wa bunduki. Kuna tetesi flani nilisikia, kwamba jua likitua Kibera huwa ni ya watz. Yaani washika doria kwa rungu wote ni watz, kina Lepatit na Lemalon ndugu zenu kutoka Oldonyo Lenkai, afu wanalipwa kwa hela za usalama wanazotozwa wakazi wote wa Kibera. Nikifika Nai ntachunguza madai hayo kisha ntarudi na mrejesho.
Ninadhani zitabaki kuwa tetesi tu, haiwezekani watanzania kuishi katika hayo mabanda ya kibera, kwasababu hata mabanda wanapoishi nguruwe wangu ni bora kuliko hayo ya Kibera, wanaoweza kuishi maisha hayo ni wakenya tu. Jacob Juma, Cris Msando, Makaburi, huyo pandre aliyeuliwa kwa kutetea mauaji ya wapinzani,, the list is endless......
 
Juzi Afrika Kusini rais Uhuru ametunukiwa tuzo la Mandela la mwanademokrasia bora Afrika, hiyo ni baada ya yeye kukubali uamuzi wa mahakama wa kubatili ushindi wake wa awali. Japo aliishia kutema cheche dhidi ya mahakama, lakini hilo tukio la yeye kukubali kurudia uchaguzi, lilipongezwa na wengi.

Sasa nasoma taarifa kwamba makanisa ya Bongo yaweza kufungwa iwapo yatajadili siasa za nchi. Hii ni baada ya mhubiri Kakobe kukosoa uongozi wa sasa. Mambo mengine kama haya yawe fundisho kwetu kwamba tulitoka mbali sana, leo hii hapa Kenya tuna hata wahubiri waliochukua milengo ya kisiasa kabisa, unakuta mhubiri ni wa mlengo wa upinzani kwa kwenda mbele na hakomi kuikosoa serikali kila uchao lakini anapeta tu.

Viongozi wetu wa siasa kila wakialikwa makanisani wanapiga siasa hadi mahubiri yanakosa nafasi, na hii ni desturi ya kila Jumapili.

Lakini siwezi nikasema sana maana sijui serikali ya Tanzania ilifiakiaje maamuzi hayo, maana pia ustawi wa nchi ni jambo la msingi, kukosoa hakufai upite mpaka, unafaa ukosoe ukiwa na nia ya kujenga na sio kubomoa. Kuna watu wakianza kuropoka kwenye vipaza sauti watasema hadi utadhani wamelewa
-----------------------------------------------------------------------

- Tanzanaian churches face being deregistered if their leaders voice their opinions on the country's - This came after a renown bishop accused President Magufuli of turning the country into a one-party state and becoming authoritarian - Magufuli denied this but several newspapers and citizens were previously jailed for insulting or speaking out against the leader Tanzania President John Pombe Magufuli made international news when he threatened to close down churches criticizing him. The threat was made after a Pentecostal cleric, Zachary Kakobe, used a Christmas sermon to bemoan how Tanzania was turning into a one-party state by banning political activity.

According to a report by the BBC on Friday, December 29, the Home Affairs Ministry later issued the threat, warning religious institutions against getting involved in political affairs. Read more: Magufuli threatens to close Tanzanian churches days after wining global award
Lol! Hii rivalry ya Kenya na tz ni nzuri sana maana inawapotezea wanahabari umakini wa kuandika habari, badala yake wanajikita kwenye kutetea nchi zao!

Hilo tishio halikutamkwa na magufuli, ila ni naibu waziri wa home affairs. Ndo maana vyombo vinavyojua maadili ya kazi zao kama bbc, ambao hata huyo mwandishi amewanukuu waliandika kuwa "Tanzania yatishia kufungia makanisa " Tanzania threatens to shut churches

Sasa wakenya kwa kuwa magufuli anawanyoosha na amekuwa tishio kwenu, chochote kinachotokea tz basi wao wanamjua magufuli tu, hata aseme mkuu wa mkoa! Waandishi wa habari wa hovyo kabisa tunawashuhudia kutoka Kenya.

