Wakenya tushukuru kwa demokrasia yettu, kama hizi habari nasoma za Tanzania ni kweli

Acha zako we kibwengo, hao mashekhe walisaidiwa sana. Walipunguziwa domo wakaharakishiwa shughuli yao ya kupatana na bikra zao 72. Hamna dhambi hapo. Hapo ni katika harakati ya kuwasaidia tu. Kenya hamna Guantanamo Bay, kuna hospitali tu, za kuziba tundu za risasi kwenye miili ya watu mashuhuri kama Lissu.

Waliomuua Musando wamekamatwa?

Mnaua watu wenu halafu mnajisifu kuziba tundu za risasi za majirani zenu.

Huo si ukichaa.
 
Jpm kawashika vibaya, mfano ni zuiio LA tanzanity lilikua linaingizia Kenya billion of money , kwann wasinune, bomba LA mafuta ambalo litakua linaingizia tz 1$billion per year, sasa utalinganisha kikwete na maguful,
 
  • Thanks
Reactions: Oii
Award ilikuwa ni "Mandela peace award", mwaka jana ilinyakuliwa na mfalme wa Morocco, mwaka huu ni Magufuli, ndiyo sababu gazeti lenu limeandika Magufuli beats Uhuru, hizo awards zingine ni kwa ajili ya kusindikiza mshindi wa jumla, haiwezikani na haijatokea mshindi wa jumla pia akaepewa zawadi hizo ndogo ndogo, soma vizuri hilo gazeti lenu utaelewa.

Hakuna kitu kama hicho, acha kukariri.

Tiba
 
Hakuna kitu kama hicho, acha kukariri.

Tiba
Huu ni uwanja wa kuelimishana na kukosoana, tunaomba ingia uwanjani lete kile unachokijua kwamba ni sahihi kwa kuambatanisha na ushaidi maridhawa, karibu sana jamvini mrembo.
 
Habari hizo zimeletwa na gazeti la kishilawadu la Kenya na ndio maana ukitazama kwenye kichwa cha uzi nimeandika "Kama ni kweli", maana hili gazeti huwa la kiudaku udaku hivyo lazima nithibitishe kwengine. Hadi sasa sijaona mainstream media yoyote ya Kenya ambayo imeandika kuhusu hilo tukio.

Kuhusu Magufuli kutunyoosha, huo ni wimbo mnaouimba kila siku lakini kiukweli hadi leo sijaona chochote amekifanya ambacho ni tishio kwetu, kuchoma vifaranga na kunadi ng'ombe hiyo ni issue ndogo sana, japo tuliipigia makelele lakini kiukweli ukiangalia kwa jicho la tatu ni issue ya kupuuza.

Rais ambaye kwa kweli alikua ameanza kutupelekesha kidogo ni Kikwete, maana kwenye muhula wa pili alikua tayari ameanza kujiamini na akaanza kuiweka Tanzania kwenye ramani kwa uwezo wake wa kujieleza nje kwa wawekezaji, nchi yenu ilikua imeanza kwenda kwa asilimia zaidi ya saba kiuchumi, mambo mengi mnayoyafanya leo au yanayo onekana leo alikua ameyapa msingi. Ukiangalia hayo madaraja, mabasi na mengineyo ambayo mnazindua, alivifanya Kikwete.

Magufuli nampa heko kwa mikwara dhidi ya mafisadi na kushtukiza Watanzania kwenye maofisi, lakini kwa mtu aliye nje ya Tanzania kama mimi sioni kngine zaidi ya hapo. Hadi labda kwenye muhula wa pili ndio vitu vitajitokeza, vitu alivyovianzisha na kuonekana, maana hata reli ya kati hiyo bado ni stori kwa mtu asiye Mtanzania na ako nje ya nchi. Nakumbuka Kikwete alikua amepata hela ya safu yote kutoka kwa Mchina ambaye mlimpiga chini kwa mihemko, sasa naskia mumeanza kumtongoza Mchina arudi,

Humu tuliambiwa Tanzania itaipita Kenya kiuchumi ndani ya siku mia moja za Magufuli, tumesubiri ila tunaona asilimia ya ukuaji ndio inashuka kutoka kwa ile saba ya Kikwete. Japo PR propagandist wa CCM aka Lumumba boys ambao hukesha humu, hujaribu sana kuweka twists, awali nilikua nakushuku wewe kuwa mmoja wao, lakini kuna uzi fulani niliona ukibishana na mmoja wao, tena hoja zako zilikua na mantiki sana ndio nikakuona kama mzalendo wa kweli. Sikumbuki uzi, ila ulikua unakosoa mbinu za Magufuli kuanika mawaziri wake nje badala ya kuwaadhibu ndani. Hapo ndio nilijua haupo humu kutetea kila kitu lakini kujadili mada kwa kutumia akili zako mwenyewe na sio kikazi.

