Wakenya wanaolalamika kulipwa 2USD kwa Saa kuifundisha AI wapo Sawa kutupia lawama Kampuni Husika, au wawalaumu Watunga Sera wao kuwafanya desperate ?

Wakenya wanaolalamika kulipwa 2USD kwa Saa kuifundisha AI wapo Sawa kutupia lawama Kampuni Husika, au wawalaumu Watunga Sera wao kuwafanya desperate ?

Logikos

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Posts
15,460
Reaction score
24,233
Nimeona hio Documentary ya 60 Minutes; Kwa ufupi AI inahitaji kuwa trained ili iweze kugundua vitu kama picha, watu emotions n.k. Sasa Serikali ya Kenya imekuwa ikivutia makampuni kuja kuwekeza Kenya kwamba watu wana knowledge na labor ni cheap (kama walivyokuwa wanakwenda sana nchi kama India)

Sasa nimesikia hawa jamaa wanasema kwamba wananyonywa kwa kulipwa 2USD kwa saa sababu USA kazi kama hio mtu angelipwa 30usd..., na kuna mikataba imeonekana kampuni kubwa zote zinatumia middle man ndio afanye kuajiri sasa unakuta kampuni inalipwa 12 usd, na wao kulipa 2USD.., Je huu ni wizi au huenda nao wana costs zao za hapa na pale ?

Nadhani cha kujiuliza hio 2USD inaendana vipi na wengine wanalipwa ngapi katika mazingira yenu na sio nani analipwa ngapi nchi nyingine....

Nadhani watu inabidi tuelewe when it comes to Capitalism Kampuni ipo answerable kwa shareholders na ni profit at all costs..., na hata ukilipwa nyingi tambua hawawezi wakapata ndogo au wanaogopa bad publicity (if they can pay you less they will...,

It's the nature of the beast)...; Kwahio wasilaumu kampuni ambazo zipo pale kupunguza costs; bali watunga sera wao kwa kuwafanya kuwa desperate na kukosa ujira hivyo kufanya lolote kwa chochote.


View: https://youtu.be/qZS50KXjAX0?si=Aa02tUevll3cOe8q
 
2 usd sawa na elfu sita kwa saa
akienda saa 8 ana 48,000 kwa mwezi ana milioni moja na laki kadhaa..

nje ya 2usd per hour upewe Chakula, Nauli na vi allowance vya hapa na Pale..

Kibongo bongo Ni hela nyingi

Hio Fursa ikija bongo siilazii damu wala kulalamika
 
2 usd sawa na elfu sita kwa saa
akienda saa 8 ana 48,000 kwa mwezi ana milioni moja na laki kadhaa..

nje ya 2usd per hour upewe Chakula, Nauli na vi allowance vya hapa na Pale..

Kibongo bongo Ni hela nyingi

Hio Fursa ikija bongo siilazii damu wala kulalamika
Na hio ndio point yangu kuu..., badala ya kuleta Documentary wakenya wananyonywa na hizo kampuni za ulaya wangeleta documentary jinsi viongozi (walamba asali wanavyoshindwa kuwasaidia watu wato kupata ujira hadi kufanya kazi barabarani (machinga sehemu hatarishi) au mtu anatembeza njugu siku nzima wakati mtaji wake / mzigo wote kwenye beseni hata buku kumi haufiki.... Na kumbuka hawa wanachofanya ni repetitive manual work.., sio kwamba wapo Studio wanaandaa a masterpiece (mfano wasanii wakisema wanalipwa pesa ndogo kulingana na mzigo unayouzwa sokoni na ni yeye ndio amesababisha 100 percent ya mzigo)

let's look things in perspective....
 
Hio Fursa ikija bongo siilazii damu wala kulalamika
Jamaa wameona fursa wanawashitaki Meta kwa unreasonable working conditions, kuna kipindi walikuwa wanaona porno, images za kutisha, child abuse n.k...., kwahio wewe mdau unasema wasogee tu hapa Bongo tupunguze wauza karanga kitaa ?

Au na wewe utapiga miezi kadhaa alafu ucheki fursa ya kuwashitaji huenda ikakupatia kiinua mgongo ?
 
Back
Top Bottom