Habari hizo zimeletwa na gazeti la kishilawadu la Kenya na ndio maana ukitazama kwenye kichwa cha uzi nimeandika "Kama ni kweli", maana hili gazeti huwa la kiudaku udaku hivyo lazima nithibitishe kwengine. Hadi sasa sijaona mainstream media yoyote ya Kenya ambayo imeandika kuhusu hilo tukio.
Kuhusu Magufuli kutunyoosha, huo ni wimbo mnaouimba kila siku lakini kiukweli hadi leo sijaona chochote amekifanya ambacho ni tishio kwetu, kuchoma vifaranga na kunadi ng'ombe hiyo ni issue ndogo sana, japo tuliipigia makelele lakini kiukweli ukiangalia kwa jicho la tatu ni issue ya kupuuza.
Rais ambaye kwa kweli alikua ameanza kutupelekesha kidogo ni Kikwete, maana kwenye muhula wa pili alikua tayari ameanza kujiamini na akaanza kuiweka Tanzania kwenye ramani kwa uwezo wake wa kujieleza nje kwa wawekezaji, nchi yenu ilikua imeanza kwenda kwa asilimia zaidi ya saba kiuchumi, mambo mengi mnayoyafanya leo au yanayo onekana leo alikua ameyapa msingi. Ukiangalia hayo madaraja, mabasi na mengineyo ambayo mnazindua, alivifanya Kikwete.
Magufuli nampa heko kwa mikwara dhidi ya mafisadi na kushtukiza Watanzania kwenye maofisi, lakini kwa mtu aliye nje ya Tanzania kama mimi sioni kngine zaidi ya hapo. Hadi labda kwenye muhula wa pili ndio vitu vitajitokeza, vitu alivyovianzisha na kuonekana, maana hata reli ya kati hiyo bado ni stori kwa mtu asiye Mtanzania na ako nje ya nchi. Nakumbuka Kikwete alikua amepata hela ya safu yote kutoka kwa Mchina ambaye mlimpiga chini kwa mihemko, sasa naskia mumeanza kumtongoza Mchina arudi,
Humu tuliambiwa Tanzania itaipita Kenya kiuchumi ndani ya siku mia moja za Magufuli, tumesubiri ila tunaona asilimia ya ukuaji ndio inashuka kutoka kwa ile saba ya Kikwete. Japo PR propagandist wa CCM aka Lumumba boys ambao hukesha humu, hujaribu sana kuweka twists, awali nilikua nakushuku wewe kuwa mmoja wao, lakini kuna uzi fulani niliona ukibishana na mmoja wao, tena hoja zako zilikua na mantiki sana ndio nikakuona kama mzalendo wa kweli. Sikumbuki uzi, ila ulikua unakosoa mbinu za Magufuli kuanika mawaziri wake nje badala ya kuwaadhibu ndani. Hapo ndio nilijua haupo humu kutetea kila kitu lakini kujadili mada kwa kutumia akili zako mwenyewe na sio kikazi.
Hilo la rais wetu kushinda tuzo la demokrasia, walitoa mfano kwa kusema Uhuru ameshnda kwa ajili ya kukubali kurudia uchaguzi, maana sidhani kama akina Museveni, Kagame, Zuma n.k. wanaweza kukubali kitu kama hicho, washinde uchaguzi na kutangazwa na tume halafu ubatilishwe.
Hebu naomba nielimishe, Magufuli ameshnda tuzo la amani, ni kipi amekifanya ambacho kimehusshwa na amani, ni kwa ajili ya ndani ya nchi? Au Afrika au wapi. Nitakua nyuma nimeachwa na hizo habari.
La mhubiri kumkosoa rais, nimemskliza Kakobe, kwa kweli ametema cheche lakini hayo hayakutosha kutishia ufungwaji wa makanisa yake.