GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Kwa nini nauliza hayo?
1. Inasemekana, miaka ya nyuma, kabla ya Magufuli na hatimaye Samia kuingia madarakani, Wakenya walikuwa wanaingia Tanzania na kununua viazi mviringo na kuvipeleka Kenya. Vikifika huko, havipelekwi kwa Wakenya, bali husafishwa vizuri na kisha kuwekwa kwenye vifungashio vyenye nembo ya Kenya na kisha kupelekwa ng'ambo, hasa Dubai!
2. Inasemekana, miaka ya nyuma, japo Kenya haijawahi "kulima" Tanzanite, lakini ilikuwa ikifahamika kama moja ya nchi zinazoexport Tanzanite duniani!
3. Inasemekana, ni Wakenya ndiyo waliokuwa watu wa kwanza kuanza kusafirisha kwenda ng'ambo parachichi za Njombe. Walikuwa wakizifuata mashambani Njombe, wanazipeleka kwanza Kenya kuzipaki na kuzipiga chata ya Kenya hivyo kuonekana zimezalishwa nchini Kenya! Hata sasa, kuna Kampuni za Kikenya zianzofanya biashara ya kusafirisha parachichi kwenda nchi za nje. Pia, kuna Wakenya walioingia ubia na Watanzania wakaanzisha mradi wa kilimo cha parachichi Njombe!
4. Inasemekana, wakati watoto wa Kikenya wakipelekwa shuleni kwa lengo la kusoma na kuelimika, wa Kitanzania hupelekwa shuleni kwa lengo la kukua kiumri na kumaliza madarasa aliyopangiwa!
5. Inasemekana, hata waandishi wao wa habari wanao uweledi kuzidi wa Tanzania! Kwamba, hata vipindi vyao vya runinga na redio vinavutia kuvifuatilia kwa sababu vinaandaliwa kwa ubunifu wa hali ya juu tofauti na vya wenzao wa Tanzania!
6. Inasemekana, makampuni yao ni mengi sana nchini Tanzania ukilinganisha na makampuni ya Watanzania nchini Kenya!
7. Inasemekana, ingawa Tanzania inaizidi Kenya kwa ardhi kubwa na nzuri kwa kilimo, lakini bado Kenya inaizidi Tanzania kwa kusafirisha kwenda nchi za nje mazao mengi ya matunda, maua na mboga mboga!
8. Inasemekana, kama siyo Serikali ya Tanzania kuwabana wachimbaji wadogo wa dhahabu, wengi wangetamani wakauzie dhahabu yao nchini Kenya badala ya Tanzania!
Mengi yanasemwa kuwahusu WaKenya!
Je! Watanzania hawawezi kuyafanya hayo yanayofanywa na Wakenya? Wametuzidi kipi hasa?