Hilo la rais wetu kushinda tuzo la demokrasia, walitoa mfano kwa kusema Uhuru ameshnda kwa ajili ya kukubali kurudia uchaguzi, maana sidhani kama akina Museveni, Kagame, Zuma n.k. wanaweza kukubali kitu kama hicho, washinde uchaguzi na kutangazwa na tume halafu ubatilishwe.
Hebu naomba nielimishe, Magufuli ameshnda tuzo la amani, ni kipi amekifanya ambacho kimehusshwa na amani, ni kwa ajili ya ndani ya nchi? Au Afrika au wapi. Nitakua nyuma nimeachwa na hizo habari.

La mhubiri kumkosoa rais, nimemskliza Kakobe, kwa kweli ametema cheche lakini hayo hayakutosha kutishia ufungwaji wa makanisa yake.
Akhsante kwa kuuona upotoshaji wa hilo gazeti, kila nchi huwa ina magazeti au vyombo vya habari vingine vya hivyo!

Labda niongelee hili la kuwanyoosha kama nilivyolisema hapo awali!

Kwanza ifahamike kuwa nikiongelea kuwanyoosha simaanishi kitendo cha kupiga mnada ile mifugo na kuchoma moto vifaranga, japo naamini njia mbadala za kidiplomasia zingetumika kuhsu ile mifugo wamiliki wakalipa hata vile vifaranga vikarudi vilikotoka. Hili simaanishi kuwa ndio liliwanyoosha. Tena ukikumbuka vizuri wakati hili linafanyika, wakenya tayari walikuwa wanachuki kubwa sana dhidi ya jpm, labda nikukumbushe ilianzia wapi.

Chanzo cha chuki ya wakenya kwa jpm ambacho ndo tunasema aliwanyoosha ni pale tz ilipoanza kuzuia baadhi ya bidhaa kutoka Kenya ili kulinda zile ambazo zinazalishwa hapa nchini. Utakumbuka vizuri kuwa kuanzia mwaka jana baadhi ya bidhaa zinazotoka Kenya kuja hapa nchini zilipungua sana. Hiki ndo kitu kilichoanza kuamsha hasira za wakenya. Katika mashambulizi, kenya mlizuia gas na ngano kutoka tz, na hapo tz ika react tena kwa kufungia bidhaa zaidi ikiwemo maziwa na vingine! Utakumbuka hapa ndo moto uliwaka ikafikia hatua tz ikakataa kuuza tena baadhi ya raw material ikiwemo mahindi na kudai mahindi yakoborewe kwanza ili yauzwe kama unga badala ya kuuzwa hivo hivo. Hapa ndo tulikuwa tunasigana kweli kweli hadi Kenya mkaruhusu gas na ngano, na tz kuruhusu vya kenya kuingia. So nilipokuwa nasema kukomesha ni hii economic Battle, sio zile habari za kitoto za vifaranga!

Kuna kipindi tz hasa kwa jk ambaye umemsifia (ndio, kuna maazuri yake kafanya likiwemo la kukuza uchumi kwenye kiwango ambacho hakijawahi kufikiwa) product za kenya zilikuwa nyingi sana mpaka kero. Tena mimi ni miongoni mwa watu tuliokuwa tunakereka zaidi. Nilikwenda kanda ya ziwa maeneo Musoma miaka kadhaa, nilikuta hadi maji ya kunywa yamejaa ya kutoka Kenya, na mengine kutoka Uganda. Sa hz maeneo yote yaho hakuna bidhaa za kutoka nje zinazoingia kinyemela.