Pamoja na maoni yangu hapo juu, binafsi sikubaliani na kauli ya huyo naibu waziri. Wawaache watu wajadili siasa watakavyo kama hawavunji sheria za nchi. Wasitake kusifiwa tu kila mda, kama ni hivyo, hata wanaowasifia huko kanisani nao wawazuie. Ukweli kwenye hili serikali ya magufuli inapwaya. Warekebishe hii tabia inakera.

Mwisho ndugu yangu MK254 ni kuhusu hii tuzo ya Nelson Mandela. Najua na wewe unafaham kuwa tuzo ya jumla ni ile ya AMANI ambayo magufuli aliibuka kidedea. Hii aliyochukua uhuru ya demokrasia iko kwenye kundi ya tuzo ndogo ndogo, haina tofauti na aliyoshinda Nkurunzinza, rais wa Chad, Mahakama kuu ya Kenya, Mkuu wa majeshi wa zimbabwe ambaye amekuwa makamu wa rais, Mwandishi wa habri ambaye pia ni mwanaharakati kutoka misri na wengine! Kwa hiyo kidedea hapa kwenye hizi tuzo za mandela ni Magufuli.

Hata hivyo, hilo tamko la NW halikuwa zuri kipindi hiki ambacho rais amemaliza kupata tuzo.
 
Habari hizo zimeletwa na gazeti la kishilawadu la Kenya na ndio maana ukitazama kwenye kichwa cha uzi nimeandika "Kama ni kweli", maana hili gazeti huwa la kiudaku udaku hivyo lazima nithibitishe kwengine. Hadi sasa sijaona mainstream media yoyote ya Kenya ambayo imeandika kuhusu hilo tukio.

Kuhusu Magufuli kutunyoosha, huo ni wimbo mnaouimba kila siku lakini kiukweli hadi leo sijaona chochote amekifanya ambacho ni tishio kwetu, kuchoma vifaranga na kunadi ng'ombe hiyo ni issue ndogo sana, japo tuliipigia makelele lakini kiukweli ukiangalia kwa jicho la tatu ni issue ya kupuuza.

Rais ambaye kwa kweli alikua ameanza kutupelekesha kidogo ni Kikwete, maana kwenye muhula wa pili alikua tayari ameanza kujiamini na akaanza kuiweka Tanzania kwenye ramani kwa uwezo wake wa kujieleza nje kwa wawekezaji, nchi yenu ilikua imeanza kwenda kwa asilimia zaidi ya saba kiuchumi, mambo mengi mnayoyafanya leo au yanayo onekana leo alikua ameyapa msingi. Ukiangalia hayo madaraja, mabasi na mengineyo ambayo mnazindua, alivifanya Kikwete.

Magufuli nampa heko kwa mikwara dhidi ya mafisadi na kushtukiza Watanzania kwenye maofisi, lakini kwa mtu aliye nje ya Tanzania kama mimi sioni kngine zaidi ya hapo. Hadi labda kwenye muhula wa pili ndio vitu vitajitokeza, vitu alivyovianzisha na kuonekana, maana hata reli ya kati hiyo bado ni stori kwa mtu asiye Mtanzania na ako nje ya nchi. Nakumbuka Kikwete alikua amepata hela ya safu yote kutoka kwa Mchina ambaye mlimpiga chini kwa mihemko, sasa naskia mumeanza kumtongoza Mchina arudi,

Humu tuliambiwa Tanzania itaipita Kenya kiuchumi ndani ya siku mia moja za Magufuli, tumesubiri ila tunaona asilimia ya ukuaji ndio inashuka kutoka kwa ile saba ya Kikwete. Japo PR propagandist wa CCM aka Lumumba boys ambao hukesha humu, hujaribu sana kuweka twists, awali nilikua nakushuku wewe kuwa mmoja wao, lakini kuna uzi fulani niliona ukibishana na mmoja wao, tena hoja zako zilikua na mantiki sana ndio nikakuona kama mzalendo wa kweli. Sikumbuki uzi, ila ulikua unakosoa mbinu za Magufuli kuanika mawaziri wake nje badala ya kuwaadhibu ndani. Hapo ndio nilijua haupo humu kutetea kila kitu lakini kujadili mada kwa kutumia akili zako mwenyewe na sio kikazi.

