- Source #1
- View Source #1
Kumekuwepo na chapisho ambalo linasambazwa kwenye mtandao wa Instagram likidai kuwaonyesha baadhi ya raia wa Kenya wakiwapokea wageni wanaodhaniwa kuwa na ugonjwa wa Ebola.
Katika chapisho hilo imeomekana kuwa na jumbe ufuatao” Marekani itaipatia Kenya USD milioni 13.5 [TZS bilioni 35.5] kwa ajili ya kujenga karantini ya kuwaweka raia wa Marekani wanaoshukiwa kuwa na maambuzi ya virusi vya Ebola.
Marekani imesema kipaumbele chao ni kulinda afya na usalama wa raia wake, kwa kuhakikisha ugonjwa huo hauingii nchini humo.
Je ?ni upi uhalisia wa chapisho hilo linalosambaa kwenye mitandao ya kijamii kwa sasa ?

- Tunachokijua
- Kupitia vyanzo mbalimbali viliripoti kuwa Serikali ya Marekani imepanga kuichangia serikali ya Kenya kiasi cha dola za kimarekani Milioni 13.43 kwa ajili ya kujenga vituo vya Karantini kwa wagonjwa wa Ebola hususan wa Marekani kutibiwa nchini Kenya.
Lakini wakati hayo yakijiri mahakama ya Kenya iliweka zuio la muda kuendelea kwa mpango huo baada ya madai yaliyowasilishwa na Katiba Insitute wa kuupinga mpango huo hadi pande zote mbili zitakaposikilizwa, vyanzo viliripoti Mei 29, 2026.
Madai
Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo X na Instagram kumekuwa na picha pamoja na video zinazosambaa zikidaiwa kuwa ni wagonjwa wa Ebola wa Kimarekani wakipokelewa katika uwanja wa ndege nchini Kenya.
Uhalisia wa madai hayo.
JamiiCheck imefuatilia na kujiridhisha kuwa picha hizo pamoja na video hizo si halisi na badala yake zmetengenezwa kwa Teknolojia ya Akili Unde (AI)
Picha na video hiyo zina baadhi ya dosari mathalani watu wenye muonekano wa kimasai wanacheza bila kuwa na kinga zozote ukilinganisha na matakwa ya afya dhidi ya kujikinga na ugonjwa huo. Aidha kuna 'logo' inayoonesha kuwa imetengenezwa na nyenzo hiyo ya AI.
Aidha ufuatiliaji kwa kutumia nyenzo za kidigitali pia umebaini kuwa video hiyo ina viashiria vya kuundwa ka wa teknolojia ya Akili Unde kwa Takribani 78.4%.