Kuhusu kikwete kuwanyoosha kiuchumi, ni kweli JK amesaidia sana kuinua uchumi wa nchi. Lakini kwa ziara zake hizo za nje ambazo wewe unazisifia ambazo sisi tulizilaumu hadi kufikia kusema hatuna rais, zilichangia sana kuiuza nchi hii! Mikataba ya ovyo imefanyika kipindi chake, madini yote aliuza, mbuga za wanyama ndo usiseme, ndo maana wakati huo utalii ulikuwa chini sana! So nyie mnaweza kuwa mnaona alifanya kazi lakini upande mwingine tulitakiwa kuwa mbali zaidi Kupitia ushawishi wake kwa mataifa ya nje!

La mwisho kuhusu hii tuzo ya amani ya magufuli. Kiukweli siwezi kusimama na kusema kwa nini alishinda ila watoa tuzo wanajua, maana hakuwa peke yake, aliwashinda washindani wake. Lakini sababu ya Uhuru kutolewa sababu za yeye kushinda tuzo ya demokrasia ni kwa sababu kwenye demokrasia ya jumla kama nchi kenya bado iko chini. Ndo maana ilibidi sababu muafaka za yeye kushinda tuzo ya demokrasia kwenye nchi ambayo haina demokrasia ya kutosha lazima ziwekwe bayana! Hivyo wakenya mkae mkijua kuwa hiyo ni tuzo yake binafsi sio ya nchi!

Niwakumbushe kuwa, linapokuja suala la democracy na freedom of speech, kwa takwimu za 2016 tz iko juu ya Kenya! Tusubiri ranking za mwaka huu tuone itakuwaje.
 
Hii ni ya 2017, and Toyota escudo wins the JAMII FORUMS high esteem prize for....longest comment ever! 😀😀😀 Happy new year to all of ya!
 
Hapo bado hujanirizisha kwamba Magufuli aliwanyoosha Wakenya, maana sababu za kuzuia mahindi zilitolewa na nakumbuka hamkua na mahindi ya kutosha, kuna maeneo ya Tanzania yalikua yanapitia njaa kali. Hivyo haikua busara kwa mahindi kuuzwa nje kinyemela wakati watu wa ndani ya nchi wanapitia shida. Na ndio maana tukafuata mahindi hadi Zambia na yakapitia kwenu.

Kabla ya vifaranga na ng'ombe, Magufuli hakua amefanya chochote cha kuibua chuki kutoka kwa Wakenya, mzozano ilikua kwenye level ya serikali kwa serikali. Kwanza alikua anasifiwa sana kwa zile PR zake za shtukiza shtukiza akiandamana na wanahabari, hizo habari zilikua zinawafikia Waafrika wote hadi Nigeria, hivyo wote walikua wanamuona kama masihi dhidi ya utepetevu kazini (haswa kwa wasiojua desturi ya uvivu wa Kibongobongo)

Kwa kweli baada ya hilo la vifaranga na ng'ombe kumeibuka chuki sana ya Wakenya dhidi ya Magufuli na kwa kiasi dhidi ya Watanzania, hilo nimeanza kuliona na sijapendezwa kabisa, hizi chuki sio nzuri haswa kwa mtu kama mimi ambaye nafanya biashara zangu EAC. Kwa mara ya kwanza nimeona Wakenya wa maeneo kama Namanga wanazunguka nyumba kwa nyumba wakiwasaka Watanzania. Juzi Watanzania wamekamatwa Malindi wakivua samaki, halafu kwenye mitandao ya kijamii aisei nilihuzunishwa sana kuona maneno ya Wakenya yaliyojaa chuki dhidi yenu, na wote walikua wanataja yale ya ng'ombe na vifaranga.
Leo hii mtu kujitambulisha kama Mtanzania ndani ya bar hapa Kenya inaibua hisia fulani, sio kama hapo awali ambapo Watanzania walikua wanachukuliwa kama wastaarabu fulani fulani hivi.

Kwa muda mrefu sana Tanzania imekua ikiendekeza mbinu za chuki dhidi ya Wakenya tangu enzi za Nyerere, japo Wakenya walikua wanapuuza na kuendelea na maisha, lakini kwenye utawala wa Magufuli ndio nimeona raia wa Kenya wakianza kujibu hizo chuki kwa mara ya kwanza.

Kama kuna rais wa Tanzania ambaye alichukuliwa kuwachukia na kufanya vituko dhidi ya Wakenya, labda tungerudi kwa huyo JK maana kipindi chake ndio kulikua na operations za kuwasaka walimu wa kutokea Kenya. Mara akazuia ndege za KQ mara hiki mara kile, na kipindi hicho ndio alifaulu kuinua Tanzania kiuchumi ikakua kwa alama zaidi ya saba na kuwapa Watanzania mwamko wa kiaina ikiwemo kisiasa na demokrasia maana kwenye utawala wake ndio aliwaruhusu kumkosoa mtakavyo.