Hilo la rais wetu kushinda tuzo la demokrasia, walitoa mfano kwa kusema Uhuru ameshnda kwa ajili ya kukubali kurudia uchaguzi, maana sidhani kama akina Museveni, Kagame, Zuma n.k. wanaweza kukubali kitu kama hicho, washinde uchaguzi na kutangazwa na tume halafu ubatilishwe.
Hebu naomba nielimishe, Magufuli ameshnda tuzo la amani, ni kipi amekifanya ambacho kimehusshwa na amani, ni kwa ajili ya ndani ya nchi? Au Afrika au wapi. Nitakua nyuma nimeachwa na hizo habari.

La mhubiri kumkosoa rais, nimemskliza Kakobe, kwa kweli ametema cheche lakini hayo hayakutosha kutishia ufungwaji wa makanisa yake.
 
Acha unafiki wewe!
Umekaririshwa hivyo?
Mbona Maaskofu wanaposema Mheshimiwa kuwa chaguo la Mungui huji hapa na kusema "Unajua madhara ya kusema Siasa Kanisani?"

Kwako wewe siasa huja pale viongozi wa dini wakisema Negatively tu?

Wakisema Positive mko kimya!!!
Acheni Unafiki!
after all kwani siasa ni shetani kwamba ina ugomvi na kanisa,we have been brainwashed hivyo kuwa siasa na dini ni west and east kitu ambacho sio kweli
 
Kikwete utawala wake ulifanana sana na Uhuru Kenyatta, safari nyingi za nje, kushindwa kudhibiti rushwa, kushindwa kusimamia uwajibikaji kwa viongozi wa umma na serikali, kuongezeka kwa matumizi ya hovyo ya serikali, kushindwa kuziba mianya ya upotevu wa fedha za serikali kiasi cha serikali kukosa pesa za kuendeshea nchi, na kushindwa kusimamia vizuri mali asili za Taifa.

Magufuli amefanikiwa katika yote hayo. Ni ukweli usiopingika kwamba Magufuli anawanyorosha wengi sio Kenya peke yake, ila Kenya imehadhirika zaidi kwasababu ya kudhibiti biashara kati ya Kenya na Tanzania, wakenya wengi kuanzia viongozi hadi watu wa kawaida kama vile wafugaji wanalalamikia Magufuli kwa kudhibiti movements za watu na bidhaa kati ya Kenya na Tanzania, mwanzo ilikuwa ni rahisi sana kwa wakenya kuja kufanya kazi bila hata kulipia work permit, lakini baada ya Magufuli kuingia, wakenya wengi waliokuwa wanafundisha Tanzania walirudishwa na Kenya ilipiga kelele za kusema Magufuli hampendi Uhuru kutokana na urafiki wake na Raila, wafugaji hawaruhusiwi tena kuvuka mpaka kiholela, kupiga marufuku kusafirisha chakula vyote hivi viliiathiri zaidi Kenya, ni mtu mwenye akili ndogo tu atakayesema kwamba Magufuli hajaisumbua Kenya.

Dunia nzima, wakiwemo watanzania wengi sana wanamkubali sana Magufuli, mfano mzuri ni hii Mandela peace award aliyoipata katika mwaka wa pili tu wa uongozi wake, wakati kuna marais wanekaa muda mrefu lakini amewashinda, japo hata mimi kwa maoni yangu sidhani kama alistahili kuipata kwa sasa hibi, lakini hii ni ishara tosha kwamba anakubalika duniani, Wakenya hasa wale ambao wapo mrengo wa Jubilee kamwe hawawezi kumkubali Magufuli kwa sababu amemfunika sana Uhuru Kenyatta, kila kitu anachofanya Uhuru Kenyatta anaonekana hafanyi kitu, ndiyo sababu kwa unafiki wanajidai eti Kikwete ndiyo alikuwa ni tishio kwao, huo ni unafiki unaochagizwa na ukabila, ukabila utaitafuna Kenya.
 
sasa bro kama unajua alipo azory c utuambie? then kama unamjua exactly aliyemuua tuwekee hapa tumjue ili rupate pa kuanzia hatutak habar za redio za mbao
Mana nashangaa mara serikali who is serikali? na kama ndivyo huyo bwna serikali alimuua lini na wapi na uliona? na kama huwezkujibu haya tutaendeleaje kukuamini?
Kuandika kwenyewe hujui
 
Back
Top Bottom