Alafu hio link ulio ileta ni summary haina content yeyote, nitakusaidia kwa ku post original article ya Ndii, enda ukaisome vizuri
Open Letter to President Uhuru Kenyatta
Hapo amesema sababu kuu ya Germany kutokua na vifo vingi licha ya wao kua na kesi nyingi za corona ni kua Germany wako na ICU beds nyingi kushinda Italy na France...
Ukiangalia takwimu za vifo, Ni kweli kwamba Germany iko na vifo vichache licha ya kua na kesi nyingi za corona kuliko nchi kama France na Italy.
View attachment 1399338
Lakini ukitafuta hizo data za ICU per 100,000
View attachment 1399340
USA iko na vitanda vingi vya wagonjwa mahututi kuliko nchi yoyot ile lakini tayari wengi wamekufa kuliko Germany, Alafu ukiangalia hapo Italy ni ya tatu duniani kwa kuwa na vitanda vingi vya ICU mbona wamekufa wengi zaidi ya nchi nyengine duniani? na vipi China ambao wako nyuma ya Italy na Spain kwa vitanda, mbona wameweza ku contain usambazaji na vifo???
David Ndii aliangalia na akachagua kutumia huo mfano wa Germerny na Italy maksudi kwasababu ulikua unaendana na hoja yake ambayo alikua anataka kuonyesha kwamba Kenya haina vitanda vya kutosha kwa wagonjwa mahututi. Hii ndo maana hua napenda kuambia watu mkisoma taarifa zengine hata ziwe zimeandikwa na nani, soma kisha ufikirie mwenyewe (think for yourself! mungu alikupa akili), kama mtu ametaja kitu flani chunguza kivyako kama ni kweli, usikue una download habari tu na kuamini kila kitu kwasababu alie andika ni mtaalam, unaweza kua manipulated hadi ukaamua kuua kakako kwasababu mtaalam alisema hivyo ndo sawa kulingana na takwimu zake.
Na saa zengine uache kuwashwa na pilipili usio ila, David Ndii alikua anakashifu Kenya.... sasa wewe unacheka kwasababu anakashifu uongozi na serekali ya Kenya kana kwamba hali ni shwari Tanzania....... Mimi hua nawaambia kila siku, Tanzania hamna wanahabari, hamna watu jasiri walio na akili ya kuchunguza na kuuliza maswalimuhimu kwa serekali ya siku mumeachia hio kazi kwa viongozi wa upinzani, wanasiasa ambao wako na malengo yao.
Tanzania iko na ICU kidogo kuliko Kenya.
Tanzania iko na hospital beds kidogo kuliko Kenya..
Lakini hautaona mwanahabari yeyote huko TZ ana thubutu kuuliza maswali muhimu kama hayo ambayo Ndii anauliza , kazi yao ni kuripoti ni yepi ambayo magu ametamka leo.
------
Lakini kwa upande mwengine, na support hayo mawaidha ya Ndii ya kwamba Serekali ikabe matumizi na ifutilie mbali mipango kadhaa ya kiserekali ambayo si muhimu kwa sasa hadi serekali ibaki na angalau $1B ambazo zitatumika kwa economic stimulus program baada ya janga la corona kuisha ili kufidia wanabiashara na kufufua viwanda, ma kampuni na uchumi kwa jumla.Yani hizi $1B itakua ni pesa zinaenda kwa mikononi mwa watu na biashara ili warudi kwa hali ilio sawa baada ya kufilisishwa na matukio yanayofanyika sasa....