Haya nazungumza kama Mkenya aliye nje ya Tanzania, hivyo maoni yangu yapo kwenye mlengo huo, kama nyie mlichukizwa sa safari zake, basi hapo sijui, lakini sisi tuliona rais wa Tanzania ambaye alikua anatupatia ushindani mkali sana kwenye utalii na wawekezaji kwa kuinadi Tanzania kwa bidii. Nakumbuka pia huyo huyo JK aliwahi kuwafuta mawaziri sita kwa mpigo kwa sababu za ufisadi. Lakini hata hivyo alikua na mapungufu yake ambayo mliyaona nyie. Michezo yake ilikua kimya kimya huku akicheka cheka lakini mambo yanafanyika kiaina. Ipo siku aliwafikisha kwenye ukuaji wa kiuchumi kwa asilimia 7.2%, yaani mtazamo wa kiutalaam sio PR za vijiweni.

Hilo la tuzo sitaki kuling'ang'ania maana sote tunakubaliana kwa issue moja kwamba hatuoni sababu za Magufuli kutunukiwa tuzo la amani, maana sikumbuki wapi amepatanisha kwenye nchi zinazozozana, au Tanzania ndani labda kaongeza amani yenu ikawa zaidi ya ilivyokua au labda nikitumia kigezo ulichotumia cha kwamba Kenya hakuna demokrasia ndio maana Uhuru akashinda tuzo la demokrasia, hivyo basi labda Tanzania haina amani na kupelekea kuwekwa bayana kwa rais Magufuli kushinda tuzo la amani....hehehe kizungumkuti
 
We malaya jiheshimi ,acha kushobokea wanaume malijari wenye uwezo Wa kukutatua malinda
cna muda wa kubishana na wanyoa viduku wa facebook hii ni ya mwsho kwako mbwa jike mkubwa ww
 
Hao Wakenya wanaowachukia wa Tz huko Kenya , waambie wa Tz hatujaribiwi tutawatimua watu wao wote wanaopiga kazi bila work permit hapa nchini.
 
Heri ya mwaka mpya!

Kwanza kuna kitu hapa nakiona pengine ndo kinaleta kuchelewa kutoelewana. Nahisi neno Kenya na Wakenya masikioni mwenu linaweza kuwa lina tofauti kubwa kimantiki japo kwa muktadha ninaoumaanisha mimi tofauti yake ni ndogo. Ninaposema Magufuli kawanyoosha wakenya hakuna tofauti na kusema magufuli kainyoosha Kenya. Wether suala lililopo ni mgogoro wa serikali kwa serikali au ni mgogoro wa wananchi kwa wananchi, mwisho wa siku athali za mzozo wowote zinawaangukia wananchi. Kwa hiyo kwa mantiki hii, neno kenya na wakenya lina tofauti ndogo.

Pamoja na kuwa unakataa lakini zile ban ambazo ziliwekwa na tz kuhusu bidhaa za kenya ziliwaathiri sana maana ni kitu ambacho hakikutegemewa kutokea kwa kipindi hicho, na hii moja kwa moja ilikuwa inagusa maisha ya wakenya maana wao ndo wafanyabiashara na pia kodi inayolipwa inawafaidisha wananchi wote wa Kenya.

Sasa hili la zuio la uingizwaji wa baadhi ya bidhaa halikuonekana kuwachukulia muda wakenya wengi kwa sababu sio wengi wanafanya biashara ya kuleta huku bidhaa, na pia hata faida ambayo serikali inaipata kutokana na bidhaa hizo kuletwa tz wananchi wengi hawaioni moja kwa moja. Ndo maana wengi hawakuwa wakiliongelea hili, lakini serikali yenyewe ambayo ilikuwa inajua inachokipoteza ndio maana walikuwa wanahaha kuhakikisha vikwazo hivyo vinatatuliwa.

Suala la Vifaranga na ng'ombe linawagusa wananchi wa kenya moja kwa moja, ndo maana wengi walipatwa na hasira lakini ukiangalia serikali haikulikomalia saana zaidi ya kuiandikia serikali ya tz barua ya kutoridhiswa na kitendo hicho.

