Hebu weka huu uzi palipo Watanzania, kwa mfano uuweke kwenye majukwa ya Watanzania humu JF uone mziki wake, utatukanwa hadi ukimbie.
Watu nje ya nchi ya Tanzania hutegema kusoma yaliyo kwenye magazeti yenu ambayo kutwa yanaimba mapambio ya sifa, maana pakiibuka mwandishi asiyeimba sifa anakumbana na masaibu kama tunayosma kuhusu huyo Kabendera, nimesoma sehemu mumemfungulia mashtaka ya uhaini kisa tu kaandika, jameni uhaini adhabu yake kifo, dah huko kwenu balaa.
Kwa kifupi comments za watu nje ya nchi wanaotegemea kusoma magazeti sio kipimo bora, MaCCM mnafaa kuangalia upepo kwenu ndani, je Mtanzania wa kawaida anasemaje, comments zake ziko vipi ukimpa uhuru wa kusema, tatizo pia kwenu mumezuia wapinzani wasiongee, wakikusanyika hata watano wanapokea kibano, ilhali MaCCm wenyewe hata halaiki mnakusanyika, kutwa mpo kikampeni zaidi. Niliona uzi humu hata polisi wanahutubia na kusifia kwenye mkutano wa CCM.