Wakenya watupa vijembe kwa Diamond. Wasema WASAFI FESTIVAL ilikuwa ya kipuuzi, Wajutia kuharibu pesa yao

Wakenya watupa vijembe kwa Diamond. Wasema WASAFI FESTIVAL ilikuwa ya kipuuzi, Wajutia kuharibu pesa yao

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

'kwamba nianze kuimba wakati wewe ndo mwanamuziki '.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndio mkuu wakenya wana-mind vibaya yani,wao wamezoea live show,sasa ndugu zetu wameenda kufanya show kama wanavyotufanyiaga huku bongo...
 
Tuweke ushabiki pembeni kwa faida ya muziki wetu ni lazima tubadilike, Live iwe kweli Live tuachane na playback. Ni lazima tubadilike sio kila jambo ni chuki ila ukweli ni kuwa tufanye live perfomance na hii itawaondoa wenyewe wasio kuwa wanamuziki wataondoka tu. wabaki wanamuziki wa kweli. Mimi binafsi sitoi pesa kuingia kwenda kusikiliza CD na kupiga kelele nataka nishangilie bila kuambiwa ni kama mpira mkicheza vizuri tutashangilia. shoo za playback kapige vijijini huko low cost lakini ukienda cities piga live music na band.
 
Unajua nowadays mziki uko fake sana. Studio ndo zinamaliza utamu wote.. ngoma nyingi mpaka za mbele zimebebwa na studios tu. Tofauti na akina Fugees na huko nyuma kabisa akina ABBA. So ukisema uimbe ngoma yako uloinogesha na Beats za producer mkali ukaiimba na Band eti ni hatari sana. Lazima uwe fundi sana

Sent using Jamii Forums mobile app
100% true studio anaweza kukaa siku nzima anaingiza sauti na hapo inachujwa na uhakika hata mimi nikiingia studio nitatoa ngoma hit ila ukiniambia imba live nitakimbia.
 
Nimesikitishwa sana, sio kwa comments za wakenya bali kwa muwakilishi tunayemtegemea kwenye mziki kimataifa kufanya show mbovu,iliokosa maadili kama ile. Jamaa kafikia hatua anakatika jukwaani wanawake Wanamchezea matako!!
Personally ameniangusha sana.

Kweli anguko likianza kukunyemelea mambo yanaanza kuwa hovyo hovyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mchicha mwiba yule .. kwani hamjui !? Hahaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajua nowadays mziki uko fake sana. Studio ndo zinamaliza utamu wote.. ngoma nyingi mpaka za mbele zimebebwa na studios tu. Tofauti na akina Fugees na huko nyuma kabisa akina ABBA. So ukisema uimbe ngoma yako uloinogesha na Beats za producer mkali ukaiimba na Band eti ni hatari sana. Lazima uwe fundi sana

Sent using Jamii Forums mobile app

Big up, wewe unajuwa kanuni za muziki. Order chochote hapo ulipo nakuja kulipa.
 
Back
Top Bottom