Kuwalinganisha JK na JPM, kwangu hawa wote ni marais wangu. JK amefanya mazuri na mengine ambayo hata kama hatukuyapenda lakini muda wake umepita hatuna cha kufanya. JPM ana mazuri yake lakini pia na mengine ambayo tunaona hayako sawa. kwa sababu bado yuko madarakani ndo maana tunakosoa pale ambapo haturidhishwi ili arekebishe angali madarakani.

Sasa ona, wewe mwenyewe umekiri hadharani kwamba JK alionekana tishio kwenu kwa kuipaisha tz kiuchumi na kufikia level ya 7.2%. Na hili lilionekana tishio kwenu, ndo maana nikasema suala ambalo linagusa uchumi wa nchi ambalo huongelewa na wachache huwa ni tishio kubwa zaidi kwa nchi kuliko suala la kijamii ambalo laweza kuongelewa na wengi lakini likawahi kuisha.

BTW, hizo chuki ulizosema zimeanza kuwa sugu miongoni mwa wakenya sio nzuri hasa ukiangalia eti sababu ni hiyo mifugo ambayo niliskia kuwa wamasai wa upande wa tz waliwapa fidia ya ng'ombe wamasai wenzao wa upande wa kenya. Next time nikija ntakuwa extra cautious nisijenyofolewa maini maana kuna maeneo nilishayazoea kweli kweli.
 
Juzi Afrika Kusini rais Uhuru ametunukiwa tuzo la Mandela la mwanademokrasia bora Afrika, hiyo ni baada ya yeye kukubali uamuzi wa mahakama wa kubatili ushindi wake wa awali. Japo aliishia kutema cheche dhidi ya mahakama, lakini hilo tukio la yeye kukubali kurudia uchaguzi, lilipongezwa na wengi.

Sasa nasoma taarifa kwamba makanisa ya Bongo yaweza kufungwa iwapo yatajadili siasa za nchi. Hii ni baada ya mhubiri Kakobe kukosoa uongozi wa sasa. Mambo mengine kama haya yawe fundisho kwetu kwamba tulitoka mbali sana, leo hii hapa Kenya tuna hata wahubiri waliochukua milengo ya kisiasa kabisa, unakuta mhubiri ni wa mlengo wa upinzani kwa kwenda mbele na hakomi kuikosoa serikali kila uchao lakini anapeta tu.

Viongozi wetu wa siasa kila wakialikwa makanisani wanapiga siasa hadi mahubiri yanakosa nafasi, na hii ni desturi ya kila Jumapili.

Lakini siwezi nikasema sana maana sijui serikali ya Tanzania ilifiakiaje maamuzi hayo, maana pia ustawi wa nchi ni jambo la msingi, kukosoa hakufai upite mpaka, unafaa ukosoe ukiwa na nia ya kujenga na sio kubomoa. Kuna watu wakianza kuropoka kwenye vipaza sauti watasema hadi utadhani wamelewa
-----------------------------------------------------------------------

- Tanzanaian churches face being deregistered if their leaders voice their opinions on the country's - This came after a renown bishop accused President Magufuli of turning the country into a one-party state and becoming authoritarian - Magufuli denied this but several newspapers and citizens were previously jailed for insulting or speaking out against the leader Tanzania President John Pombe Magufuli made international news when he threatened to close down churches criticizing him. The threat was made after a Pentecostal cleric, Zachary Kakobe, used a Christmas sermon to bemoan how Tanzania was turning into a one-party state by banning political activity.

According to a report by the BBC on Friday, December 29, the Home Affairs Ministry later issued the threat, warning religious institutions against getting involved in political affairs. Read more: Magufuli threatens to close Tanzanian churches days after wining global award
Hiyo ni tafsiri ya mwandishi wa habari hiyo kwa lugha ya kiingereza. Uhuru wa kuabudu umekuwepo Tanzania tangu uhuru na utaendelea kuwepo. Kilichotokea katika nchi jirani si lazima kitokee Tanzania. Dhehebu likivunja sheria za nchi litafungiwa. Mhubiri akikiuka maadili na kuvunja sheria atashtakiwa kama ilivyo katika nchi zote. Tanzania hatujafika huko anakotarajia mwandishi huyo. Huo ndio tunaita uandishi chochezi. Warusi wanaita "disinformatsiya." Waingereza wansita disinformation.
 
Back
Top Bottom